CHADEMA yawasha moto Arusha. Mbowe azindua Mkakati mpya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,051
2,000
Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , leo kimeanza kupanga mipango mipya ya kukisogeza karibu zaidi na Wananchi , ambapo Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe ameanza kwa kufungua kikao cha Kamati ya Utendaji Mjini Arusha

Mwangómbe_Mbarali_on_Instagram:_“Mwenyekiti_wa_Chama_Taifa_Mhe._Freeman_Mbowe_akifungua_kikao_...jpg

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE
FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, tarehe 27 Mei 2021 siku ya Alhamisi, anatarajiwa kuzindua ‘Operesheni Haki,‘ ambayo itafanyika nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kampeni hiyo itazinduliwa jijini Arusha.

Taarifa ya Chadema imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.

Sambamba na hilo, taarifa ya Chadema imesema, Mbowe ameendesha kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho, katika Kanda ya Kaskazini, kilichofanyika leo jijini Arusha.

“Leo Mei 25, 2021, Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.
 

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,310
2,000
Vipi Lowasaaa fisadi au sio fisadi. CDM wakinijibu hili itakuwa vzr sana. CDM wapo kimaslahi zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom