Mange Kimambi amjibu Godbless Lema

Mange Kimambi amjibu Godbless Lema

Kutoka jijini Los Angeles huko Marekani, Mwanaharakati na Dada wa Taifa Mange Kimambi amemjibu Godbless Lema ambaye anadaiwa kulamba asali na kutuhumiwa mitandaoni kwa usaliti.

Ameanza kwa kusema Moja ya vitu Chadema imejijengea katika jamii ni kwamba wanapigamia utawala wa Sheria. Kwamba wanapigania HAKI, Ila Lema kwenye PRESS yake ya Jana ni wazi ameona ni vyema apitie njia za PANYA. Njia za kupigiana simu na kuongea na wakubwa fulani. Njia za kuomba huruma kwa wauwaji, njia za Kuwapigia magoti watekaji, Serekali haramu.

Mange ameendelea kusema LISSU yuko ndani mpaka sasa hivi kwasababu anapigania utawala wa Sheria. Angetaka kutoka kwa huruma za watu angeshatoka Kitambo sana.

Mange ameenda mbali na amekumbushia kuwa Mbowe ambaye aliingia JELA na Mbowe aliyetoka jela
walikuwa ni watu tofauti kabisa kwa Sababu alitoka Jela kwa huruma za Samia Suluhu ndiyo maana alipotoka akaamua kuiuza CHADEMA, gafla akaanza kuimba mapambio.

Akaendelea kusema kuwa LEMA anataka LISSU naye atoke jela kwa huruma za Samia ili naye akauze CHADEMA.
Mange ameendelea kusema LEMA ameshafika bei, sasa anajaribu kuimaliza CHADEMA.

Kwa uchungu mkubwa Mange ameendelea kusema Abdul anamdharau LEMA kupita kawaida, anamuona LEMA ni mshamba na poyoyo hasa baada ya kutetemeka alipopewa maburungutu ya pesa za damu. Mange amedai pamoja na Lema kumtusi na kumuita Mpumbavu bado heshima yake iko pale pale na kwamba Abdul ana muheshimu yeye Mange kimambi kupita kawaida. MANGE amedai Abdul alivyomfuata huko Marekani aligoma kuhongwa, alisimama kidete ila LEMA kanunulika.

Amedai kuwa LEMA akiziona hela za Abdul anatetemeka mpaka Abdul anamuona mshamba, anamcheka na kumuona popompo. Mange amedai kuwa Abdul ambaye ameishia darasa la nne amemteka LEMA kiakili kiasi LEMA amekuwa poyoyo. Kile ambacho Lema anaita ni Strategic Engagement ni janja tu maana ameshafika bei.

My take: Mange ameacha maswali ya msingi sana.
Je, imekuwaje chama kinachodai haki na sheria, mmoja wa viongozi wake anaenda kuomba huruma kwa wale wale wanaotakiwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria?

Basi watu watafakari, wakisema: Je, haki hudaiwa kwa sheria, au hutegemea huruma ya wenye mamlaka?
Hicho alichokisema Mange nilikisema hapa.

Baada ya Lema kusema, ndiyo kilikuwa kitu cha kwanza nilicho point out contradiction ya Lema kutaka fadhila za Samia wakati huo huo kila siku watu wa upinzani wanaimba kupinga nguvu kubwa za rais na kukataa mahakama kuendeshwa kwa amri kutoka juu.

The sad thing is, mahakama ilishaamuru Lissu apewe haki zake za kuonana na wanasheria wake na viongozi wa CHADEMA.

Sasa Lema anaenda kumpigia magoti Samia kuomba haki ambayo Lema kashapewa na mahakama?
 
Nyumbu sio wa kuwaamini kabisa
Huwa hayana mwelekeo, yanakwenda popote anapotokea mjinga mwenzao anapokwenda
Ndio maana wanaliwa sana na Mamba

1793665735697.png
 
Huyu kishawekwa kwenye mshikaki mmoja na Kabwe Zuberi.

Janja janja kujifanya wapo na wananchi kumbe wao wapo na matumbo yao tuu.

Lema akiivuka mishale hii salama, nitamuita Msigwa.
Labda abadilishe uelekeo. Otherwise, hafiki mbali.

Akumbuke kwamba Chama ni cha wananchi. It’s almost impossible to fight them and win!
 
Mange nonsense...

- Lema anadharauliwa sana na Abdul... ooh mimi Mange Abdul ananiheshimu sana..!

Hiyo heshima anayodai kupewa na Abdul yeye alijuaje kama anapewa?

Nae huwa anaongea na Abdul kwa simu sio!.

- Lema alipowekewa maburungutu ya pesa alitetemeka!, alikuwepo akamuona Lema akitetemeka?!

Anaishi kwa habari za kuambiwa kisha anaziamini kwa 100% then anataka na wengine tuziamini kama anavyoziamini yeye!

Kila siku ushahidi hana, ni kelele tu, ndio maana akipingwa anatishia kuwasemea wengine ili wafukuzwe U.S.

Kuwa mfuasi wa hiki kiumbe lazima uwe mjinga kama chenyewe, Lema aache kuhangaika na hii akili ndogo anapoteza muda.
PESA ZA ABDUL HAZIJAWAHI KUMWACHA MTU SALAMA. HATA WEWE NA LEMA ZIMEWAPITIA KWA KASI YA ELNINO.
 
Kwa uchungu mkubwa Mange ameendelea kusema Abdul anamdharau LEMA kupita kawaida, anamuona LEMA ni mshamba na poyoyo hasa baada ya kutetemeka alipopewa maburungutu ya pesa za damu. Mange amedai pamoja na Lema kumtusi na kumuita Mpumbavu bado heshima yake iko pale pale na kwamba Abdul ana muheshimu yeye Mange kimambi kupita kawaida. MANGE amedai Abdul alivyomfuata huko Marekani aligoma kuhongwa, alisimama kidete ila LEMA kanunulika.
Nimesoma yote huko juu kwa umakini mkubwa na heshima nyingi ya yaliyoandikwa huko na kutamani sana Mange aendelee kwa moyo huo huo.
Lakini mara ghafla kabisa, bila ya matarajio, nikafika kwenye hii aya iliyonivuruga akili yote na kurudi kule kule kwa Mange nimjuaye siku zote, na kunivunja moyo kabisa.

Haya mambo ya Abdul haya. Huyu Abdul, hivi yeye ni nani kudharau watu wote kiasi hiki? Hii inawezekana?

Kama Lema amenunuliwa, mwache anunuliwe. LLema hata siku moja hajawahi kuwa mtu mwenye 'conviction' ya chochote.
Sasa wewe Mange, nawe unatueleza habari za Abdul kukutafuta, unavyo vielelezo vyovyote.
Huyu dogo na ushetani wake wote, anao ujasiri wa kununua watu kama bidhaa nyepesi hivi?

Mange, sikiliza. Ukinipa ushahidi usiokuwa na shaka wa wewe kutaka kununuliwa, sitakuwa na mashaka tena na wewe juu ya mapenzi yako kwa taifa letu, na siyo harakati za kutafuta shibe tu.
It's as simple as that. Give us some convincing proof of your being sought as a commodity by that ruffian, evil boy.
 
🤑💰 haijawahi kumuacha mtu salama! Mange huyu huyu kuna siku mtasikia ana support chama cha maovu!
Na ni kweli, mange anawavuruga CHADEMA Ile mbaya na umbea wake, haka ka dada CHADEMA wakaangalie kwa jicho makini la sivyo katawavuruga KAMA KALIVYO VURUGA NDOA YAKE!
CHADEMA KALABAGAHO!
Hivi ni kiongozi yupi huko CHADEMA kazungumzia habari za Mange, kama siyo hao hao wanaofanya kampeni za kuvuruga chama hicho?
Bila kufikiri watu wenye akili timamu nao wanaanza kuimba wimbo wa kuwalaumu viongozi wa CHADEMA kuhusu anayoibua Mange!
 
Na kuhusu Mange aisee sielewi kwanini anapewa attention kiasi hiki, amekua kama msemaji wa Lissu na chadema kitu ambacho sio sawa
Kwa sasa hivi, utanisamehe sana kwa kufuru hii; lakini kati ya Mange na Lema kuhusu usalama wa CHADEMA, nitakwenda na Mange hivyo hivyo.

Lema kishafika kwenye hatuwa ambayo hawezi kurudi. Hili siyo swala la "uliberali au uhafidhina. Lema tayari yumo kwenye hatua za kuisambaratisha CHADEMA.

Bahati iliyo nzuri kwa CHADEMA, yale masalia yote ambayo yangemuunga mkono na kuleta vurugu nyingi ndani ya chama, yote hayamo tena.
Lema kabaki akipayuka mwenyewe bila ya kuungwa mkono huko ndani ya chama.
 
Haya mambo ya Abdul haya. Huyu Abdul, hivi yeye ni nani kudharau watu wote kiasi hiki? Hii inawezekana?

Kama Lema amenunuliwa, mwache anunuliwe. LLema hata siku moja hajawahi kuwa mtu mwenye 'conviction' ya chochote.
Sasa wewe Mange, nawe unatueleza habari za Abdul kukutafuta, unavyo vielelezo vyovyote.
Huyu dogo na ushetani wake wote, anao ujasiri wa kununua watu kama bidhaa nyepesi hivi?

Mange, sikiliza. Ukinipa ushahidi usiokuwa na shaka wa wewe kutaka kununuliwa, sitakuwa na mashaka tena na wewe juu ya mapenzi yako kwa taifa letu, na siyo harakati za kutafuta shibe tu.
It's as simple as that. Give us some convincing proof of your being sought as a commodity by that ruffian, evil boy.
Kitu gani kinakushangaza hapa? Hivi hujui jinsi ambavyo pesa ya mlipakodi wa nchi hii inavyotumiwa vibaya na hao mazafakas? Hujui, kwa mfano, kwamba kuna American lobbyists wanapiga pesa yetu kiulaini ili eti wawasaidie mazafakas kwenye sakata la muswada wa sanctions ambao bado unafanyiwa kazi na U.S. Senate?
 
Kwa sasa hivi, utanisamehe sana kwa kufuru hii; lakini kati ya Mange na Lema kuhusu usalama wa CHADEMA, nitakwenda na Mange hivyo hivyo.

Lema kishafika kwenye hatuwa ambayo hawezi kurudi. Hili siyo swala la "uliberali au uhafidhina. Lema tayari yumo kwenye hatua za kuisambaratisha CHADEMA.

Bahati iliyo nzuri kwa CHADEMA, yale masalia yote ambayo yangemuunga mkono na kuleta vurugu nyingi ndani ya chama, yote hayamo tena.
Lema kabaki akipayuka mwenyewe bila ya kuungwa mkono huko ndani ya chama.
Chama cha maovu kiko pembeni kikichekelea kama mtoto aliyepewa mapipi!
Chukuwachakomapema wako vyema sana sana kuvuruga WAKINZANI. KISA?! NJAA!
Viongozi toka ukinzani nawo wanaendekeza njaa sana sana!
 
Kitu gani kinakushangaza hapa? Hivi hujui jinsi ambavyo pesa ya mlipakodi wa nchi hii inavyotumiwa vibaya na hao mazafakas? Hujui, kwa mfano, kwamba kuna American lobbyists wanapiga pesa yetu kiulaini ili eti wawasaidie mazafakas kwenye sakata la muswada wa sanctions ambao bado unafanyiwa kazi na U.S. Senate?
Atasema leta ushahidi
 
Hii inathibitisha hakuna aliye mbabe mbele ya pesa, hadi Lema? Hajui ame dissappoint watu wangapi waliomuamini na wanaotaka haki itawale. Mapambano ya haki ni magumu sana kwa kweli.
Acha tu! Hasa wakati chama kinachangamka na kupata mwelekeo! Chukuwachakomapema know how to play the game! Kwanini CHADEMA hawajifunzi, kwanini wasiamuwe kuwa ngangari hata kama viongozi wana njaa? ILA TUSIDANGANYANE, mbele ya 💰🤑, KUSALITIANA NA KUPOTEZA MWELEKEO, LAZIMA ITOKEE!
 
Utakuwa mfuasi wa Mange, usinipe kazi ya kuutafuta umbea!
Mange nonsense...

- Lema anadharauliwa sana na Abdul... ooh mimi Mange Abdul ananiheshimu sana..!

Hiyo heshima anayodai kupewa na Abdul yeye alijuaje kama anapewa?

Nae huwa anaongea na Abdul kwa simu sio!.

- Lema alipowekewa maburungutu ya pesa alitetemeka!, alikuwepo akamuona Lema akitetemeka?!

Anaishi kwa habari za kuambiwa kisha anaziamini kwa 100% then anataka na wengine tuziamini kama anavyoziamini yeye!

Kila siku ushahidi hana, ni kelele tu, ndio maana akipingwa anatishia kuwasemea wengine ili wafukuzwe U.S.

Kuwa mfuasi wa hiki kiumbe lazima uwe mjinga kama chenyewe, Lema aache kuhangaika na hii akili ndogo anapoteza muda.
Yaani na wewe umejiona umefanya analysis. Du shule nyingine balaa kweli
 
Kutoka jijini Los Angeles huko Marekani, Mwanaharakati na Dada wa Taifa Mange Kimambi amemjibu Godbless Lema ambaye anadaiwa kulamba asali na kutuhumiwa mitandaoni kwa usaliti.

Ameanza kwa kusema Moja ya vitu Chadema imejijengea katika jamii ni kwamba wanapigamia utawala wa Sheria. Kwamba wanapigania HAKI, Ila Lema kwenye PRESS yake ya Jana ni wazi ameona ni vyema apitie njia za PANYA. Njia za kupigiana simu na kuongea na wakubwa fulani. Njia za kuomba huruma kwa wauwaji, njia za Kuwapigia magoti watekaji, Serekali haramu.

Mange ameendelea kusema LISSU yuko ndani mpaka sasa hivi kwasababu anapigania utawala wa Sheria. Angetaka kutoka kwa huruma za watu angeshatoka Kitambo sana.

Mange ameenda mbali na amekumbushia kuwa Mbowe ambaye aliingia JELA na Mbowe aliyetoka jela
walikuwa ni watu tofauti kabisa kwa Sababu alitoka Jela kwa huruma za Samia Suluhu ndiyo maana alipotoka akaamua kuiuza CHADEMA, gafla akaanza kuimba mapambio.

Akaendelea kusema kuwa LEMA anataka LISSU naye atoke jela kwa huruma za Samia ili naye akauze CHADEMA.
Mange ameendelea kusema LEMA ameshafika bei, sasa anajaribu kuimaliza CHADEMA.

Kwa uchungu mkubwa Mange ameendelea kusema Abdul anamdharau LEMA kupita kawaida, anamuona LEMA ni mshamba na poyoyo hasa baada ya kutetemeka alipopewa maburungutu ya pesa za damu. Mange amedai pamoja na Lema kumtusi na kumuita Mpumbavu bado heshima yake iko pale pale na kwamba Abdul ana muheshimu yeye Mange kimambi kupita kawaida. MANGE amedai Abdul alivyomfuata huko Marekani aligoma kuhongwa, alisimama kidete ila LEMA kanunulika.

Amedai kuwa LEMA akiziona hela za Abdul anatetemeka mpaka Abdul anamuona mshamba, anamcheka na kumuona popompo. Mange amedai kuwa Abdul ambaye ameishia darasa la nne amemteka LEMA kiakili kiasi LEMA amekuwa poyoyo. Kile ambacho Lema anaita ni Strategic Engagement ni janja tu maana ameshafika bei.

My take: Mange ameacha maswali ya msingi sana.
Je, imekuwaje chama kinachodai haki na sheria, mmoja wa viongozi wake anaenda kuomba huruma kwa wale wale wanaotakiwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria?

Basi watu watafakari, wakisema: Je, haki hudaiwa kwa sheria, au hutegemea huruma ya wenye mamlaka?
Kwanini kila mara hawa chadema na mange wanashutumiana kuhusu maburungutu ya Abdul?
Lissu, Mange, Lema kila wakiongelea habari za Abdul ni lazima waseme aliwahonga!
Wengine eti wamekataa, Wengine wamekubali!
Iweje wanaopokea rushwa za Abdul wanakaa chadema hiyohiyo na wanaokataa fedha za Abdul?
Hapo hamna chama ni genge la wapigaji tuu.
 
..Mange anasema yeye kukutana na Abduli ni sawa. Lakini Lema kukutana na Abduli sio sawa.

..Halafu Mange anadai yeye amekataa fedha za Abduli, lakini anadai Lema amechukua.

..Nampenda Mange akiwachafua Ccm. Simpendi akiwachafua Chadema.
 
Lema angekua na nia njema hilo swala wangelijadili kwenye vikao vyao vya chama ateuliwe mtu waone wanafanyeje na si kutoka yeye peke yake na kuucha uongozi wa juu eti yupo kwenye mikakati sio kweli kesi ipo sehemu ya hukumu yeye ndio kwanza anazungumzia mikakati hapana pana miguu katembea vibaya hapo..
 
Back
Top Bottom