Bongo imekuwa kama Colombia, Bolivia au Mexico.. Watu wanatekwa kirahisi sana, kuliko hata JB anavyotekwaga kwenye filamu za bongo movie.. Na maisha yanaendelbea.. Tanzania imegeuka TANZAGIZA.. Yaani imefikia kipindi mtu hata ukichelewa kurudi kazini familia yako inaanza kulia.. Faru John ni mnyama.. Lakini baada ya kupotea aliundiwa tume kujua yupo wapi? kwa nani?! na anafanya nini?!.
(Kufuru hii)...
Au sababu anafanana na jina la mtawala?!..Jibu baki nalo.. Binadamu wanapotea, wengine wanazikwa kikatili ndani ya mifuko ya sandarusi.. Bila hata takbirah au sala ya baba yetu..Na hakuna tume yoyote inayoundwa..
Hii amani bandia iliyopo leo siku ikipotea. Tutaitafuta kama cheti cha form four cha Daud Albert bashite.. Na hatutaiona kamwe.. [HASHTAG]#Haki[/HASHTAG] na usawa kwa watu wote.. Ndio mlinzi bora wa amani kuliko hata bunduki mabomu na vita. Tusiichezee amani.
Mrudisheni Roma bhana.. Mimi nipo kusoma biblia hapa. Mithali imeandika.. Mkuu aliyepungukiwa akili uwaonea watu sana.