Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba wa Serikali ya Magufuli

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mange Kimambi: Mwanaharakati mwiba wa serikali ya Magufuli
Ikiwa ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu Rais John Magufuli wa Tanzania aingie madarakani, rais huyo ameonesha kutokusita kukabiliana na wapinzani wake, kuanzia wanasiasa na hata viongozi wa dini.

Rais Magufuli amethibiti shughuli za kisiasa za wapinzani. Mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa vyote vimezuiliwa, huku viongozi wote wa juu wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema wakiwa wanakabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani ikiwa ni pamoja na makosa ya kusababisha vurugu.

Serikali ya Rais Magufuli, ambaye ni muumini mzuri wa kanisa Katoliki, imetishia kuzifutia usajili asasi zote za kidini ambazo aidha zinajihusisha na siasa au kuzungumzia siasa katika mahubiri ya ibada

Lakini sasa rais huyo anakabiliana na upinzani mkubwa katika utawala wake kutoka kwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye ushawishi wake bado unawashangaza wengi.

Mange Kimambi, mwanamitindo aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa siasa, ndie muasisi wa maandamano yanayaopangwa nchi nzima kupinga kile anachokiita kuwa ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa haki za kiraia nchini Tanzania.

Mange, akiwa na wafuasi karibu milioni mbili kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambaye miaka miwili iliyopita aliutumia ukurasa wake Instagram kumuunga mkono Rais Magufulu wakati wa kampeni za urais, leo hii anautumia ukurasa huo huo kuitisha maandamano makubwa ya kumpinga Magufuli na serikali yake.

Mange ni mama wa watoto watatu anayeishi nao Los Angeles, nchini Marekani. Harakati za mama huyo kumpinga Rais Magufuli zilianza kwenye mitandao ya kijamii takribani miezi sita tu baada ya rais huyo kupinga kuonyeshwa mubashara kwa shughuli za bunge kwasababu za kiuchumi.

Wafuasi wake, wengine wakiwa watumishi wa umma, wamekuwa wakimtumia taarifa mbali mbali zikiwemo zile zinazoaminika kuwa nyaraka nyeti za serikali, kufichua kile wasichokubaliana nacho juu ya mwenendo wa serikali.

Wapo wengi pia ambao wamekuwa wakimtumia picha na taarifa kuonyesha hali duni ya huduma za kijamii katika maeneo yao.

Mange ni mmoja wa watu wa kwanza nchini Tanzania miaka ya mwanzo ya 2000, ambapo alitumia kurasa zake kuzungumzia maisha yake na marafiki zake pamoja na mitindo ya mavazi. Lakini Mange alizungumzia pia habari binafsi mbalimbali za watu maarufu waishio ndani na nje ya Tanzania, wakiwemo walimbwende, wanamuziki na waigizaji filamu.

Wengi wanaamini habari hizi ndizo ziliwavutia watu wengi kuanza kumfuata katika kurasa zake za mitandaoni.

-Wakati ambapo shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani zimedhibitiwa na watu kadhaa wamekamatwa na kushtakiwa kwa kuikosoa serikali kwa namna ambayo mamlaka haikupendezwa nayo, ukurasa wa Instagram wa Mange umefanyika sauti kuu kwa wakosoaji wengi wa serikali ya Rais Magufuli
Wakosoaji wa serikali na wanaharakati wa haki za binadamu wameendelea kuonya kwamba haki za kisiasa na uhuru vyombo vya habari na watu kujieleza vimeendelea kuminywa nchini Tanzania. Hata hivyo serikali imekuwa ikitupilia mbali madai haya.

Mara ya mwisho wafuasi wa upinzani walipoandamana mwezi Februari, makabiliano yao na polisi yalisababisha kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilline ambaye inaelezwa kuwa alipigwa risasi kwa bahati mbaya.

Ikiwa maandamano haya yatafanyika ama la, ni jambo ambalo wengi wanasubiri kuliona. Lakini muitikio wa serikali katika kuapa kudhibiti maandamano haya umetafsiriwa na wengi kuwa ni mafanikio ya ushawishi wa Mange kupitia ukarasa wake wa Instagram tu, jambo ambalo vyama vingi rasmi vya upinzani nchini Tanzania vimeshindwa kulifanya.
 
Ni mwendo wa kuhamisha magoli tu leo kwa vijana wa UFIPA.....Tuliwaambia mwanamke mwenye LAANA NA MCHAFU kama huyu kamwe hawezi ingiza nchi hii kwenye matatzo...Naishauri tu SERIKALI ICHUNGUZE CCTV CAMERA NA VIDEO MBALI MBALI ZA DIASPORA WOTE walioshiriki kwenye huu UHAINI NA KUCHAFUA TASWIRA YETU iwajue na iwaambie hatuwataki hapa nchini kwetu...Nina amini huko walipo wanajutia

Kuna waropokaji humu wanasema askari wamejazwa barabarani hili SI KWELI....tutupieni hizo picha za askari tofauti ya hizo za moshi na arusha(PHotoshop)......


Miongoni mwa VIONGOZI WA KAMATI KUU CHADEMA waliojionyesha hadharani kuunga mkono maandamano aliyoitisha MANGE(hapa ndipo tunaposema haya maandamano yalikuwa yanaratibiwa na chadema) ni huyu Msigwa....sasa tulio wengi tuna jiuliza mbona hajatekeleza kwa vitendo hata jimboni kwake kwa kuandamana?
Je,haoni hili linamfanya aonekane ni mnafiki.....kwa wananchi wake?
Pia haoni hili linamuondolea uhalali wa kusema wenzake vibaya?maana yeye mwenye kasema lakini kashindwa onyesha vitendo.....
Haoni pia hili litamuondolea kuaminika kwake tena kwa WATANZANIA pale BUNGENI?
Huyu nae aanze kujiandaa kiakili na kimwili...2020 Iringa mjini kwaheri
 
Mangekimambi wabongo wasikupoze kiaina, Wanaharakati wamekusaliti!! Hata viongozi na wafuasi wa upinzani unaowapigania wamekusaliti. Sweden wamekaribishwa na Balozi waeleze malalamiko yao, wamegoma, unachopigania hakitafika kwa muhusika Sababu Sweden nao waoga, wamekusaliti!!!
 
Ni mwendo wa kuhamisha magoli tu leo kwa vijana wa UFIPA.....Tuliwaambia mwanamke mwenye LAANA NA MCHAFU kama huyu kamwe hawezi ingiza nchi hii kwenye matatzo...Naishauri tu SERIKALI ICHUNGUZE CCTV CAMERA NA VIDEO MBALI MBALI ZA DIASPORA WOTE walioshiriki kwenye huu UHAINI NA KUCHAFUA TASWIRA YETU iwajue na iwaambie hatuwataki hapa nchini kwetu
Lakini kajaza askari na vifaa barabarani.Kuna la kujifunza hapa na kesho haiwezi kuwa kama jana!!
 
hongera sana Mange kitendo cha mapolice kukaa barabarani ni prove tosha kuwa ni wewe ni mwanamke shujaa... ....kwani nini wangapi wana Instagram account na serikali haiwatambui???? lol
Polisi hawaajiri ili wakae..walichofanya polisi leo ndio kazi yao ya kila siku..msifie kuwa shujaa wa kutukana labda.
 
Ameleta taharuki kubwa nchni.kwakuw jaribu limefeli ya maandamano watawala watakuwa na viburi hawataongoza watatawala wameshawaelewa watanzania ni waoga.wito wangu kwa viongozi wachukue lalamiko ya wanaotaka kuandamana wawafanyie kazi napia wananchi tusiwe waoga kueleza hisia zetu.utawala ukishakuwa wakimabavu huwa unakuwa na mwsho mbya mf gadaf na sadam
 
Hakuna cha mwiba hapa. Kama anajiamini si aje Tz. Huko kanda ya ziwa kuna msemo " mange ni sawa na kipumulio(kijambio) kinachohamasisha wengine kujamba" halafu kikabaki constant after the reaction. Watanzania wanajua Magu anatupeleka wapi. Yeye aendelee kuwashwa huko insta
Mange amekutoeni mapovu kama mmemeza jik.
 
Back
Top Bottom