mara kwa mara manispaa ya musoma imekuwa inachelewesha mishahara ya watumishi wake, tatizo liko wapi na ni kwanini hawa watumishi wanakuwa hawapewi sababu za kucheleweshwa kwa mishahara yao? mfano mpaka leo hii bado hawajatoa mishahara ile hali maeneo mengine yaliyo mengi wamehapokea mishahara, tatizo lliko wapi hapa Musoma? Mkurugenzi angetoa ufafanuzi kwa kuweka specific date ya kutoa mishahara ili kuleta amani kwa maisha ya Watumishi wake. Cha msingi ni kupeana taarifa na si kukaa kimya