Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
MAONI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Watu wajiepushe na kumponda Magufuli maana aliyoyafanya hayahitaji Maelezo mengi bali yalionekana Physically sasa Hawa watu huenda wakajikuta kwenye wakati Mgumu sana 2025, Nguvu ya umma sio ya kubeza hata kidogo,Mwaka 2015 ilikuwa CCM vs UKAWA usijeshangaa Mwaka 2025 ikawa CCM vs WANANCHI.

Mimi kama mwananchi na mwanaCCM nakumbuka ilivyokuwa ngumu kuiuza CCM mwaka 2015 kiasi ambacho hata wafanyakazi wa CCM waliogopa kuvaa sare za chama hata walipokuwa ofisi za Lumumba kwa kuhofia kipigo na fedheha toka kwa wananchi.

Naam, kazi kubwa ilifanyika hadi kutafuta washauri nguli ambao walitushauri tukiwa majukwaani tujinadi kama chama cha Magufuli na sio CCM.

Kuna kila dalili mwaka 2025 na kuendelea ni dhahiri CCM itaenda kwenye uchaguzi dhidi ya wananchi na hapo siku zijazo itabidi kumtafuta Magufuli mwingine kunusuru chama.

Mitandaoni Magufuli ni Rais wa hovyo kuwahi kutokea nchi hii,Kitaani Magufuli ni shujaa watu wanampenda mpaka sifa nyingine wanamuongezea.

Ile surprise waliyoona watu wa mitandaoni wakati wa msiba wa Magufuli tuombe Mungu isije kujirudia kwenye chaguzi against yoyote anaesema tofauti juu ya Magufuli.

Inawezekana Hayati Magufuli aliletwa kuanzisha siasa mpya kwenye nchi. Tunayoyaona mtaani yanaeleza lugha fulani ambayo unaweza kuwa mkaidi kuikubali ila wakati siku zote ndio msema kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom