MAONI:. Ndoa ,,, Waislam vs Wakristo

Status
Not open for further replies.
Hiyo ndoa ni "Najisii" hadi Qiyama....!!
 

Nakukumbusha kaka angu katika imani. Hii hapa aya suratul Nisaa aya ya 34 "arijalu kawamuuna alaa nisai......" "Wanaume ni walinzi wa wanawake, kwa sababu M.mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojihifadhi hata wasipokuwepo waume zao, kwa kuwa mungu amewaamrisha wajihifadhi......"
 
Asalaam 3aleykum W W... Ndugu Mpendwa, Kila mwanaAdamu ana kasoro zake na upungufu wake katika kutii Amri za moula wetu Karimu Moula wetu rahimu Mwenye Rehema na Misamaha mingi na mwenyeEzzi Mungu ndo alokamilika.!! mimi na wewe na viumbe vyake tumekuwa tukihalifu na kutenda dhambi nyingi.... Lakini MwenyEzzi Mungu ni ------ (mvumilivu) na hutupa Time na kupokea TOBA (repent) na milango yake huweka wazi kwa yule atakae rudi au muombaji msamaha.
Ofcoz. kukosea ni ubinadamu na sote huteleza katika maisha... Lakini tumepewa chance ya kuomba MAGHAfirrah na kujirekebisha (corrections). kila mjjaa ata hesabiwa kwa yake na siyo aliyoyatenda na hatoshirikishwa na Hesabu za wengine !! Hiyo tafadhali ijue "You & me will be accounted by our deeds" hakuna nafasi ya kuExplain watu waivyo kuwa wakifanya au nchi/Maisha zilivyokuwa zikiendeshwa. " Vitabu/Amri alivyoteremsha Allah ni vile vile NO change "tangu enzi na hadi End of the Day. Siye ndiye hupindishapindisha. Kwa Heshima na taadhima kwako Rehema,Baraka (mke,watoto,Mali,Maisha yote) za Moula wako ni zako na kwa sababu yako. THE DOORS are open and thers enough space for all. ALLAH bless you and Umma.AMIN
 

Na kinyume chake ni sahihi, hata sisi wakristo hasa Roma mzazi akimuozesha mwanae kwa Muislam (Kwa kuchukua mahari) anafungiwa
 
Aleikum Salaam Ndugu Life is Short. Nimependezewa na jibu lako sana. Sisi binadamu WOTE tuna kasoro na wote tuna dhambi. Lakini mimi naambiwa kuwa sio Mwislamu kamili kwa kuwa sifungi, hio ndio ilikuwa point yangu na wewe umeshanijibu kuwa hamna binadamu asiye an kasoro. pale ambapo atatokea binadamu asiye na kasoro ndio nitaweza kuitwa na Waislamu wenzangu kuwa nipo gizani au Mwislamu wa jina na kadhalika. Nyosha mkono kama unafuata sharia ZOTE za dini yako halafu una ruhusa ya kuniita chochote upendacho. Usifanye masihara na Sharia Law!
 

Waalaykum msalaam. Kwanza mkuu mimi sijasema kuwa mimi ni muislamu kuliko wewe. Nilichosema mimi ni kuwa, kwa wewe kutangaza hadharani kuwa hujafunga kwa miaka 10 kwa kuwa tu umeamua hivyo (Kumbuka hukutoa sababu yeyote ya msingi). Zaidi ya hapo ukaongeza kuwa huna mpango wa kufunga kabisa, hapa kwa mujibu wa taratibu na sheria za kiislamu sidhani (makusudi kabisa nimetumia neno sidhani, hata ukirudi kwenye ile posti yangu ya kwanza ndilo neno nililotumia) kama unaweza kusimama mahali na kuusemea uislamu. Hii ni kwa sababu japokuwa uislamu una mambo mengi, lakini funga ni nguzo ya tatu ya uislamu na funga ni moja ya ibada ambayo imesisitizwa sana katika uislamu na ghadhabu anazopata M'mungu kwa mtu kuacha kufunga kwa makusudi ni kubwa mno. Hivyo basi mtu anayeacha kufunga bila sababu ana walakini sana na imani yake juu ya uislamu wake. Kumbuka kuwa si mimi nayehukumu hapa, nilichofanya mimi ni kukupa tu msimamo wa uislamu juu ya kuacha kufunga bila sababu. Unaweza ku-google hapo kwa maelezo zaidi juu ya kuacha funga. Kumbuka pia kwenye uislamu dhambi hazilingani, kwa mfano kuua si sawa na kumtukana mtu.

Halafu mkuu kuwa kwangu muislamu mbaya hakuwezi kuhalalisha wewe kuwa mbaya vilevile. Pili dini si sharia peke yake. sharia ni sehemu ya dini. Uislamu ni mfumo wa maisha wenye kila kitu. Kuhusu vijana wa Saudi, hapo kuna mkorogo wa mambo mengi na sidhani kama hapa ni mahali pake. Duniani leo kuna matatizo mengi sana ambayo kama tukianza kuyajadili hapa hatuwezi kumaliza. Nafikiri ni busara zaidi tuendelee kubaki kwenye mada husika japokuwa kwa kiasi fulani naona kama tunatoka.

Mkuu kwa nini unanisemea mambo ambayo huna uhakika nayo. Maana umeshasema nampeleka mke wangu akapewe dawa ya mimba, nakula riba wakati hata hunijui. Tufanye basi labda nafanya hayo mambo. Lakini kama umesoma vizuri pale juu nimekwambia kwamba Allah(sw) anatambua watu tunafanya makosa na ndiyo maana milango iko wazi kwa waumini kutubia na kuomba msamaha. Hicho ndicho kinachotufanya sisi binadamu. Ndiyo maana kuna hadi aya, Allah(sw) anasema, "Kama mngalikuwa ninyi binadamu hamfanyi makosa, basi ningeliwaondoa na kuwaleta wengine wanaokosea na kuomba msamaha" (Siyo tafsiri rasmi, bidodo kama unaweza tusaidie na hii tafadhali). Kwa hiyo basi naweza kuwa nafanya hayo lakini nina nafasi ya kutubu na kutaka maghfira.

Kuhusu suala la sheria za dini kupitwa na wakati, dini ni hiari na uislamu haujapitwa na wakati. Huwezi kudai wewe ni muislam halafu wakati huo huo unaukataa huo uislamu. Huu ni mkanganyiko wa aina yake, nimesema hapo kuwa unaweza kuacha uislamu kama huridhiki, ni hiari si lazima.

Mkuu binadamu hatujakamilika na tunabadilika, mimi siwezi kujiona bora kuliko yeyote. Hata kama mimi ni bora kuliko wewe sasa hivi kitu ambacho siwezi kujua wala kuwa na uhakika nacho, lakini nitajuaje kama wewe kesho utakuwa bora kuliko mimi. Allah(sw) anatuambia ni kwa rehma zake tu mtu anaweza kumtii na kufuata haki, si ujanja wetu. Na ukifikiria kwa makini, hii kitu ina maana sana, maana mtu hajichagulii anachoamini. Ni kama vile mtu anajikuta tu anaamini kitu fulani. yaani hatuna udhibiti kabisa wa imani zetu na ndio maana sisi waislamu tunatakiwa kumshukuru Allah(sw) kwa neema hii kubwa ya kuwa waislamu

Allah(sw) atuongoze sote katika nuru na njia ya haki....Amin.
 

Mkuu japokuwa uko sahihi lakini kuna vitu ambavyo vimeshakatiwa shauri katika dini. Huwezi kupinga aya ya M'mungu wazi wazi na kuita ni ujinga halafu uendelee kuwa muislamu. Na hii haina maana kuwa anayekwambia ukweli huo ni muislamu saaaaaaaaaana. Huenda hata yeye ameshakufuru ila hajui tu, lakini hilo haliondoi ukweli kuwa hata wewe umekufuru. Upo hapo mkuu??
 
Katika ukoo wetu hamna aliyeoa wala kuolewa na muislamu. Hivyo kusoma hii mada ni burudisho sana.
 
binti mkristo kuolewa namwislam ni dhambi yamauti,hujiamulia hilo wenyewe bila ridhaa ya kanisa au wazazi.uchunguzi tuloufanya-rc-unaonesha vijana wakiislam huoa wakristo kwa sababu tatu muhimu.1~binti mkristo kafundishwa kuwa ndoa niyamilele hakuna talaka hadi kifo,jambo ambalo mwislam halipati kwabinti mwislam kwakuwa kafundishwa kuwa mkishindana taraka ruksa,hivyo hukaa kimtego tu kwamume akijua wakati wowote taraka sababu hata ktk harusi inaagizwa siku ileile.2~huamini kuwa kuoa binti mkristo na kumfanyakuwa mwislamu hupata thawabu kwa molawao.3~baadhi ya mashirika yakidini toka Iran,yanatoa zawadi (pesa)kwa vijana wakiislam watakaowatia mimba,au kuoa binti zakikristo,kwakuwa mtoto atakaezaliwa atakuwa mwislam.
 
Mungu ndo huyo huyo mmoja ispokua nyie mmekufuru pale mliposema Jesus ni mwana wa Mungu na kumtukuza kiumbe wake kama Mungu. Mungu ni mmoja wala hakuna aliyefanana nae, Hakuzaa wala hakuzaliwa. Kiufupi nyie mna dini yenu na sie tuna dini yetu

uko sahihi mkuu ila usibishane na waliokufuru waeza jiingiza kwenye kufuru pasi nawewe kujua,,..cz wengi wao humu ni mashabiki tu na hawako tayari kujifunza so ni vema ukawa kimya usije haribu swaum yako bure!! rejea (surat baqarah aya ya 138)
 
Mungu ndo huyo huyo mmoja ispokua nyie mmekufuru pale mliposema Jesus ni mwana wa Mungu na kumtukuza kiumbe wake kama Mungu. Mungu ni mmoja wala hakuna aliyefanana nae, Hakuzaa wala hakuzaliwa. Kiufupi nyie mna dini yenu na sie tuna dini yetu

tumemtukuza kadirir ya uislamu au ukristo
 
Katika ukoo wetu hamna aliyeoa wala kuolewa na muislamu. Hivyo kusoma hii mada ni burudisho sana.
Oh my Dear BJ,
MaShaallah, naona unabweteka na unasikia raha.... Sawa sote tupo kwenye mgongo ardhi hii jitaarishe kesho kijana handsome religious young Muslim atafanya ziara kwenu licha ya kuoa tu, atafungua milango na madirisha mupate mwangaza atasilimisha wanyumbani wote na mutaburudika zaidi, in-ShaAllah.
kila la heri.
 
Mjasiria, Salaam Aleikum, Shukran kwa majibu yako. Nimekuelewa. Naomba samahani kama unafikiri nimetoa mfano mbaya kama nilitumia mfano wa mke kutumia dawa ya kuzuia mimba. Nia yangu sio ya kuvunja heshima yako wala ya mkeo (maka umeoa) ila kuonyesha kuwa sisi binadamu tuna kasoro. Mimi kama wewe, nimepita madrassa na naifahamu dini yangu na najua sharia muhimu za dini yetu. Nadhani ni muhimu kuachana hapa kwa heshima kwa kuwa hatutaonana macho kwa macho na pointi tunazozichambua. Japokuwa nina dhambi zangu naamini kuwa mimi naishi kwa kusaidia wasiojiweza, naangalia familia yangu na kuheshimu wazee wangu na marafiki zangu, natoa zakat naswali vile vile, lakini napinga kabisa kuwa kuna binadamu hapa duniani anaweza kuniambia kuwa mimi si Mwislamu bora kwa kuwa sifuati baadhi ya sharia za dini. Hapa ndio kuna utata. Kama hamna mtu anayeweza kuishi na kufuata sharia zote za dini, basi hamna mtu ana haki ya kuniambia mimi sio mwislamu kamili na kadhalika. Naomba radhi kama nimesukasirisha au kutokupa heshima unayostahili, lakini point yangu iko pale pale. Mimi naweza kuwa Muislamu kama wewe na Mola peke yake ndio anajua, hapa duniani hakuna mahakama itayonihukumu na dhambi zangu. Na wale Waislamu wanaopenda kuwasaidia wenzao kuona njia na uwanga, basi wawe tayari kunyosha mkono na kusema mbele ya Mungu wao kuwa , ndio, wao wamefata SHARIA zote za dini. Nasema baadhi ya sharia ni za kale sio kwa kutoheshimu sharia za dini ila katika maisha haya ya karne ya 21, asilimia ngapi unafikiri ya Waislamu wasiotumia madawa ya kinga ya mimba, hawapokei riba, hawanywi pombe na wanasali sala tano na kufunga? Sasa atakapovunja sharia hizo, kwa nini wao ni Waislamu zaidi kuliko mimi? Tusichambue sharia, aidha tunazifuata au hatuzifuati. Hata nchi zenye wananchi wengi wa Kiislamu wanashindwa kufuata Sharia law kama ilivyooandikwa katika Quran Tukufu, kwa sababu gani unafikiri?
 

Hii dua kiboko!
 
uko sahihi mkuu ila usibishane na waliokufuru waeza jiingiza kwenye kufuru pasi nawewe kujua,,..cz wengi wao humu ni mashabiki tu na hawako tayari kujifunza so ni vema ukawa kimya usije haribu swaum yako bure!!

ukweli nikuwa MUNGU tunayemwabudu sie wakristo tangu mwaka 33bk ilipoanza RC,siyule anaeabudiwa na waislamu tangu mwaka 570bk ulipoanza uislam,nadaima mwislam ndo hutangaza kwamba Mungu ni yuleyule ili kuficha mengi yaajabu ndani ya uislamu,mfano wawazi mwislamu anaamini kuwa peponi munguwake atampa zawadi ya mke bikra,tena maraika,wakati BIBLIA itakataa hayo na kusema mambo yakuoa na kuolewa ni yahapa duniani tu.
 
bidodo@@,,...nimesoma comments zako zote,,..hongera sana Allah azidi kukuzidishia elmu(Rabbana zidna ilma) umejitaidi kuelimisha kwa qadri Allah alivyokujalia but stil watu nafsi zetu ngumu na tumekua wagumu kukuelewa na kuanza kukufuru,,.. Ivo usiumize dole gumba lako au kuzichosha keypards zako kwa nafsi nzito zenye makongwa shingoni mwetu tumeekewa vizuizi mbele yetu..nyuma yetu n.k.(surat ya sin aya ya 10) inasema,,...:Ni Sawa Kwao Ukiwaonya Au Usiwaonye,Hawataamini::,,..ivyo tumuachie Allah afanye kazi yake,,..na kamwe usilumbane na asiekua na elmu ya Allah SW)),,...Jazaka llah kheiry,,.... @"BIDODO"@
 
Last edited by a moderator:
..na kamwe usilumbane na asiekua na elmu ya Allah SW)),,...Jazaka llah kheiry

bora umemuonya mapema asijeuona mwanga,akamjua MUNGU waukweli akafika mbinguni,bora umzuie muangamie wote jehanum.
 
Hebu nipe source ya haya maelezo yako

Kama unajua kiarabu soma kwanza biography ya mtume muhamed.
Ukitoka hapo soma quran.

Ukisha maliza soma Torah, ambacho kitabu cha mungu cha myaudi.

Ukisha toka hapo soma bibilia, ya kisasa.

Hapo utakua haudanganywi na mtu tena.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…