Maneno ya mama...we acha tuu!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno ya mama...we acha tuu!!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Bakulutu, Mar 11, 2012.

 1. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,920
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Kusema ukweli, mama ni mama.Nakumbukia na nayaona matumizi ya baadhi ya maneno aliokuwa akinieleza mama enzi nikiwa nakuwa..
  1. Usingizi hauishi mwanagu..
  2.Huwez kuacha kutamani mwangu,ila ishinde tamaa...
  3.Fimbo ya mbali haiui nyoka..
  4.Utu wako ndio utu wa mwenzio..
  5.KAZI HAZIUI(HAZITOI UHAI) mwanangu,fanya kaz unavyo weza ukiwa mzima..
  6..............
  7...........
  KUMBUSHIA NA WEWE YAKO...
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Maguzu masese (nguvu haziishi kwa kufanya kazi)
  shizugile shitashokaga kukano(ukipika chakula huwezi kirudisha kwenye ghala-maana yake usiwe mchoyo wa chakula)
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kumbe Kongosho kwenu ni Nagasaki....sikujua...
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Konichiwa?

  Boti boti dena!

  Tulihama Hiroshima mwaka 1973
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Bazengano batibisaga madako (majirani hawafichani masaburi - maana yake jirani akikuomba mzigo mpe ndio kusaidiana hivyo)
   
 6. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...chakula kikiiva ni kama mav* so usimnyime mtu msosi!
  ...babaenu anahangaika na ada yenu,someni,sisi kuna siku hatutakuwepo duniani,elimu ndio urithi wenu!
   
 7. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  etiii?...
   
 8. S

  Skype JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 7,284
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Gwanhana gete nkoi.
   
 9. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka nikiwa na kama 10 yrs , tulisafiri na Mama yangu mzazi kwenda Nrb siku moja tukiwa katika moja ya mitaa ya Kibira , mie nikiwa
  tunafatana na Maa tukakutana na mtu M'baba njiani akiwa anaongea peke yake.
  Mie nikawa namcheka yule M'baba , Maa akaniuliza JG unacheka nini ?
  Nikamjibu namcheka yule mtu anaongea peke yake huku akifatiza na kurusharusha mikono.
  Maa akanambia mwanangu usimcheke ukikua utayaona kwa nini watu wazima huongea peke yao.
  Naaam , early 90" ilitokea siku nimepatwa na mijimambo ! Na ndiyo siku hiyo iliponitokea kuongea man alone kwa street , nika'refar yale maneno ya Mama.
   
 10. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ....duuhh..!!
   
 11. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,683
  Likes Received: 874
  Trophy Points: 280
  Mtoto hapendwi na uchafu wake! Yaani usiache kumkemea mtoto wako/jirani kutokana na tabia mbovu kama vile matusi, udokozi, uchokozi, kudekadeka ovyo, na uchafu wa mwilini pengine ukichelea kuonekana unamnyanyasa mtoto au ukampenda sana mtoto ukashindwa na kusahau wajibu huo muhimu!
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,119
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  asanteni mliokumbuka,
  mimi mara nyingi nikukutana na mama
  napenda anipe historia ya familia/ukoo wetu.
   
 13. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  mi wangu alikua akipenda kunambia:
  Mwanangu siku hizi hakuna shoga kuna shonga!
  Shonga-in commorian manake balaa
   
 14. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,920
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Angel,...mbona kama kifaransa hivi au ni Kilingala??
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Pia alikuwa ananiambia 'Tabia yako ndo itakayokuhukumu, watu wanakuona'
  maana, ni matendo madogo madogo ya kila siku hubaki kwenye jamii inayokuzunguka.
   
 16. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Ni kingazija si wanachanganya na kifaransa wale
   
 17. M

  MandawaNaManenge Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mi alikuwa anapenda kusema:

  - Usingizi hauna reference. Ni kama usingizi hauna mwisho. Maana hata ukiuliza kati ya usingizi wa 12 March 2011 na wa 06 June 2011 upi mtamu. So alikuwa anahimiza kutopenda kulala sana maana hapana tija na hauishi.

  - Alisema pia tuushinde ubaya kwa wema. Hili neno ni zito saana maana yaliyojiri hapo kati, kama si neno hilo, basi unachuka panga unakata tamaa ( OSS jazz band tone- ' sasa jama nasema nataka kukata tamaaa)
   
 18. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wa kwangu alikuwa anaongea Kichaga sikumbuki ila alikuwa ananipa kichapo ile mbaya. Sasa ivi ndo najua kwa nini alikuwa ananipa mboko vile!
   
Loading...