Maombi yenu tafadhali

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,801
20,759
Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF,

Leo asubuhi tarehe 29/03 ni siku ya furaha kwangu kwa sababu kuu mbili. Kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa mke wangu mpendwa, ametimiza miaka 29🙂. Namtakia kheri ya kuzaliwa na ningependa kusheherekea nanyi ndugu zangu.

Pili, Leo hii tuko hospital magomeni hapa. Mda huu amepangiwa c section (kujifungua kwa operation). Huyu akiwa mtoto wetu wa pili. Hivi navyoandika hapa yuko chumba cha upasuaji (Theatre) na mimi niko nje nasubiri.

Ndugu zangu huu ni mwezi wa Kwaresma na pia ni mwezi wa Ramadhani. Tuwe pamoja na kheri njema ya maombi yenu.

Ndugu yenu Gily . .

Updates:
07:41 Nimefurahi sana ndugu zangu nimepata mtoto wa kiume. Niko nae hapa analia kinyama mpaka natamani nilie. Mungu kanipa hitaji la moyo wangu, nilikuwa natamanj sana kuwa na mtoto wa kiume. .

Mke wangu bado yuko chumba cha upasuaji. Nimepewa taarifa she is doing fine ila bado wanamshona na kumsafisha. I can't wait to see her.

Updates:
08:00 mke wangu katoka chumba cha upasuaji. Tuko chumba cha wodi private. Anaendelea vizuri madaktari wanampima pressure iko vizuri kabisa. .
 
20230329_054959.jpg
20230329_054955.jpg
 
Mama na mtoto watakuwa wanakula birthday pamoja, safi sana.

Neema ya yake ikawe juu yenu!.
Alitaka iwe hivyo kwa sababu ilikuwa planned c on 25th March, akaomba iwe on 29th March wawe na birthday moja. .

Ila hata mwanangu wa kwanza wa kike alizaliw 29th September. Haha birthday zao wote mke wangu na wanae ni tarehe 29. .

Amina. .
 
Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF

Leo asubuhi tarehe 29/03 ni siku ya furaha kwangu kwa sababu kuu mbili. Kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa mke wangu mpendwa, ametimiza miaka 29🙂. Namtakia kheri ya kuzaliwa na ningependa kusheherekea nanyi ndugu zangu. .

Pili, Leo hii tuko hospital magomeni hapa. Mda huu amepangiwa c section (kujifungua kwa operation). Huyu akiwa mtoto wetu wa pili. Hivi navyoandika hapa yuko chumba cha upasuaji (Theatre) na mimi niko nje nasubiri.

Ndugu zangu huu ni mwezi wa Kwaresma na pia ni mwezi wa Ramadhani. Tuwe pamoja na kheri njema ya maombi yenu. .

Ndugu yenu Gily . .
Mbona wakati wakutiana mimba hukutaka maombi yetu
 
Back
Top Bottom