Manyara: Waziri mkuu Azindua kituo cha Tanzanite Magufuli. Astaajabishwa na Kazi kubwa iliyofanyika Ukuta wa Mirerani

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Leo waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa anazindua kituo cha Tanzanite Mirerani mkoa wa Manyara, kuwa nami...

=======

Waziri Mkuu: Nimekuja na salam zenu kutoka kwa mheshimiwa Rais, mama Samia Suluhu anawasalimia sana wana Mererani, pia makamu wa Rais. Viongozi wetu wanawatakia mafanikio makubwa kwenye kazi zenu, wale ambao mnafanya kazi za madini mpate mafanikio makubwa, mnaofanya kazi za kilimo, mlime mpate mafanikio makubwa. Mheshimiwa Rais ameniambia niwaambia nitakuja kuwatembelea.

Ndugu wanamirerani, ziara hii pamoja na kuja kuzindua, leo nimepata fursa ya kupita pembeni mwa mgodi wetu mkubwa, nilikuwa sijawahi kupita kuona hali hiyo.

Kwa kweli Kazi kubwa serikali imefanya, kujenga ukuta eneo hili lote na miundombinu yote tunayoiona hapa sio jambo la mzaha na wala msilione kama ni jambo tu la kawaida, limetibitishwa na idadi ya watu niliowakuta hapa, hapa panashika uhai wa watu.. Maisha ya watu yako hapa.


Lazima serikali tuweke utaratibu mzuri tuendelee kuona malengo yenu yanafikiwa. Ujenzi wa ukuta huu ni nia njema ya kuwafikisha huko mnakotarajia.

Tanzanite hii ndio inatusaidia kupata fedha za maeneo mengine.
 
Magufuli ameifanyia mambo mema na makubwa sana nchi hii. Alikuwa Rais bora kabisa wa nchi yetu. Shujaa wa Afrika na kiboko cha mabeberu, Rais Magufuli, apumzike kwa amani mbinguni.
Kumbuka na maraisi wa nyuma yake nao pia walifanya makubwa katika nchi hii
 
Sawa kabisa ni wakati sasa mbuga ya Burigi nayo ipewe jina la magufuli kama itapendeza na shule zote ziitwe magufuli
 
Back
Top Bottom