Maneno mazuri ya kumrudisha mpenzi wako aliyekuacha

Vw Jr

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
377
338
..Kwa Maneno Haya Lazima Akusamehe..

..Usiniache kwenye Dunia ya maumivu,usiniache kwenye mvua ya sononeko, njoo unirudishie tabasamu kwenye maisha yangu. Njoo unibusu na busu lako litokomeze maumivu haya.. Bado nahitaji joto tamu la huba toka kwako,,, njoo baasi unifute machozi,,,nirudishie zile siku tamu ambazo baridi iliponisumbua usiku kimbilio langu lilikuwa kumbatio kwenye mwili wako...Bila uwepo wako kwangu,tafsiri ya neno MAISHA ni ukatili ,,njoo baasi unambie unanipenda tena..


..Kila ifikapo usiku nimekuwa nimekuwa kiumbe nayezama kwenye bahari ya Machozi. Sababu moyo wangu umepondeka sana,,, Nirudishie Furaha katika Maisha yangu.. Njoo na Koleo ya Upendo ili niitumie kulizika neno HUZUNI. Tabasamu lako ni wakili pekeee awezaye kunitoa ndani ya hili gereza la mateso ya upweke,,,


..Njoo ufungue kinywa chako chenye meno meupe yaliyo katika mpangilio sanifu.. Kisha utoe kibali ili ulimi wako unitamkie kuwa bado UNANIPENDA. Njoo basi hata unidanganye kuwa bado Nina THAMANI kwako ili tu unisogezee siku za kutazama hii dunia inukayo jasho la dhambi..


..Yanini Nikudanganye kuwa nitakuhonga Dunia? Bila ulazima,, nijiongezee kifurushi cha dhambi ya kujitakia??.. Ilikhali najua dunia njia?. Neno NAKUPENDA sitoacha kukuambia,, sababu neno NAKUPENDA licha ya uchache wa herufi zake,, Lina Thamani zaidi kuliko chochote chini ya hizi Mbingu,, Hasa linaposimama Kama Kamusi kwenye swala la kuzitafsiri hisia za Moyo ulobeba shehena nzito ya UPENDO wa Kweli KAMA HUU UPENDO NILIONAO KWAKO..
 
Binafsi siwezi kubembeleza huo mtihani wakubembeleza nilifeli siku nyingi sana akitaka kwenda huwa namtakia safari njema hivi viumbe vipo vingi sana
 
Back
Top Bottom