maneo haya ni sahihi au ni makosa??????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

maneo haya ni sahihi au ni makosa???????

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by The Boss, Sep 30, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwanza kuna hili la 'mbele za mungu'

  kwani ni mbele za mungu au mbele ya mungu??????

  ukisema mbele za mungu ni kama unasema mbele zake mungu(his private parts)

  halafu kuna hili la nabii na mtume......

  mimi ninavyofahamu ni neno lenye maana moja.......

  sasa sielewi hapa kwa ni ni watumiaji wana yatumia maneno yote mawili kwa pamoja??????????
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mbele za mungu:
  Katika lugha sayansi ya lugha wataalam wanatuambia kuwa kutumia wingi kwenye kumtaja Mwenyezi Mungu kunaitwa (Majestic or Royal Plural au wingi wa ukubwa na utukufu au wingi wa kifalme). Au kwa Kiswahili inajulikana kama Lugha ya Majazi. Majazi ni kule kutumia wingi kwa kumaanisha mtu au kitu kimoja... Hiyo yote ni katika kumtukuza Mwenyezi Mungu katika ufalme na dhati yake.

  Tofauti ya Nabii na Mtume:
  Nabii ni mjumbe aliyetumwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka bila kuteremshiwa sheria au kanuni mpya ilhali Mtume ni yule aliyeteremshiwa sheria mpya. Hivyo, Nabii hutumia sheria ya Mtume aliyemtangulia.

  Kwa ufupi ni kuwa kila Mtume ni Nabii lakini si kila Nabii ni Mtume. Mtume ana daraja kubwa kuliko Nabii.  Allahu yaalam
   
 3. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MI naona kwa uwezo wangu X-Paster kamaliza. No addition no less.
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
   
Loading...