Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,021
- 9,177
Manumba alazwa ICU Aga Khan
HALI ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwenye wodi ya wgonjwa Mahututi (ICU) jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com hivi punde ni kwamba Manumba amelazwa katika Hospitali hiyo tangu juzi.
Hata hivyo vyanzo vya kuaminika ndani ya Jeshi la Polisi nchini zinadai kwamba hali ya Mkurugenzi huyo wa makosa ya jinai nchini ni mbaya.......
MY TAKE:
Eah Mwenyezi Mungu Msaidie Kiumbe wako huyu apone haraka aje atutumikie Watanzania kama alivyotutumikia Jana na juzi na kesho afanye hivyo,
Umzidishie maisha marefu aishi ili aine kesho na kesho kutwa.
Amin!

Manumba mahututi, alazwa Aga KhanHALI ya Mkurugenzi wa Upeleleziwa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbayana amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan,Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapobaada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumbaalikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha piafigo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
"Alitakiwa kupelekwa nje ya nchikwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua,ikashindikana," kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alithibitisha kamishna huyo kulazwaICU Aga Khan lakini akasema kuwa hadi jana jioni, hali yake ilikuwa ikiendeleavizuri.
"Ni kweli amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendeleavizuri," alisema Senso.
Mtu wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vyamalaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figokushindwa kufanya kazi.
"Kutokana na hali aliyonayo tumeshindwa kumsafirisha kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu zaidi kwa sababu baadhi ya viungo havifanyi kazi," alisemamtu huyo.
Hata hivyo, alisema hali ya Manumba inaendelea vyema baada ya kuanza kupatamatibabu.
JK amjulia haliViongozi mbalimbali wa Serikali,akiwamo Rais Jakaya Kikwete jana walifika hospitalini hapo kumjulia halikamishna huyo wa polisi.
Habari zilizopatikana zilieleza kuwa Rais Kikwete alifika hospitalini hapo janamchana baada ya kumsindikiza mgeni wake, Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekitiwa Umoja wa Afrika (AU), Boni Yayi.Daktari
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema jana kwambaManumba alifikishwa katika hospitali hiyo tangu juzi akisumbuliwa na malaria naalikuwa hajitambui.
Dk Dharsee alisema kuwa uchunguzi wa awali ulionyesha kwamba alikuwa na malariakali iliyosababisha alazwe ICU. Hata hivyo, alisema baada ya matibabu, haliyake ilianza kubadilika na kuleta matumaini.
"Nimepigiwa simu nyingi leo (jana), nikiulizwa na watu mbalimbali wakitakakufahamu kama Manumba amefariki dunia, ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzimalakini yuko ICU," alisema.
Hata malaria mtu inabidi aende kutibiwa nje ya nchi kweli??