Maoni: Samatta ni mzigo Taifa Stars, aondolewe

Mbwana hata genk huwa ni bahati tu inamuangukia ya kufunga. Lkn huwa sioni km ni mchezaji wa kiwango kikubwa km tunavyoaminishwa!! Mbwana hawezi kucheza England hata division 1. Hakuna timu ya England inayoweza kumnunua!!
Mkuu kama unamfatilia ni mchezaji mzuri mkuu kwa hilo tumpe haki yake.
 
Sasa we unafananisha viungo wa Genk na Tanzania? ndugu mpira unaangalia au unasimuliwa? Tanzania Samatta mwenyewe inabidi aongezeke kama kiungo pale katikati genk kule anasubiri kutengenezewa tu muda wote na pasianazipata sasa wewe unataka kufananisha mpira wa Ulaya na Afrika? mpira wa ulaya akili nyingi Africa tunakamiana mtu hadi uivuke safu ya ulinzi umefanya kazi... Mi nashangaa Egypt hawamlaumu sallah wakati kiwango anachocheza sallah egypt si kama kile cha liverpool lakini wanaelewa ila huku mbongo mmoja asiye na simile anamwaga tu maneno ya hovyo kama anatoa posho taifa stars kumbe hamna kitu
Kuwa mtu mzima mkuu. Timu inaendeshwa kwa kodi zetu.
 
Samatta hana la kupoteza ndio maana akija timu ya taifa hajitumi anacheza hovyo tu kuogopa majeruhi.

Kuna mechi taifa stars walishinda bila yeye asituletee u-star wake, mtu ligi kubwa anafunga magoli, UEFA hadi Liverpool anafunga ila mechi ya timu ya taifa anafunga penati tu, hata nusu ya Msuva hafikii hiyo namba 10 apewe hata hajibu.

Bro Samata hakuzaliwa kuichezea Stars mkiona hafai achaneni nae aendelee kutafuta maisha ulaya.

..........Wabongo tuna degree nne za kulalamika na kulaumu ila hatuwezi kufanya hata robo ya walivyofanya wenzetu.
 
Kuwa mtu mzima mkuu. Timu inaendeshwa kwa kodi zetu.
Kwahiyo kama inaendeshwa kwa kodi ndo mfanye iwe sehemu ya majaribio leo acheze huyu kesho yule? kocha ana mipango yake ila kama samatta anaona hii comment yangu namshauri ajiachie tu akapambane zake ulaya
 
Ni muda sasa wakuacha kumuhusudu mbona kina aishi manula wameachwa hata yy apigwe chin t hamna analofanya tim ya taifa
 
Mbwana hata genk huwa ni bahati tu inamuangukia ya kufunga. Lkn huwa sioni km ni mchezaji wa kiwango kikubwa km tunavyoaminishwa!! Mbwana hawezi kucheza England hata division 1. Hakuna timu ya England inayoweza kumnunua!!
utakuwa mgonjwa ww bahati ya kupiga goli34 kwa msimu hiyo ni bahati ya aina gani? wewe ukipata bahati ya cross kama ile ya genk vs liverpool unaweza kupiga kichwa kama kile? hebu ongea hoja za msingi kama unamchukia tafuta sababu nyingine ila siyo hii ya kubahatisha
 
Lakini Kwa mechi ya Jana,aisee Samatta alizingua kiukweli kabisaaa,tuache kupepesa macho
amezingua kwa lipi hasa? washambuliaji walikiwa ditram na msuva yeye amecheza kama kiungo kati ya viungo na washambuliaji kazi yake hajaifanya?
 
Hata mimi naona majukumu ya timu ya taifa hayatekelezi ipasavyo kwa kujitoa kama wachezaji wengine wakubwa wa kiafrika wanaocheza ulaya yeye anatakiwa kuwa mfano kwa kujituma ipasavyo katika timu ya taifa ili na wengine wajifunze angalia kina mane wanapokuja katika timu zao za taifa nini wanafanya au wachezaji wakubwa wa afrika magharibi wanavyojitoa na kujituma kwa nchi zao. Hata ronaldo wachezaji anaocheza nao timu ya taifa hakuna anaenusa kiwango chake au umuhimu wake katika dunia ya michezo lakini anajitoa katika timu yake mpaka anaumia kwa kuipambania nchi yake japo haiwezi kumlipa kama klabu yake sembuse ije kuwa samata eti anaogopa kuumia?.
 
Namuhusudu sana ila kwa mwelekeo wake kama Captain kwa sasa, nampa mechi ijayo ya mwsho vingenevyo natoa shillingi sijaona jipya wala juhudi ya dhati hadii sasa
 
amezingua kwa lipi hasa? washambuliaji walikiwa ditram na msuva yeye amecheza kama kiungo kati ya viungo na washambuliaji kazi yake hajaifanya?
Si Kwa ukamilifu ukilinganisha na kina alilo nalo na umuhimu wa mechi yenyewe. Alikuwa anapoteza mpira kiurahisi saana na hata kujituma kwake hakukulingana na thamani yake na hata thamani ya nchi yake.
 
Namuhusudu sana ila kwa mwelekeo wake kama Captain kwa sasa, nampa mechi ijayo ya mwsho vingenevyo natoa shillingi sijaona jipya wala juhudi ya dhati hadii sasa
Kiukweli hata Mimi nakubali saana juhudi zake hata kufikia hapo alipo,ila kwa mwendo anaokwenda nao timu ya taifa...hapana
 
Samatta hana la kupoteza ndio maana akija timu ya Taifa hajitumi anacheza hovyo tu kuogopa majeruhi.

Kuna mechi Taifa Stars walishinda bila yeye asituletee u-star wake, mtu ligi kubwa anafunga magoli, UEFA hadi Liverpool anafunga ila mechi ya timu ya Taifa anafunga penati tu, hata nusu ya Msuva hafikii hiyo namba 10 apewe hata hajibu.

Mpira wa Miguu ni mchezo wa timu nasiamini kama Samatta peke yake anaweza fanya miujizabila kusaidiana na wachezaji wengine katika timu. Mnapomlaumu yeye peke yake katika position yake pasi na kuangalia wachezaji wengine wanafanya nini kuhakikisha kwamba Samatta anafanya va katika nafasi yake.

Jambo jengine ni kwamba, yeye akiwa kama Nahodha wa timu ana jukumu lingine kubwa ambalo linahusiana na kuleta “team morale” as a player and a leader. Je hivyo anafanya?

Mnafananisha na namna anavyocheza akiwa Genk, well jaribuni kuifikiria timu ya Taifa kama mashine, ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi, he sio muhimu kwamba part zote za gari ni lazima ziwe zinafanya kazi kwa usahihi? Tunafikiri kwamba timu yetu ni hiyo perfect machine?
 
Samatta tatizo lake anajiona mzungu.. anazingua sana.... nadhani jambo la kwanza asiwe captain.. kwa sababu captain gani analeta mizaha kwenye mambo serious?

Tatizo wanajisahau kama wamebeba bendera ya taifa, wakumbuke kuwa wao ni taswira ya nchi, nawashauri wasichukulie kwa kuwa hii ni michezo basi wadharau, wawe serious. Mnatuumiza mnapocheza chini ya kiwango na wengine mkionyesha kutojali.
 
Sasa kama amefanikiwa, akae pembeni awaache wenzake wanaotafuta mafanikio sio kucheza yekeyeke
Kawambie Messi ,Ronaldo ,Mane,Salah hawana msaada team zao za Taifa ,wanavyocheza kwenye vilabu tofauti na team zao za taifa.
 
Ndo maan baadhi ya players hua wanasusa kuchezea timu za taifa kwa position ya second striker ni ngumu kidogo kufunga mara kwa mara pia upande wa kiungo mkabaji palikua pamepwaya kina sure boy walkua wameng'ang'ania mbele tu but watu kama hawa Mudathir yahya,mkude,feisal na ajibu sio wakuwabeza upande wa kati tackling za feisal unafikiri angetembea nani pasi za mwisho za ajibu unafikir samata angeshindwa kutupia
 
Haki watanzania hatuna jema hata siku mojaaaaa timu ikishinda ndio kila mtu mzuri ikishindwa mnamtaja kocha au samatha duh kwa kweli tutashindwa cku zote. Km mnaanza kuleta maneno atatokaa na mtabaki mkiruka kiruka tu maneno yametuzidi mno watz hatuna jema hata kidg ni kuongeaaa tu na kukatishana tamaaa
 
Back
Top Bottom