Manispaa ya Arusha yatumia Milion 25mil kuwalipa Origino comedy ili kujaza watu mbele ya JK

Kesho Arusha itazinduliwa rasmi na Rais wa JMT JK kuwa Jiji.Sherehe zitakazofanyika kwenye eneo la Mnara wa mwenge,na baadae Rais atazungumza na wananchi w Arusha kwenye uwanja wa mpira wa Sheih Amri Abeid.

Kutokana na hali ya kisiasa Arusha kuwa tata,Halimashauri imeidhinisha 15mil kwa ajili ya kundi la sanaa la Original comedy,na 10mil kwa ajili ya msanii Diamond,katika kikao cha madiwani jana kulikuwa na ubishi mkali,kati ya madiwani wa ccm na wale wa CHADEMA.

Mtoa habari wangu alisema kuwa CHADEMA wanapinga matumizi makubwa kwa jambo la muda mchache wakati kuna shule hazina vyoo,na huduma nyingine ni mbaya.Jumla ya gharama zote za kuzindua JIJI ni zaidi ya 120mil,ikiwa ni pamoja na chakula cha mchana kwa mh Rais na ujumbe wake,kinachotarijiwa kuwa 20mil.

Mmoja wa madiwani wa CHADEMA Nanyaro alitoka nje ya kikao kwa madai kuwa hawezi kuwa sehemu ya maamuzi ya kifisadi

tutolee habari zako ambazo hazina ata,chembe ya,ukweli apa,mpuuxi we
 
Nitawashangaa watu wa Arusha kama mtaenda kwenye mkutano kwa sababu ya Diamond na Ze Comedy. Kama kweli mnachomsusia JK kina mantiki kwa maendeleo ya taifa, diamond na comedy ndo wataleta maendeleo? Hii inaonyesha kuwa ninyi si watu wa maendeleo bali na watu wa burudani. Kumbukeni hao kina Diamond na Ze comedy wanazidi kudhoofisha uchumi wenu kwa kulipwa mapesa mengi ambayo yangetumika kufanyia maendeleo ya mkoa wa Arusha. Mkienda kwa sababau ya hao jamaa mjue nayi si wazalendo.

Excellent! Nawaomba wakazi wa Arusha tuisusie hiyo hafla ili kuonesha kusikitishwa kwetu na matumizi ya hovyo ya hela zetu. Binafsi sinta jaribu kabisa kupita maeneo hayo. Ni ujin.ga kwenda nionekane umo wakati inside najiteketeza. Nimechukizwa sana.
 
Namwomba sana Diwani wangu Mh. Ephata Nanyaro aje atuthibitishie hili maana ametajwa kuliona japo hakukubaliana. Hii habari inaleta maumivu makali, hata Ndovu haishuki!
 
Last edited by a moderator:
acheni hata wakitumia bilioni hadi kuwa jiji ni kazi kubwa wamefanya acha wajipongeze babu kwa raha zao msiwaonee donge
 
sasa si upinge kwa hoja mbona unakuwa kama umekurupuka kutoka usingizini?

achana nae huyo gamba! Angekuwepo Arusha akadaiwa hela ya parking hadi siku ya Idd halafu hela zinaishia kwenye upumbav.u huu angepata akili!
 
achana nae huyo gamba! Angekuwepo Arusha akadaiwa hela ya parking hadi siku ya Idd halafu hela zinaishia kwenye upumbav.u huu angepata akili!


ikiwa hii habari ni kweli sijui hawa viongozi wanaazima wapi akili! kwanza watu wa Ar wanapenda hip hop watu dizaini ya diamond si issue
 
so mnataka comedy wakale police? diamond nikijana anaye jituma so mil 10 acha dogo ajiwekee mfukoni ni vijisenti kwa ccm
 
You know it could be great idea, pesa hizi zoooooore zinazotumiwa vibaya na serikali(wao hupenda kuiita Serikali ya CCM) tuziorodheshe..kwa kuwa tuna kumbukumbu nazo..na KAMA CCM ikitaka kurudi madarakani 2015, izirudishe kwanza!

du usisahau kujumlisha na gharama za shrehe za 50 yrs billion 64...kuapishwa rais kuapishwa wakuu wa wilay na mikoa semina za ulaji ngurudoto lodge na kadhalika
 
Kwa masikitiko makubwa tunalaani matumizi mabovu ya fedha yaliyofanywa na Halmashauri ya Arusha. Sisi hapa Arusha tunautamaduni wetu wa kuitikia mikutano na matukio bila kuvutwa na pilau na nyama.Tumepokea kwa mshituko mkubwa taarifa ya kutumika kwa mamilioni ya fedha eti kwa sababu ya kuzindua jiji!! Haingii akili kabisa kuswaga fedha hizo zote kwa siku moja wakati tuna mahitaji muhimu mfano soko la NMC ni kama makambi ya wakimbizi !! Jamani huu utamaduni wa pilau na nyama huku Arusha haupo jamani oneneni aibu kama mlizoea maeneo mengine huku si mahali pake huku watu wanahitaji maendeleo tuna shida ya maji, elimu, matibabu nk!!!

Narudia tena haingii akilini watu kuteketeza mamilioni ya fedha kwa siku moja na kesho wakaamka na kilio cha njaa!!

Jamani Swali….wote humu jamvini tuna akili mfano mdogo tu bila kwenda shule….kula hayo mamilioni ya fedha kwa siku moja au kuamka asubuhi na kukuta vyoo safi na vya kisasa pale NMC pamoja na Soko la Kilombero !!!

Mud acha huu uzi hewani unamafundisho muhimu kwa WATANZANIA!!
 
Ni kama CCM/Serikali walipoipandisha hadhi Lugalo Hosp. kuwa Hospital ya Rufaa, wakati kimsingi watu/madaktari wanataka huduma bora afya huko waliko/nchini kote. Kama haitoshi, akili ndogo ya JK imempa kudhani kwamba kuipandisha hadhi Arusha basi ndio maendeleo. Anasahau kuwa kero za maji, afya, elimu na barabara ziko pale pale.

It was a tragedy of historical proportion for JK to be a president, let alone for two terms.
 
WHATTTTTTTTTTTTT
ningejua nisingesoma hiii habari manake nimepata hasira za ghafla hata usingizi sitapata
natamani kumlipua mtu basi tu sina bastola na siko arusha
mashule mahospitali hayana vifaa afu wajinga wanachezea hela kwa staili hiyo
utasikia mijitu inasema kidumu chama so whattt? kwa mtaji huu tutafika?
Arusha simameni imara kataeni huu ufisadi wa kijinga na waliohusika wote wawajibisheni
 
Jiji la Ars ni dogo kwa miundomsingi wangetumia hilo fungu kujenga barabara mbadala kutoka na kwenda Mji mdogo wa Njiro

Folen ya barabara kuelekea njiro imekuwa kichefuchefu.
Na wala jitihada za kutatua au kuweka mbadala hauonekani.
Halaf wanaleta msanii anayekuja kuimba 'back cd' kisha wanamlipa 10m.
Na hao wavitimbi 15m.
Kweli CCM haina tena dira.0
 
Masikini kodi zetu! Kwani hilo ni Tamasha au ni shughuli ya kiserikali?
 
Tunajua siku hizi si MP, si magufuli wala wengine wakipita anga za Chadema basi huwa wanabeep na CCM oyeeee..wakiona mwitikio si mzuri basi huchomekea "peopleeeeeeeeeeeeees "halafu kelele wanayoshikia wanaamua vuta hisia kuwa ni kwa ajili yao.Magufuli alichomekea sehemu akijifanya kuwa alikuwa akiplay fair game.Sijui kama siku hizi CCM wanaruhusiwa itumia fasta kiaina kupendezesha show.

Sasa hili la ze komedi original kuzoea kupiga peoples wakiwa ktk luninga.Inaelekea Masanja alishalizoea bila kujua kuwa ni sehemu ya maneo yatumiwayo na CDM na si ile "watu wakasema peoplees" au pengine anajua na liamua tuu jifany akateleza ulimi na kuwachefua kidogo wanaompa ulaji mjini.Kwa wataalamu wanaweza tuambia kama haya yalikuwa makusudi au lah, na kama ni makusudi lengi likuwa ni kumpatia JK kelele kidogo kw ajili ya camera au ilikuwa na kuharibu au bahatai mbaya au vyote kwa pamoja?
 
Back
Top Bottom