Maneno ya Jaji Warioba kuhusu Katiba Mpya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amepigilia msumari kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya, na kutaka maoni ya wananchi yasipuuzwe kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza walishirikishwa kuitengeneza.

Akihojiwa jana kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha ITV, Jaji Warioba alisema ni muhimu mchakato wa Katiba Mpya ukakamilishwa kwa kufikiria hatua ya kuchukua kuanzia ilipoishia mwaka 2014.

Alisema Katiba ni muhimu na imefika hatua kubwa ya kuwa na katiba mpya, kwani sheria na Tume iliundwa ili kupata maoni ya wananchi na ilizunguka nchi nzima kuyakusanya, na mambo yaliyokuwepo katika Rasimu ya Tume yalichukuliwa Bunge la Katiba yalitokana na maoni ya wananchi.

Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, alisema Katiba za zamani walikuwa hawaulizwi wananchi na kwamba kwa mara ya kwanza ya mwaka 2014 iliyoandaliwa ilipata maoni ya wananchi, hivyo maoni ya wananchi yasidharauliwe.

“Usije ukasema Katiba siyo muhimu wakati wananchi wanasema ni muhimu, tulipofikia ni hatua muhimu tunachotakiwa ni kutafakari kwamba tunamaliza vipi na lini, hata nilipomsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan, hakusema kwamba tusimalizie hiyo, anazungumzia lini.”

“Na mimi naona kwa sasa hivi ni lazima tufikirie hivi ni lini tunatakiwa tukamilishe, tutumie utaratibu gani, mwaka 2014 ilikuwa twende kupata maoni ya wananchi lakini kwa mazingira ya wakati ule haikuwezekana sasa muda umepita inabidi ile Katiba Inayopendekezwa ifanyiwe marekebisho,” alisema.

“Wanaosema wanataka Katiba ya wananchi wakati mwingine nasikiliza sana hawa wanataka Katiba ya wananchi au wanataka Katiba ya wanasiasa kwasababu wanachozungumzia sana ni Tume Huru ya Uchaguzi, Rais kuchaguliwa kwa asilimia zaidi ya 50, matokeo ya Rais kuwe na uwezekano wa kupeleka malalamiko mahakamani kuwa na mgombea huru,” alibainisha.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, mambo hayo ni muhimu lakini msisitizo wa wananchi ilikuwa ni hiyo au walikuwa na mambo yao, wananchi walikuwa na mambo mengine waliyosisitiza mojawapo kuporomoka kwa maadili ndiyo maana kumekuwa na rushwa, ufisadi na hakuna maadili hivyo walisema ni lazima jambo hilo liingizwe kwenye Katiba.

Aidha, alisema walizungumzia tunu ya taifa ya misingi na miiko ya uongozi, haki za binadamu na malengo ya taifa, hivyo kwakuwa Rais alikubali kukutana na wanasisasa wa vyama vya upizani wazungumze ni Katiba ya aina gani wanayoitoa kwa wananchi na kwa kipindi gani waipeleke.

“Ukiangalia mazingira yenyewe hatuwezi kuipata Katiba mwaka huu, kwa sababu inabidi twende kwa wananchi na hiki siyo kipindi cha kuwakusanya kwa sababu kuna hatari ya Corona, ni lazima tuwe na msimamo wa kitaifa tuamue lini tutakamilisha hii ama tunakamilisha kila kitu kwa wakati mmoja ama tunachukua sehemu flani flani tunazikamilisha ikifika wakati flani tunakamilisha yote ile,”alisema.

“Mimi nadhani wengi wanajua umuhimu wa Katiba, ushauri wangu wanasiasa wakubali mualiko wa Rais wawe tayari kuzungumza kwa makini siyo kwa mapambano kwa sababu hili ni suala linalohusu wananchi wazungumze wakubaliane wakifanya hivyo itakuwa rahisi kupata ridhaa kwa wananchi,” alisisitiza.

VIONGOZI WASIKILIZE
“Mimi napenda utaratibu wake wa kukutana na wadau mbalimbali, na hayo yaliyopita yanaweza kubosheshwa jambo la kwanza ni mikutano hii iwe ya Rais anapokutana na wadau basi tulenge kwa wale anaokutana nao, isiwe ni nafasi ya watu wengine kueleza mambo yao.

“Tumeona katika mikutano hasa ule wa vijana walijitokeza viongozi wengi kuzungumza na ikachukua muda wa saa tatu hadi nne kabla Rais hajazungumza, wananchi wanataka wamsikilize Rais, ukichukua muda mrefu hivyo mtu hawezi kukaa, hivyo unapotekea mkutano wa Rais basi ufanywe kuwa wa Rais hao wengine wana nafasi nyingine,”alisisitiza.
Jaji Warioba alisema ni vyema anapokutana na wananchi ni vizuri akawasikiliza kwanza na kwamba ilivyoonekana viongozi walizungumza zaidi, na kwamba njia sahihi ni kama alivyokutana na sekta binafsi.

NIPASHE
 
Huyu mzee huwa anawaza nn

USSR
 
Huyu ndiye alipaswa kuwa rais siyo hizi takataka nyingine.
 
Haaaaa haaaaaa
 
Back
Top Bottom