Manispaa ya Arusha yatumia Milion 25mil kuwalipa Origino comedy ili kujaza watu mbele ya JK

Bila ze comedy na diamond Kikwete atakosa watu wa kuja kumsikiliza.
Na mkurugenzi naye na timu yake wanatafuta namna ya kuishi mjini kupitia ujio wa raisi hapo Arusha.
Shilingi 120 milioni zote kwa matumizi/kazi gani?
 
Isingekuwa nchi ya wachuuzi hizo pesa wangepewa wakulima, potelea mbali hata isiponyesha mvua. Kunengua viuno kuna tija gani kwa taifa masikini kama TZ. Enzi za Mwalimu isingekubalika hata kidogo.

RIP Baba wa Taifa (Mwl. Julius Kambarage Nyerere)

Baba Ritz kakosa mvuto Ngoja dyamond amfanyie fyucharing labda aibu itafichika
 
Nilisikia Diamond atakuwepo huyu kalipwa ngapi?
Kutokana na hali ya kisiasa Arusha kuwa tata,Halimashauri imeidhinisha 15mil kwa ajili ya kundi la sanaa la Original comedy,na 10mil kwa ajili ya msanii Diamond,katika kikao cha madiwani jana kulikuwa na ubishi mkali,kati ya madiwani wa ccm na wale wa CHADEMA.
 
Kwenye biblia hakuna dua mbaya dhidi ya mja wa mwenyezi mungu, lakini ingekuwa heri pale jk atakapofika eneo la mnara wa mwenge wa kumbukumbu ya azimio la arusha anguke na kuzimia kwa masaa kadhaa, labda itamzibua masikio kuwa wananchi tunalipenda na tunataka azimio la arusha litumike.
 
Mbona mkuu wa mkoa wa ARUSHA hajazuia hili kama yule wa KILIMANJARIO ALIYEZUIYA MADIWANI WASIENDE KIGALI KUJIFUNZA???????
 
Huyo baba mwanaasha anajua kua kuna mapacha watano kule geita wamefariki kwa kukosa kufaa cha kutunzia watoto njiti???ambulance imekosekana ya kuwapeleka kwenye hospitali yenye hiyo huduma,anajua hiloo???hii dhambi itawatafuna madiwani wote wanao tetea uoza unaoendelea wa kumkirimu huyo jakaya....acheni masihara jamani mbona kama ni starehe yupo kilasiku ulaya na markani.????cheni ubwege jamani dhambi hizo mnajipalilia badala ya kupalilia neeme.
 
Kesho Arusha itazinduliwa rasmi na Rais wa JMT JK kuwa Jiji.Sherehe zitakazofanyika kwenye eneo la Mnara wa mwenge,na baadae Rais atazungumza na wananchi w Arusha kwenye uwanja wa mpira wa Sheih Amri Abeid.

Kutokana na hali ya kisiasa Arusha kuwa tata,Halimashauri imeidhinisha 15mil kwa ajili ya kundi la sanaa la Original comedy,na 10mil kwa ajili ya msanii Diamond,katika kikao cha madiwani jana kulikuwa na ubishi mkali,kati ya madiwani wa ccm na wale wa CHADEMA.

Mtoa habari wangu alisema kuwa CHADEMA wanapinga matumizi makubwa kwa jambo la muda mchache wakati kuna shule hazina vyoo,na huduma nyingine ni mbaya.Jumla ya gharama zote za kuzindua JIJI ni zaidi ya 120mil,ikiwa ni pamoja na chakula cha mchana kwa mh Rais na ujumbe wake,kinachotarijiwa kuwa 20mil.

Mmoja wa madiwani wa CHADEMA Nanyaro alitoka nje ya kikao kwa madai kuwa hawezi kuwa sehemu ya maamuzi ya kifisadi.

swali la kujiuliza ni kwanini viongozi wa kuchaguliwa (madiwani) wakishaingia ktk nafasi zao hawataki maoni ya wananchi katika masuala kadha wa kadha....kama ni kweli walichaguliwa kihalali watawashirikisha wananchi ingawa labda kanuni za uendeshaji wa halmashauri haziwabani kufanya hivyo.
katika suala hili la uzinduzi wa jiji ,wakazi wa arusha wangeombwa kutoa maoni yao wasingeafiki chakula cha rais kiwe cha milioni 20 au kuwaleta comedy kwa gharama hiyo....kwa mfano je kungekuwa na ubaya gani kuzindua jiji kwa kufanya charity walk ya kusaidia uboreshwaji labda wa wodi ya akina mama pale mount meru na Rais akaalikwa kwenye hayo matembezi...au kuna tatizo gani mkizindua jiji kwa kufanya usafi mitaani....au kwa kuliomba azimio la arusha lirejeshwe na ile miiko ya uongozi ikawa ndiyo kipaumbele cha arusha.
 
Hizo pesa nijasho la walalahoi au nipesa za ccm? Naomba jamani wana JF mlio karibu mtujulishe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:target:
 
Kama hao The Comedy show moja wanalipwa milioni 25 show moja basi jamaa matajiri sana...kiwanda cha uongo at work.
 
ulitaka wapewe kiasi gani...?

wasanii wakilipwa kidogo mnalalamika.... wakipewa nyingi mnalalamika...

wapinzani acheni roho za korosho... ze comedy ni vijana wamejiajiri acheni wapate kifuta jasho chao...
 
Hao jamaa hamnazo kabisa. Nimeona wanajenga hospitali ya Kata ya Oloirien pembezoni mwa mto Kijenge, kama unaelekea Moshono
Sijui wanafikije hawa.Ngoja ikamilike tuone.
 
Kama hao The Comedy show moja wanalipwa milioni 25 show moja basi jamaa matajiri sana...kiwanda cha uongo at work.

Mkuu ulianza vizuri.............ulikomalizia umemalizia na kinyesi mkuu wangu
 
Hopeless! Kwann hzo pesa zisitumike kusafisha jiji coz linatia kinyaa!
 
Back
Top Bottom