Manispaa ya tabora idara ya sekondari kuna nini?

lutelemba

Member
May 25, 2011
26
1
Mimi nashangazwa na Manispaa ya Tabora Kupitia kwa Mkurugenzi na Afisa elimu idara ya sekondari, kwa kuamua kwa makusudi kabisa kutotenga fungu la kusomesha walimu kwenye budget, eti kwamba manispaa ya Tabora haina mpango huo. Cha kushangaza manispaa ya Tabora hata walimu walioko masomoni hawasaidiwi chochote, iwe nauli, ghalama za masomo na vingine, hata mbunge wetu kalinyamazia tu hilo halioni, AFisa elimu sekondari hana msaada kabisa kwa walimu, kila siku kugombana na walimu, Mkurugenzi kashindwa lao moja na afisa elimu sekondari. Wanajamii tusaidieni walimu Manispaa ya Tabora idara ya secondari kuna mdudu atatumaliza au wote tunaweza kukimbia kabisa. Tunahitaji michango yenu ya mawazo angalau Mbunge hatusaidii amekalia simba tu, Mkurugenzi hamna kitu, karibuni kwa mawazo.:tonguez:
 
pole, je huyu mbunge mmesha mfikishia malalamiko yenu kiofisi na je mnaifahamu kwa uzuri budget ya halmashauri yenu na je mna sabau zilizofanya kutoiweka sasa baada ya hapo tutaanza kuangalia kwa undani ili tujue wapi na nini tufanye,
 
Acha ya Tabora, sisi wa Shinyanga manispaa hilo la kutolipwa nauli, au hata pesa ya kununulia daftari la sh3000. Hakuna. Sambamba na hivo
1. Madaraja upandishwaji si kwa wakati.
2. Bado wanalazimisha watu warudi vituoni kufanya TP.
3. Tunatozwa 1500TSH ya Kitambulisho.
SOLUTIO.
1. Tujitoe ktk CWT sbb hizi ndio kazi zake ila ipo kwa maslahi ya wachache na kushirikiana na waajiri wetu kutukandamiza.
2. TUANZISHE VIKAO VYA UJIRANIMWEMA KISHULE KUJADILI matatizo na kwenda kuyadai sisi kama sisi na sio kumtegemea mtu.
3. Tunaweza tukiwa mmoja, wawili, na zaidi na hatusubiri kuwezeshwa.
4. Pamoja tuna weza.
 
Back
Top Bottom