Majimbo ya uchaguzi yaongezwe kwa fidia ya viti maalumu

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,497
46,023
Kama kuna haja ya kuongeza majimbo ya uchaguzi basi ondoeni ubunge wa viti maalumu. Majimbo mapya ya uchaguzi yaongezwe kwa kupunguza idadi ya viti maalum. Ingependeza kwa kila jimbo 1 la uchaguzi linaloongezwa vipinguzwe viti 3 vya ubunge wa viti maalumu.

Mantiki ya ubunge katika nchi za demokrasia halisi ni mtu achaguliwe na wananchi katik jimbo la uchaguzi sio kuteuliwa kama ilivyo katika mhimili wa serikali au mahakama.
 
Mnataka kuchezea kodi zetu tu hakuna lolote la maana hata mkiamua madiwani wote waende bungeni

USSR
 
Katika vitu ambavyo naona ni matumizi mabaya ya raslimali fedha ni hao waitwao wabunge wa viti maalumu.Kuna wengine anaweza akamaliza miaka mitano ya bunge hajawahi hata kuchangia hoja bungeni.Hata kama ni programu ya kuwa empower wanawake uandaliwe utaratibu wa kuhakikisha namna gani wanashinda mfano kutenga baadhi ya majimbo ambapo wagombea wawe wanawake tu kwa kipindi fulani .Lazima tuachane na ubunge huu wa kupewa hata watu ambao wanauza sura bungeni kwa kupaka make up tu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Sahihi
 
Serikali huwa inatumia zaidi ya 200b,kuwalipa Wabunge wa viti maalumu.Haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipa Kodi.
 
Back
Top Bottom