Manispaa ya Arusha yatumia Milion 25mil kuwalipa Origino comedy ili kujaza watu mbele ya JK

diamond million10 ni nini anachoimba ambacho hatukijui.....alafu chakula cha mheshimiwa mil 20 au wameagiza mchele kutoka marekani nini? viongozi wa nchi hii wa ajabu sana wanatumia hela zote hizo wakati hilo jiji lina matatizo mengi tu ya kijamii sijawahi ona Rais anayependa kutumia hela za walipa kodi kwa manufaa yake mwenyewe badala ya manufaa ya wananchi..hatumtaki aje a town sijui nani kamualika kwanza
 
Mkuu ulianza vizuri.............ulikomalizia umemalizia na kinyesi mkuu wangu

Wala hajaanza vizuri mkuu huyu kichwa cha kuku, angalia vizuri hizo figure yeye anadai ze comedy wanalipwa 25 milioni kwa show wakati mleta hoja amesema ni 15 milioni.
 
Anaweza akajaza watu na wakaishia kumzomea , atakua amelipia hiyo 25 mill kuzomewa!
 
Kesho Arusha itazinduliwa rasmi na Rais wa JMT JK kuwa Jiji.Sherehe zitakazofanyika kwenye eneo la Mnara wa mwenge,na baadae Rais atazungumza na wananchi w Arusha kwenye uwanja wa mpira wa Sheih Amri Abeid.

Kutokana na hali ya kisiasa Arusha kuwa tata,Halimashauri imeidhinisha 15mil kwa ajili ya kundi la sanaa la Original comedy,na 10mil kwa ajili ya msanii Diamond,katika kikao cha madiwani jana kulikuwa na ubishi mkali,kati ya madiwani wa ccm na wale wa CHADEMA.

Mtoa habari wangu alisema kuwa CHADEMA wanapinga matumizi makubwa kwa jambo la muda mchache wakati kuna shule hazina vyoo,na huduma nyingine ni mbaya.Jumla ya gharama zote za kuzindua JIJI ni zaidi ya 120mil,ikiwa ni pamoja na chakula cha mchana kwa mh Rais na ujumbe wake,kinachotarijiwa kuwa 20mil.

Mmoja wa madiwani wa CHADEMA Nanyaro alitoka nje ya kikao kwa madai kuwa hawezi kuwa sehemu ya maamuzi ya kifisadi

Nitawashangaa watu wa Arusha kama mtaenda kwenye mkutano kwa sababu ya Diamond na Ze Comedy. Kama kweli mnachomsusia JK kina mantiki kwa maendeleo ya taifa, diamond na comedy ndo wataleta maendeleo? Hii inaonyesha kuwa ninyi si watu wa maendeleo bali na watu wa burudani. Kumbukeni hao kina Diamond na Ze comedy wanazidi kudhoofisha uchumi wenu kwa kulipwa mapesa mengi ambayo yangetumika kufanyia maendeleo ya mkoa wa Arusha. Mkienda kwa sababau ya hao jamaa mjue nayi si wazalendo.
 
Kweli lazi nchi ibaki tupu!
Huu ni uchizi kabisa!
Kutokana na hali ya kisiasa Arusha kuwa tata,Halimashauri imeidhinisha 15mil kwa ajili ya kundi la sanaa la Original comedy,na 10mil kwa ajili ya msanii Diamond,katika kikao cha madiwani jana kulikuwa na ubishi mkali,kati ya madiwani wa ccm na wale wa CHADEMA.
 
Jiji la Ars ni dogo kwa miundomsingi wangetumia hilo fungu kujenga barabara mbadala kutoka na kwenda Mji mdogo wa Njiro
 
Kwani uzinduzi wa jiji unahitaji shamrashamra na mbwembwe, huu ni ufisadi, hi yote ni kwasababu wabahofia watakosa watu uwanjani Arusha, na watu wa Arusha wanapenda hipop akina diamond siyo maarufu arusha! Wataendelea kudanganya umma mpaka lini sasa kuna uhusiano gani kuzindua jiji na burudani za muziki au vichekesho!
 
Msilalamke acha wafanye maamuzi ya hovyohovyo, Nyinyi wenyewe si ndio mmewapa tena viti 27 vya udiwani? Najisikia kumuwasha kibao mpigakura wa sisiemu akilalamikia haya matumizi
 
Mi-cdm uchwara kwa uwongo na porojo uchwara hamjambo. Nasikitika kwamba uwongo huo mtakuwa mkishindwa kila kona. Semeni angalau 1/8 ya ukweli mtafikiriwa. Huyo diwani wako mmoja katoka na kakwambia hivyo na kwanini hajakwambia kilichofanya cdm wenzie wabaki. Halafu unaleta uzi dhaifu hapa. Nyie vipi, mbona hamueleweki. Tukiaita vinyago vya mpapure mtakataa. PELEKENI porojo zenu hafifu Kinondoni huko wanazisubiri
 
ze original comedy,diamond wawepo wasiwepo uzinduzi utafanyika sioni haja ya kutengewa fungu kubwa huu ni ufujaji wa hela za walipa kodi ,kuna huduma za muhimu zinahitajika na za kimsingi hii ingetosha kuchimba visima hata nusu yake tu ,
 
Isingekuwa nchi ya wachuuzi hizo pesa wangepewa wakulima, potelea mbali hata isiponyesha mvua. Kunengua viuno kuna tija gani kwa taifa masikini kama TZ. Enzi za Mwalimu isingekubalika hata kidogo.

RIP Baba wa Taifa (Mwl. Julius Kambarage Nyerere)

Mkuu, nakubaliana nawe. Kwani uzinduzi ni kitu gani muhimu sana cha kutumia pesa yote hizo?
Hili jambo si lingeweza tu kutangazwa katika gazeti la serikali, kama ambavyo halimashauri, wilaya na mikoa mipya inavyofanywa.

Huko mbele ya safari mtashuhudia mkoa mpya ukitangazwa, kunafanyika sherehe ya uzinduzi na mgeni rasmi ni Rais mwenyewe aliyetoa na kusaini decree.

Mara nyingi masikini hupenda kuwa na matumizi makubwa kujilinganisha na tajiri!
 
Back
Top Bottom