Manumba, Tunataka Taarifa ya Mtoto wa Mengi/Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manumba, Tunataka Taarifa ya Mtoto wa Mengi/Mengi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Feb 20, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sifa moja ya Watanzania ni kufanya mambo kisanii/kishkaji. Bw Reginald mengi alilalamikia kitendo cha polisi kumbambikizia mwanae madawa. Hadi leo hatuambiwi nini kinaendelea. Dr Mwakyembe ameitaja kwenye taarifa yake.

  Imefika mahali kama nchi tuache usanii. Hizo ni tuhuma nzito na kama nchi tuna haki ya kujua nini kilijiri. Kama ni tuhuma za uongo au ukweli hatua zichukuliwe. Hata swala la Dowans limeisha kimya kimya, nini kinaendelea, mbona tunafichwa?

  Siridhiki na nchi inavyoendeshwa
   
 2. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na yule jamaa wa Kitengo cha Madawa ya kulevya cha JNIA, pamoja na kuhusika kwake vile katika kufanikisha uharamia ule, bado yuko kazini anadunda tu!...huh!
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Join Date : 16th February 2012
  Posts : 1
  Rep Power : 0


  Welcome...nadhani tume ikiundwa itakuja na jibu muafaka...nchi ya tume hii kijana!!
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mai siunajua mpaka tukumbushane ukisahau wanakupotezea ukikumbusha wanaludi kujitetea ukikazania kiweleweke kama madaktari ndio unapata majibu ya tatizo lako kwa kuwa viongozi wetu walio wengi wanaamini kiongozi ni kusublia jambo litokee na si kuanzisha ama kusimamia jambo kidedea mpaka litokee.
   
 5. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama Kikwete mwenyewe ni msanii unategemea Vibaraka vyake watakuaje.
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nchi hii tunaishi kijanja kijanja
  Rais Mjanja mjanja bullshit hatuna Rais
   
 7. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 641
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  • Haki ya kujua (the right to be informed) ni ya kikatiba. Lakini haina nguvu ya kisheria kwa Tanzania.So, ni kutulia tusubiri neema za Mungu kwenye hilo. Kwa nchi zingine za Ulaya unaweza kuomba taarifa kutoka kwenye taasisi za kiserikali.
  • Swala la Dowans kulipwa hilo liko wazi. Kisheria, baada ya kusajili kesi iliyotolewa maamuzi nje ya nchi, maamuzi hayo yanakuwa sawa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama za ndani. Swali ni je, kuna mtu au taasisi inayoweza kupinga maamuzi ya mahakama? Malipo ni shughuli za kiofisi sio lazima yatangazwe na magazeti. Tafakari, akili kichwani!
   
 8. n

  nicksemu Senior Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  They can take everything away from us except memories. Siku yao inakuja 2015
   
 9. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mengi aliwatuhumu publicly na kuwataka Watubu, Wajiuzuru na kuwaambia kama wanaona amelizalilisha Jeshi la polisi kwa kulizushia Uongo, basi Wamshitaki na kwamba yeye amejiandaa na Ushahidi wote. Wako kimya mpaka leo!

  Kama Mengi kasema uongo, mbona hawataki kujiosha mbele yetu kwa kumshitaki ili tujue kwamba kweli amelichafua Jeshi la Polisi? Wanaogopa nini!

   
 10. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Wamepigwa chini footmen, lol!!
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hivi na yule askari wa kike (Suzan nadhani)aliyeuawa kwa kupoteza msafara wa KIKWETE....iliishia wapi ile?
  Nchi hii!
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hii nchi ilishauzwa siku nyingi, sasa huridhiki nini unataka chenji?
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nadhani hawa wanaojitia kimbelembele kujibu kwa hili la Mengi wamegwaya. Wasanii siku zote ndivyo walivyo. Polisi wachache wamesababisha tulichukie jeshi zima na migwanda yao.
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Polisi na TISS haya ni magenge ya kihalifu ,wana mkono kwenye mauaji ya wananchi wengi wasio na hatia kwa faida ya watawala(CCM).
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Wajameni ACHENI NISEME HATA MKINICHUKIA ACHENI NISEME, HATA MKINI..................... ACHENI NISEME......
  "JAKAYA KIKWETE NA BARAZA ZIMA LA MAWAZIRI HAWAFAI HATA KUONGOZA KUWA WAJUMBE WA NYUMBA 10; WOTE WAJIUZULU"


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mkuu nchi inaendeshwa kishkaji shkaji unategemea kuna uwajibikaji hapo thubutu
   
 17. m

  mpiganaji86 Senior Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunataka na taarifa ya tapeli maarufu mjini' papaa musofe ,tuambiwe baada ya kurudisha kiwanja alichovamia cha edwin mlay wa mbezi amechukuliwa hatua gani ?
   
 18. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  tanzania na watu wake ni zaidi uijuavyo Manumba + Mwema = Kifo Kinyama
   
 19. m

  mchambakwao Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe aliuwawa,maskini.Si walitangaza kuwa alijiua au? lakini kitaa walikuwa wakisema kiongozi wake ndiye aliyepotosha msafara
   
 20. l

  luhwege Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Si hayo tu jamani ni mengi na meno ya tembo kule zanzibar yaliyokamatwa kwenye meli yakisafirishwa yamefikia wapi mbona kimya jamani nchi hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
   
Loading...