Maofisini kuna mambo

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,435
Reaction score
166,886
Hapa ofisini kwetu kuna kaka mmoja mwanasheria. Anaheshimika na watu wote kutokana na tabia yake ya kuwahi sana ofisini, unadhafu na ukimya wake.
Leo nimewahi sana kufika ofisini kwa kuwa nilikuwa nimetokea muhimbili kumuona mgonjwa.
Nilichokishuhudia, mheshimiwa huyu nimemkuta ****** akichota mikojo yake na kunawa usoni. Aliponiona alishtuka sana, akaniambia ana safisha nyota na kujikinga na uchawi ambao wabaya wake wamekuwa wakimtupia.
Jamani, kumbe vyeti sio ufahamu.
Nimecheka sana leo.
 
du, eee bwana eee. Kumbe sheikh Yahaya bado anawateja??? Aibuuuuuuuu itokanayo na kudanganyika.
 
Isishangae sana baadhi ya wasomi tz,wanaamii na kutenda mambo ya kishirikina.. You just keep calm atakuogopa milele,tena angekuwa bosi ingekuwa fresh sana.more marupurupu.ofisini kwetu kuna jamaa anashindwa kutembea vizuri,amelazwa hospitali anhisi tumbo lina pini,au misumarina na inatoa sauti akiruka.shit happens.
 
Vyeti?? mbele ya waganga wa kienyeji? Mbele ya waganga wa kienyeji hakuna cha usomi wala nini kwa walio wengi. Wanawatii na kuwaabudu kama miungu. Fikiria mtu kunawa mikojo yake! Kaambiwa afanye hivo na mganga wake bila shaka. Haingii akilini. Lakini ndo hali halisi.
 
duh kazi kweli kweli.....watu kama hao wasiomtegemea MUNGU maishani mwao,adhabu kama hizo huandamana nao...ama kweli shetani hawezi kukupa kitu cha bure....lazima akuaibishe...aibu gani hiyo sasa na uchafu juu
 
Msishangae.
Nakumbuka miaka ya 80, nikiwa field wizara fulani, kuna katibu wa wizara alikuwa anakuja na kuku mweupe kila siku ofisini, akisema kuwa huyo kuku ni mzimu wa babu yake na unamlinda.
Ofisini mwake alikuwa akiwasha ubani 24 hrs, ukiingia huwezi kukaa zaidi ya dakika 5. Mlangoni alibandika karatasi fulani lina maneno ya kiarabu yenye rangi nyekundu.
 
Waka waka ehee waka waka ehe this is africa!!!!
 
Ukienda; Bagamoyo,Handeni, na kwingineko, Nyakati kama hizi huwa kuna misururu ya ma rand cruiser ya waheshimiwa wetu, some of them are distinguished professors, wakifika huko mtu anafanya lolote ambalo mganga huyo(hata darasa la saba hakufika) anamuelekeza ili eti ashinde tena kwenye kinyang'anyiro!!!
Professor analishwa matakataka bila kuhoji hata kidogo!!! Asikuambie mtu!! People are captives
 
Aiseee mambo ya aibu kwa kweli!
 

hata humu JF wamo!!!
 

hi itakuwa ni brand mpya eeh!!...
 

inawezekana hao ndio wanasababisha hata mauaji ya albinos!! inasikitisha sana
 
Washirikina wote na waaminio uchawi akili zao zimo humu ndani ya hii kaptura.
 
hahahahaha hehehehe bwahahaha
alikuwa Nyani Ngabu nini?
 

Mkuu hapo kwenye red nimecheka kumbe ukitaka watu wasijae ofisini kwako choma ubani tu!
 
Hewa ya oxigen ilikuwa ikimalizwa na harufu ya huo ubani aliokuwa ukichoma. Mwenye matatizo katika mfumo wake wa upumuaji lazima achungulie kaburi, kutokana na hewa mbaya ya kile chumba.
Mkuu hapo kwenye red nimecheka kumbe ukitaka watu wasijae ofisini kwako choma ubani tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…