Wachagga walitaka kuunda nchi yao (Chagga State), Mwl. Nyerere akaomba wasifanye hivyo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,938
Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi.

Mojawapo ya tawala ilikuwa ni dola ya wachagga (Chagga state). Dola hiii ilikuwa na Kiongozi Mmoja aliyeitwa Mangi Mkuu

Mangi mkuu aliteua Mamangi wadogo wadogo (RC, DC) mfano Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu, Petro Marealle, John Maruma na Thomas Marealle. Thomas Marealle aliibuka Mshindi katika Uchaguzi huo

Turudi nyuma Kidogo, mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya).

Huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa miaka hiyo hadi sasa ndio Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasiYa maendeleo..Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University.

Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe,
Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala.

Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state's iliyogawanywa. Shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru kutokana na umahiri wake katika uongozi lakini Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabilaMengine nje ya wachagga. Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake. Nyerere alisema Ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine.

Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

20230625_183656.jpg
20230625_183750.jpg
20230625_184022.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Kuna shida gani, SI ingekua nchi Yao, tambua kabla ya ukoloni kulikua hamna nchi inaitwa Tanganyika, kwa hiyo mipaka iliyopo iliwekwa na wakoloni, kwa Hilo hao wachaga kama walitaka kuwa na mipaka Yao walikua sahihi kwa wakati huo na ndio maana unasema Nyerere aliwaomba wawe watanganyika.
 
Back
Top Bottom