Maneno ya kejeli ya mume wangu

Mungu akujalie hekima katika hili!
Hivi jitu lenyewe hata halilali nyumbani hata huyo mtoto atapatikanaje?
 
Pole dada ila u mvumilivu....me nadhani chagua furaha yako....kama unahisi utaweza vumilia mikiki mikiki yake for the rest of your life tulia nae. Ila kama unaona mbele giza sepaa tuu!! alitakiwa kukutia moyo kwa kutokuwa na mtoto nasio kukunyanyasa.
 
Toka hapa...una matatizo sana ndo maana huzai

No, nadhani this is the stupidiest reply ever kwenye hii mada, ishu ya kuzaa au kutokuzaa kashaeleza huyu mwanamke sio vyema kumjibu kipumbavu hivi,wanawake mliokosa wanaume mbona mnakua na majibu mabaya hivi. sio yeye aliesababisha usiolewe dada, kua na staha na wanawake wenzako.
 
mh!!! ninavyojijua mimi! ningekuwa hata nilishasahaugi kuwa niliwahi kuolewa na huyo mtu! kha! kama kuna kitu siwezi vumilia duniani ni 'kudhalilishwa'. Yaan...dah! BWANA niepushe na jaribu kama hili, maana wanijua vyema kiumbe wako! loh
 
Duuu!!! Katika siku ya leo tazama au sikiliza mwimbo wa Christina shusho mapito kisha unipm
 
aise dadangu una limoyo,ningekuwa ni mimi ningeshajiweka pembeni muda,kama vipi muache tu kwani ye amekuwa kiroba cha unga kwamba ukimkosa utakufa njaa? aiiiih!
 
haya mambo haya! puuuuuuuuuuuuuu! Asprin hebu tuonane baadae tukazie ndoa yetu! kuna mwenye swali??

Mwenye swali ntadeal naye mimi wife. We tangulia, uwashe AC kabisa. Mi nshajinywea grants za kutosha.

Nikukute without puliiiiz...
 
hiyo kazi ni ndogo dada yangu,niPM nikupeleke kwa mganga.huyo atakuwa anakupikia,anakufuria na vyote unavyotaka niPM tafadhari

Duuh usimdanganye mwenzio kama ni wa ki dunia Mganga mzuri na mkweli ni Yesu tuu. Waliobakia wote ni matapeli tuu... Thanks...
 

Binti,

Unapoteza muda hapo, huyo bwana hatakufaa kwa shida wala kwa raha...

Ukizingatia kwamba bado hujapata mtoto, ni fursa safi ya ku-move on na nina imani kwamba you will get kids ukitulia na kufocus kwenye matibabu, kazi na mapenzi mapya

You'd rather be alone that a person who ruins your life

Hapo sijazungumzia hatari za magonjwa na mikosi mingine
 
Jamaa anachezea shilingi chooni ukiondoka atajuta
 
Mimi leo nilikua nafikiria kama yasingekua matatizo yaliyonipata nisingejua ukuu wa Mungu. Leo hii natambua kua ukiwa kwenye matatizo ndo wakati wa kumuhitaji Mungu zaidi. Maana biala hayo matatizo huwezi jua ukuu wa Mungu katika maisha yako. Hata bila hayo matatizo huwezi kusimulia wengine ukuu wa Mungu kwa ushuhuda ambao umeuona kwa macho yako ya nyama.

Mungu hawezi kuja physically kwako, watu wengi wamekutana na Mungu live walipokua kwenye matatizo kama yako. Jaribu kufuatilia ya watu ambao leo hii ni mashuhuri walikutana na changamoto katika maisha yao. Mimi wakati mwingine naangalia ndoa ya cliton na kusema kunawakati matatizo ni changamoto tu katika maisha. Ukikumbuka clitton alipata kasfa kubwa ambayo ingekua kwa mwingine mkewe angekua alishoondoka na hakuna ndoa. Angalia leo hii ndoa ya clitton ni moja ya ndoa strong duniani.

Pia hua nafikiria silaha ya upendo katika maisha ni best silaha kuliko zote. Mimi nafikiria tu kama KIng Martin Luther angetumbia jino mkwa jino principle, kungekua na Rais mweusi marekani?. Jibu ni hapana kwa mawazo yangu kwani asingeshinda vita, angekufa kabla hajamaliza kazi iliacha historia yake katika dunia hii. Hivyo upendo no silaha kuu katika kila jambo na upendo unathawabu kubwa sana kama unampenda mtu anaekuchukia na kukuudhi. Ikifika kesho atajua kua yeye alikosea na ukuu wa Mungu utaonekana katika maisha yenu.

Hivyo kifupi tu, upendo ndo silaHA KUBWA na namaanisha upendo wa kweli. Na upendo wa kweli huja baada ya msamaha wa klweli kutoka moyoni. Nakushauri msamehe kwa yote alikwisha kukutendea na ambayo bado hajakutendea, muoneshe kua unampenda lakini mwambie Mungu wako anampenda zaidi kuliko wewe upendavyo. Lakini pia jua kua unamuhitaji Mungu zaidi kuliko chochote maana hata watu hawawezi kukusaidia, msaada wa kweli uko kwa Mungu tu. Na upendo wa Mungu kwetu sisi hauna kipimo na unaanzia pale msalabani alipomtoa mwanae wa pekee ili afe kwa ajili yetu. Ni nani hawezaye kukupenda kiasi hiki? ukipata majibu utajua upendo wa Mungu.

Na ukuu wa Mungu unaangaliwa kwa kukumbuka aliyokutendea kabla, kama ameweza kukuweka hapo ulipo ujue anaweka kukupeleka mbele zaidi. Mkumbuke ayubu majaribu aliyokutana nayo hakuna mtu anaweza kuyaweza katika dunia ya leo, hivyo wewe jaribu lako ni dongo sana, unamuhitaji Mungu zaidi. Kwani ayumbu pamoja na hayo yote hakumuacha Mungu alipokimbiwa na mke wake hakumuacha Mungu, alipofiwa na watotowote, hakumuacha Mungu. Hivyo ni nini kitutenge na upendo wa Mungu? hakuna!

Unamwitaji Mungu zaidi, anzia kwenye msamaha kwa kusamehe wengine wanaokutendea mabaya, halafu rudi kwa Mungu akusamehe na uanze safari mpya ya matumaini ya kwenda mbinguni. Maana hakuna binadamu atakupa suluhu katika tatizo lako, mkimbilie Mungu tu. Ukisamehe linafuata hapo ni upendo, hii ndo nguzo kuu ya mahusianao yetu na Mungu. Maana Mungu anasema huwezi kumpenda yeye usipompenda binadamu unaemuona. Baada ya kuanza maisha mapya na Mungu tegemea kupata ushuhuda mkubwa katika maisha yako kama sala na abrahamu walivyopata ushuhuda wao uzeeni sana, wakati kila elimu ya dunia inakataa. Ikiwa ngumu kusamehe anza kuomba Mungu akupe roho ya kusamehe, maana yeye ndo msaada wetu.


 
Pole sana , chukua likizo ya ndoa.

Hata akichukua likizo ya ndoa bado furaha ya maisha yake hayapo, kwani hata huyo mume Mwengine akipata jee kuna uhakika gani ya kupata mtoto? Wanaume ambao hawajapata watoto sio rahisi kuivumilia ndoa bila ya mtoto, ni ngumu sana sana.
Suala langu kwako, jee mulichukua hatua gani kukabiliana na matatizo yenu ya kupata mtoto?

Mumeo ana stress za kutopata mtoto hivyo cha kufanya wewe kwanza kukaa na mumeo ongea nae vizuri mpe matumaini.

Jengine nendeni kwa wataalamu wa masuala ya kupata mtoto, kuna njia za kitaalamu za kupata mtoto. In sha Allah mutapata mtoto.

Kwa mungu hakuna kubwa, kuna mtu ambae namjua, alikaa muda mwingi bila ya kupata mtoto, walifika India kwa ajili hio lakini haikufua dafu, itapita kama miaka 2 hivi Allah akawajalia mtoto, hivi sasa wana watoto wawili chap chap baada ya kusafa muda mrefu.

Nikuulize suali Jengine? Jee mumeo nae ana miaka mingapi umri wake?
Nayo pia inachangia kuchelewa kupata mtoto kutoka kwa mwanamme ambae umri wake mkubwa na kuchelewa kuzaa mapema, hilo nimefanya uchunguzi, tatizo sio wewe hata mumeo tatizo.

Kama kidume kweli mbona hao wanawake zake njee hakuna alie zaa nae kama kweli yeye hana tatizo?

Hivyo nakuomba kaa na mumeo, jadilini kwa kina suala hili, ndoa inahitaji uvumilivu mkubwa.

Jengine zaidi kuwa makini na hili jonjwa la siku hizi,asije kukupatia, kama unaona ni hatari kwako usidai talaka, nenda nyumbani kwa wazazi wako pumzika mpaka pale atakapo kuwa tayari mumeo kukuhitaji na kubadilisha tabia yake. Tena hayo kwa makubaliano baina yako na yeye na wazee kama ma judge.

Shukran
Nakutakia ndoa njema
 
kwani nyie wanawake huwa nasikia mara tunakutana kimapenzi na mume wangu mara mbil tu kwa wiki!!!. ivi kiuharisia huwa mnataka kufanya mapenzi na waume zenu mara ngapi kwa wiki?. wanaume wengi hawapendi kufanya mapenzi kila siku, na ata akifanya ni miezi miwili anabadilika ratiba.
 
Tafuta Kidumu aiseeee,au nawe akitoka nawe toka jino kwa jino,aone uchungu wa kugongewa
 

Labda wewe mlo mmoja, sisi wanaume wengine tuna gonga kila siku anytime hata mchana, hata sebule, jikoni unakopata. Hivi umekaa na kuandika upuuzi huu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…