Manyara: Waziri mkuu Azindua kituo cha Tanzanite Magufuli. Astaajabishwa na Kazi kubwa iliyofanyika Ukuta wa Mirerani

Leo waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anazindua kituo cha Tanzanite Mirerani mkoa wa Manyara, kuwa nami...

=======

Waziri Mkuu: Nimekuja na salam zenu kutoka kwa mheshimiwa Rais, mama Samia Suluhu anawasalimia sana wana Mererani, pia makamu wa Rais. Viongozi wetu wanawatakia mafanikio makubwa kwenye kazi zenu, wale ambao mnafanya kazi za madini mpate mafanikio makubwa, mnaofanya kazi za kilimo, mlime mpate mafanikio makubwa. Mheshimiwa Rais ameniambia niwaambia nitakuja kuwatembelea.

Ndugu wanamirerani, ziara hii pamoja na kuja kuzindua, leo nimepata fursa ya kupita pembeni mwa mgodi wetu mkubwa, nilikuwa sijawahi kupita kuona hali hiyo.

Kwa kweli Kazi kubwa serikali imefanya, kujenga ukuta eneo hili lote na miundombinu yote tunayoiona hapa sio jambo la mzaha na wala msilione kama ni jambo tu la kawaida, limetibitishwa na idadi ya watu niliowakuta hapa, hapa panashika uhai wa watu.. Maisha ya watu yako hapa.


Lazima serikali tuweke utaratibu mzuri tuendelee kuona malengo yenu yanafikiwa. Ujenzi wa ukuta huu ni nia njema ya kuwafikisha huko mnakotarajia.

Tanzanite hii ndio inatusaidia kupata fedha za maeneo mengine.
Serikali hii inazidi kutia nuksi kwenye miradi kwa kuendelea kumtumia mwendazake kama daraja
 
Hakuna majina ya wenyeji?
Yule mzee aliyegundua aina ya hayo madini angepewa hilo jina.

Hata MATONYA ingekuwa good
Duu, nina mashaka na maisha yako, ukisikia pahala pengine pameandikwa jina la huyu mwamba nahisi utajinyonga!😛
 
Sawa kabisa ni wakati sasa mbuga ya Burigi nayo ipewe jina la magufuli kama itapendeza na shule zote ziitwe magufuli
Acha dhihaka kiongozi, kama umpendi wewe sio wote walikuwa wanamchukia kuna mabaya alifanya lakini kuna mazuri mengi sana aliyotufanyia ata wewe huna ukamilifu.
 
Marehemu aliua uchumi na kujitengenezea maadui wengi.

Awamu ya 6, kujishikamanisha sana na Serikali ya awamu ya 5, ni kufanya kosa kubwa la kiufundi na kujiwekea ugumu kuyafikia malengo yake kwa haraka.

Walioondoa vitega uchumi vyao Tanzania, kama wataona mwelekeo unakaribiana sana na ule wa awamu ya 6, hawatavirudisha vitega uchumi vyao, na vipya havitakuja, wala hata hawa wawekezaji wa humu ndani hawatashawishika kujenga kwa haraka.

Mwekezaji anahitaji sana uhakika wa mazingira anayowekeza. Awamu ya 5 ilikuwa hostile kwa investors na business community. Je, awamu ya 6 inafanya nini cha pekee kuonesha ina tofauti kubwa na awamu ya 5?
 
Nawakumbusha tu mpaka sasa Rais Samia hajajipa jina hata mradi mmoja
 
Back
Top Bottom