Mange Kimambi amemponza Dr. Mwele Malecela?

Mange Kimambi amemponza Dr. Mwele Malecela?

Wasomaji watashangaa sana kwamba hiki nacho kimetoka kwako,
yaani Dr. Mwele afutwe kazi kisa kuwasiliana na Mange?
Huamini? Kwamba alichokifanya Dr Mwele ilikuwa ni lazima afukuzwe kazi?
 
Wewe unadhani Mwele kutangaza kwamba kuna watu wana Virusi vya ZIKA ni kosa kubwa sana? Kwenye mkataba wake na maelezo yake ya jinsi ya kufanya kazi (Job description) kuna maelezo kwamba haruhusiwi kutangaza matokeo ya tafiti mpaka awasiliane na Waziri?
Inamaaana huon tatizo la kutangaza TANZANIA kuna virus ZIKA..??

Wazee wa route ndefu msaidie huyu
 
CONSPIRACY THEORY....
Kama hujui..

Sasa Mange kafanya kipi au kasema kipi kilichokuwa hakijulikani kwa wengine mpaka ionekane kapata info za ndani kabisa

Sifa kubwa ya Mange ni kutoogopa wala kutojali madhara ya atakachokisema, wengine wamesikia na wanajua na wako kimya, yeye akisikia anasema,
HAKUNA CONSPIRANCY YOYOTE HAPO
 
Virusi vya ZIKA vipo ama havipo Tanzania? Tuanzie hapo kwanza.
Who imesema.havipo..
Dr amesema vipo so.sijui.kama vipo ama havipo

Sipo maabara mimi,..ila kitu chenye impact kitaifa kinataratibu zake za kureport sio kulopoka
 
, yeye akisikia anasema,
Akisikia toka kwa nani? Unataka kusema anayoyasema Mange huwa yamejulikana? Mbona aliposema kuhusu kujiuzulu ilikanushwa haraka? Kabla ya Mange kusema nani mwingine alikuwa amesema?
 
Wewe unadhani Mwele kutangaza kwamba kuna watu wana Virusi vya ZIKA ni kosa kubwa sana? Kwenye mkataba wake na maelezo yake ya jinsi ya kufanya kazi (Job description) kuna maelezo kwamba haruhusiwi kutangaza matokeo ya tafiti mpaka awasiliane na Waziri?
Mkuu hii post yako ni njema sana! Naomba utuwekee huo mkataba wake wa ajira ili tujue nani kamnyanyasa nani!
 
Kama kuna watu wanaona kwamba "kutumbuliwa" kwa Dr. Mwele Malecela hakuna mashiko kwa kuwa yeye alitoa tu taarifa ya kitafiti kwamba kuna watu wana virusi vya Ugonjwa wa ZIKA hapa Tanzania, basi wanaweza labda kukisia kwamba undugu wake wa zamani na Mange Kimambi unaweza pia kuwa umemponza.

Jee nani ana hakika kama simu ya Dr. Mwele ilikuwa haifanyiwi udukuzi na kugundulika kuwa anawasiliana mara kwa mara na Mange. Jee ni lini Dr. Mwele mara ya mwisho kuwasiliana na Mange na waliongea nini? Au kuna watu walitengeneza dhana kwamba zile "habari" za Mange zinatoka kwa watu wake wa karibu walio ndani ya serikali mmoja wapo akiwa ni Dr. Mwele.

Haiwezekani kwa hali hiyo ikatengenezwa dhana kwamba kama ni kweli mama alipigwa, haikutokea Daktari aliyemtibia mama aliongea na Dr. Mwele ama na mtu wa karibu na Dr. Mwele ambaye alimpa "ubuyu" ule na Dr. Mwele naye akampa Mange Habari "ile" na Mange naye "akailipua" kwenye mitandao?

Au Dr. Mwele hata bila ya dhana hizo hapo juu, aliwahi kuambiwa "Mkanye mwanao" lakini naye "akazembea" au "kupuuzia" kwa hiyo ikatafutwa nafasi na ikapatikana alipotoa taarifa ya ule utafiti? Au inawezekana ni mfuatano wa mambo unaotokea kwa nasibu tu kwa Mama kutumbuliwa na mtoto naye kutumbuliwa?

Hizi ni dhana tu, msitokwe na mapovu!!
Hii inaitwa Conspiracy na inakubalika..

Connecting the dots!
 
Sasa Mange kafanya kipi au kasema kipi kilichokuwa hakijulikani kwa wengine mpaka ionekane kapata info za ndani kabisa

Sifa kubwa ya Mange ni kutoogopa wala kutojali madhara ya atakachokisema, wengine wamesikia na wanajua na wako kimya, yeye akisikia anasema,
HAKUNA CONSPIRANCY YOYOTE HAPO
Suala au ishu ya mama pale mjengoni kutaka kuresign ulikuwa unalijua kabla?

Ishu ya bimkubwa kuchezea kichapo hadi akalazwa uliijua before..?
 
Na wengine wakajenga dhana kwamba,pesa za epa zilitumika kumuingiza kikwete ikuullu 2005/na za Escrow zikamsaidia bwana yule 2015.
 
Hizo taratibu zimeandikwa wapi au ni kitu cha kufikirika tu!!
So unadhan hakuna taratibu vipi...??
Tumejulishwa kwamba katumbuli a kwasababu flan..

Hayo ya mangi kimwambi ni yako,sidhan km mtukufu anatym na dada yule
 
I doubt kama Mange ana impact yoyote kwenye kufukuzwa kwa kwa Dr Mwele.

Though Mange amekuwa akisema Dr Mwele ambae ni Mama yake wa Kambo amekuwa akimpa warning sana kwamba aache kuisema sema serikali sababu wao (akina Mwele) ndio wanaonekana wanampa baadhi ya info.

Ninachoamini Dr Mwele amefukuzwa kwa kusema UKWELI yale yaliyopo kwenye utafiti wake. Basi.
 
Though Mange amekuwa akisema Dr Mwele ambae ni Mama yake wa Kambo amekuwa akimpa warning sana kwamba aache kuisema sema serikali sababu wao (akina Mwele) ndio wanaonekana wanampa baadhi ya info.
Hiki ukisemacho hakifanani na dhana yangu hapo juu?
 
Hakuna dhana ya kuondolewa Dr Mwele na Mange Kimambi,kumbuka waliotumbuliwa so far ni wengi na wengine wengi watatumbuliwa bila ya kuwa na uhusiano na Mange.

Je Kitwanga(Mambo ya Ndani),Mafuru (Hazina),Kazaura(TTCL),Dr Likwelele (Wizara ya Fedha),Bashe (TRA) walikuwa na uhusiano na Mange?
 
Mfanano wa matukio hauwezi kuyafanya kuwa tukio moja. Kila siku watu wanakufa, lakini wanakufa kama alivyokufa Jirani yenu?
 
Back
Top Bottom