Maongezi ya kijana aliyeandika verse za BONGO FLAVOR necta form 4 mwaka jana...

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
70,823
93,519
Yafuatayo ni maongezi ya kijana Julius na mtangazaji wa PB, Gerald Hando wa Clouds FM. Julius afunguka na kueleza jamii sababu iliyomfanya afanye kitendo hicho.


Historia fupi...
Jina langu naitwa Julius na nina umri wa miaka 23.
Nimechelewa kumaliza shule kwa kuwa nilikua narudia sana shule.
Kwa sasa naishi Tabata Segerea, kiasili mimi ni Mchaga wa Marangu.
Mwanzoni nilkua naishi na mama mdogo, lakini sasa nakaa peke yangu, mama yangu anaishi Kisarawe, na huko ndipo nilianza shule. Nilianza elimu ya msingi Umoja mwaka 1996, baadaye mwaka1999 nikahamia kijiji cha Gwata Kisarawe na huko nilimaliza elimu ya msingi na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya sekondari Maneromango.

Upande wangu kielimu ulikua ngumu sana, hii ni kutokana na uwezo mdogo wa kuelewa masomo. Kidato cha pili nilirudia mara mbili, baada ya hapo nikarudi nyumbani na kukaa nyumbani mwaka mzima. Baadae mama mdogo akanichukua na kunileta Dar, na kuanza tena kidato cha kwanza.
Nilikua naipenda sana shule, ila inabidi ijulikane kwamba utofauti wa upeo wa kuelewa vitu unatofautiana baina ya mtu na mtu.
Mara nyingi nilikua nasukumwa kusoma sana na Mama mdogo. Mara nyingi darasani nilikua na matokeo mabaya sana (hapa anaongea kwa sauti ya chini)

Sababu ya kuandika bongo flavor...
Jinsi ninavyoishi najiuliza vitu vingi sana. Katika nchi yetu kuna hii "system" kuwa, kama unataka kuwa na maisha mazuri kuna "system" ambayo unaenda nayo mwanzo mwisho, vivyo hivyo kwa watu wenye maisha magumu.
Nilikua najaribu kutuma mesage kwa watu wanaosimamia elimu ya Tanzania kuwa vipaji vinatofautiana baina ya watu, ila watu walichukulia suala langu upande mmoja tu wakidhani labda huyu mtu hapendi shule au ni muhuni.
Wakati wa kuandika ile mistari ya Bongo flavor nilikua nikiamini baraza la mitihani na kada mbalimbali za serikali zitalipokea tukio hilo kwa upande chanya.

Wito...
Mimi napenda sana sanaa kwa ujumla na ninaamini nipo vizuri sana upande huu, sasa kama kungekua na utaratibu wa kukuza vipaji sambamba na elimu ya darasani naamini ingekua inasaidia watu kama mimi.

Alijisikiaje baada ya kutangazwa na Ndalichako...
Baada ya kufanya tukio lile na kuona reaction ya jamii, nilikua najisikia vibaya sana, na wakati mwingine hatawaandishi walikua wakinikebehi.
Lakini baada ya kuja hapa studio leo najisikia vizuri sana na nahisi kama nimetua mzigo mkubwa sana. Hii imekua fursa pekee kwa jamii ya Watanzania pengine kunielewa.

Mwisho...
Kama kuna mzazi au mtu yoyote ambaye nimemkwaza au nimemkatisha tamaa kwa jinsi yoyote ile naomba anisamehe, nia yangu ilikua ni kufikisha ujumbe na kilio cha watu wenye uwezo mdogo kieleimu lakini upande wa pili tuna vipaji vya sanaa.

Julius kwa sasa anafanya sanaa ya kuandika na kuimba muziki. Kwa sasa amarekodi wimbo mmoja unaoitwa "Mr President".
 
Si angemwandikia waziri wa elimu barua akamueleza mtazamo wake badala ya kuandika wimbo wakati anatakiwa kufanya hesabu?
 
Sanaa gani zinafanywa bila kusoma na kuwa na nidhamu?

ukweli ni kwamba elimu ni ufungua wa maisha, lakini neno ELIMU ni pana si lazima iwe ya darasani ile ya Bunsen burner, Archmerdes principle au sijui Chimulenga war n.k. Jamaa anasisitiza kungekua na msisitizo wa elimu maalumu za sanaa kwa watu kama yeye.
 
Si angemwandikia waziri wa elimu barua akamueleza mtazamo wake badala ya kuandika wimbo wakati anatakiwa kufanya hesabu?

nadhani wazo hilo hakuwa nalo, anyway ila imemfanya kawa celebrity in his world
 
Mim nimemsifu,amefanikiwa kuufikisha uumbe kwa wahusika nina imani wote walilijua hilo,na hii ndio maana watu hupindua hata nchi,;vikitumwa vilio havifiki au havisikilizw lakini ukipindua nchi tu, unajulikana na kusikilizwa ulitaka nini hata kama hutafanikiwa kuupata huo ukuuu.
 
Back
Top Bottom