Maongezi ya kijana aliyeandika verse za BONGO FLAVOR necta form 4 mwaka jana...

Ni kweli kaka, lakini kama akili zake ziko timam na malezi yangekuwa sahihi asingeandika "mistari" kwenye mtihani, angeonesha juhudi yake ya kujaribu kujibu kwa usahihi kwa kadri anavyoweza!

Amesha jaribu mpaka kachoka, kuna kipindi kinafika unasema mimi hili suala basi tena ila unalazimishwa!! sasa unategemea hapo nini kitatokea??
 
Amesha jaribu mpaka kachoka, kuna kipindi kinafika unasema mimi hili suala basi tena ila unalazimishwa!! sasa unategemea hapo nini kitatokea??

KITENDO CHA KUANDIKA "MISTARI" KWENYE MTIHANI NI UTOVU WA NIDHAMU. (NUKTA)
Kama yeye alijiona masomo anayosoma hayapandi kwa nini hakuongea na wazazi/walezi wake wakampeleka VETA?...au anataka kutudanganya kuwa yeye hawezi kuwa na kipaji chochote tofauti na "bongofleva"? Anatakiwa ajitambue, hiyo sanaa ni kweli ana kipaji nayo? alishawahi kujiskia hata kuimba kwaya darasani?...zaidi itakuwa tamaa na maigizo ya kuiga! Hashangai kuona wasanii wote waliotulia hata Tanzania hii wamepitapita Madarasani, japo hata kidato cha sita; hata hao wavuta bhangi na wahuni wanaoimba huko mitaaani hawakuwahi kuandika "mistari" kwenye mitihani.
 
kwaupande wangu ninakubaliana nae asilimia mia maana kiukweli upande wa pili wa watu wenye vipaji vya pekee wanapata shida sana hapa tanzania maana lazma asome vipaji vya watu kwa lugha ya kigeni wanasema anakuwa force kufuata kile asichokipenda na hivyo ndipo unaweza kuja kuona muigizaji anaaza kuwa mwanasiasa au muimbaji anaanza kuwa mwanasiasa. mfano capten komba lakin ikianzia chini angekuwa mbali na angefanya vizur kiasi kwamba tanzania tungekuwa na wasanii wakubwa kuliko tulio nao sasa hivi maana mskama wanapoteza pesa yao na muda wa watoto wao

ni kweli kwamba watu wametofautiana katka IQ,ila jamaa katuma ujumbe kwenye wrong number,kama anakipaji cha kuimba,angetunga wimbo ambao ungebeba ujumbe wake na sio kuandika kwenye karatasi za kujibia mtihani wa taifa. Julius alikuwa na kosa ila kwasababu amekiri,basi asamehewe.
 
KITENDO CHA KUANDIKA "MISTARI" KWENYE MTIHANI NI UTOVU WA NIDHAMU. Kama yeye alijiona masomo anayosoma hayapandi kwa nini hakuongea na wazazi/walezi wake wakampeleka VETA?...au anataka kutudanganya kuwa yeye hawezi kuwa na kipaji chochote tofauti na "bongofleva"? Anatakiwa ajitambue, hiyo sanaa ni kweli ana kipaji nayo? alishawahi kujiskia hata kuimba kwaya darasani?...zaidi itakuwa tamaa na maigizo ya kuiga! Hashangai kuona wasanii wote waliotulia hata Tanzania hii wamepitapita Madarasani, japo hata kidato cha sita; hata hao wavuta bhangi na wahuni wanaoimba huko mitaaani hawakuwahi kuandika "mistari" kwenye mitihani.

Hapo kweli kabisa mkuu!! suala la kuandika mistari halikua suluhisho la matatizo yake, ada walizo lipa wazazi wake bora ange washauri wa mpele pale bagamoyo au hata VETA kuliko kuandika mashairi!!
 
Big up sana kwa huyu jamaa coz bila hivo asingetoka asa hv ni bonge la star kila m2 anatamani kumjua na kusikiliza nyimbo yake ndo kashatoka mwenzune
 
Namuunga mkono, japo watu wanaweza wasinielewe. Mfumo huu wa elimu tilionao ndio unaoandaa watu wasio na ajira, ambao huichukia serikali yao, kwa lunga nyingine 'government create seeds of its own destruction'. Ili kupunguza ukosefu wa ajira, mfumo wa elimu unahitaji mabadiliko, lakini wengi hawalijui hili.
Uchumi wa sasa kautegemei viwanda tu, bali hata huduma, huduma hizo ni kama muziki, tamthilia n.k. Ili kukuza huduma na hatimaye uchumi, wanafunzi wanapaswa kuandaliwa ili kuweza kwenda sambamba na mfumo wa dunia.
Wamafunzi wanapaswa kupelekwa shule kadiri ya uwezo na vipaji vyao. Kunapaswa kuwa na shule za sanaa, kilimo, n.k angalau chache kwa ajili ya kuwaendeleza wanafunzi. Mimi nimewahi kuwa Makongo High School, pale Makongo kuna wanafunzi wenye uwezo mdogo sana darasani (kama Dogo Janja n.k) lakini mfumo unawakuza. SULUHU YA UKOSEFU WA AJIRA HAITOKWISHA IKIWA WANAFUNZI WATALAZIMISHWA NA MFUMO KUSOMA KUFANYA KAZI VIWANDANI, ILI HALI UCHUMI WETU HAUNA VIWANDA
 
Yafuatayo ni maongezi ya kijana Julius na mtangazaji wa PB, Gerald Hando wa Clouds FM. Julius afunguka na kueleza jamii sababu iliyomfanya afanye kitendo hicho.


Historia fupi...
Jina langu naitwa Julius na nina umri wa miaka 23.
Nimechelewa kumaliza shule kwa kuwa nilikua narudia sana shule.
Kwa sasa naishi Tabata Segerea, kiasili mimi ni Mchaga wa Marangu.
Mwanzoni nilkua naishi na mama mdogo, lakini sasa nakaa peke yangu, mama yangu anaishi Kisarawe, na huko ndipo nilianza shule. Nilianza elimu ya msingi Umoja mwaka 1996, baadaye mwaka1999 nikahamia kijiji cha Gwata Kisarawe na huko nilimaliza elimu ya msingi na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Maneromango.

Upande wangu kielimu ulikua ngumu sana, hii ni kutokana na uwezo mdogo wa kuelewa masomo. Kidato cha pili nilirudia mara mbili, baada ya hapo nikarudi nyumbani na kukaa nyumbani mwaka mzima. Baadae mama mdogo akanichukua na kunileta Dar, na kuanza tena kidato cha kwanza.
Nilikua naipenda sana shule, ila inabidi ijulikane kwamba utofauti wa upeo wa kuelewa vitu unatofautiana baina ya mtu na mtu.
Mara nyingi nilikua nasukumwa kusoma sana na Mama mdogo. Mara nyingi darasani nilikua na matokeo mabaya sana (hapa anaongea kwa sauti ya chini)

Sababu ya kuandika bongo flavor...
Jinsi ninavyoishi najiuliza vitu vingi sana. Katika nchi yetu kuna hii "system" kuwa, kama unataka kuwa na maisha mazuri kuna "system" ambayo unaenda nayo mwanzo mwisho, vivyo hivyo kwa watu wenye maisha magumu.
Nilikua najaribu kutuma mesage kwa watu wanaosimamia elimu ya Tanzania kuwa vipaji vinatofautiana baina ya watu, ila watu walichukulia suala langu upande mmoja tu wakidhani labda huyu mtu hapendi shule au ni muhuni.
Wakati wa kuandika ile mistari ya Bongo flavor nilikua nikiamini baraza la mitihani na kada mbalimbali za serikali zitalipokea tukio hilo kwa upande chanya.

Wito...
Mimi napenda sana sanaa kwa ujumla na ninaamini nipo vizuri sana upande huu, sasa kama kungekua na utaratibu wa kukuza vipaji sambamba na elimu ya darasani naamini ingekua inasaidia watu kama mimi.

Alijisikiaje baada ya kutangazwa na Ndalichako...
Baada ya kufanya tukio lile na kuona reaction ya jamii, nilikua najisikia vibaya sana, na wakati mwingine hatawaandishi walikua wakinikebehi.
Lakini baada ya kuja hapa studio leo najisikia vizuri sana na nahisi kama nimetua mzigo mkubwa sana. Hii imekua fursa pekee kwa jamii ya Watanzania pengine kunielewa.

Mwisho...
Kama kuna mzazi au mtu yoyote ambaye nimemkwaza au nimemkatisha tamaa kwa jinsi yoyote ile naomba anisamehe, nia yangu ilikua ni kufikisha ujumbe na kilio cha watu wenye uwezo mdogo kieleimu lakini upande wa pili tuna vipaji vya sanaa.

Julius kwa sasa anafanya sanaa ya kuandika na kuimba muziki. Kwa sasa amarekodi wimbo mmoja unaoitwa "Mr President".

Umeshapoteza Muelekeo wewe. Ungendika Ushairi wenye kujenga ungeeleweka. Mbona uliandika ushairi wa Mapenzi na vina havipandi?
Utafikia lengo kweli kwa style hii.
Ushauri- Nenda kaole chuoni utapa pa kuanzia.
 
inauma sana palf vjana wanapoandika vtu ambavyo havifai kabsa kwenye mitihan.n ktu ambacho kwa kweli knakatisha tamaa wale ambao nao wanategemea kufanya mtihan baadae.
 
halafu kuna makima Kama akina Nicholas wanajisifia. eti wachaga wana akili..

pathetic fool
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom