Namna ya kumrudisha X wako bila ya kuumiza kichwa wala kuonekana king’ang’anizi

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
493
478
Ni watu wengi walio katika mahusiano uachana na kutaka kurudiana. Neno Ex limekuwa ni neno maarufu sana na lenye kuonyeshwa uadui, visasi, uchafu, sumu, mkomoeni, kukosa uaminifu, tamaa, mapungufu katika mapenzi, kupitwa na wakati na kitofaa, bila kujali jinsia ya kike ama ya kiume wote huwa na haki ya kufanya maamuzi ya kurudisha mapenzi aliyopoteza.

Zipo mbinu na namna unayoweza fanya kurudisha upendo uliopoteza, kama ifuatavyo:

Onyesha ulikosea kumuacha mwanzo
Zifungue hisia zako kwake kupitia watu wake wa karibu, mwanamke au mwanaume anapozipa taarifa njema za kumhusu yeye kupitia watu wake wa karibu, uona fahari na kuwa tayari kutaka kumsikiliza mhusika iwe ni kwa nia ya kumpokea au kumchora.

Onyesha yeye ni wa thamani
Kama ulianzisha mahusiano mapya basi onyesha udhaifu uliokutana nao, jifungue namna unavyommisi, kama huku anzisha mahusiano mapya basi eleza/ onyesha ugumu uliokutana nao wakati ukiwa hauko nae.

Binadamu ni mwepesi kusamehe au kukufikiria na kuruhusu umkaribie ikiwa umemwona ni mwema na thamani yake umeionyesha inaishi ndani yako.

Mkaribie
Usiwe mtu wa kuongea tu kutamani kurudiana nae na ikiwa hata kumsogelea huwezi, unamuogopa, umejawa wasiwasi wa atakuelewaje.

Unapaswa kujisogeza kwake kupitia anachokifanya, mazingira anayoishi, kimawasiliano, kimarafiki na kifamilia. Unapomkaribia, unampa nafasi ya kukufikiria na kukuchukia. Hata kama atakuchukia ni rahisi sana kukuelewa pindi ukiwa umekaribia na kuonyesha unatamani uwepo wake. Jiingize kwa namna yeyote salama uwe sehemu ya maisha yake.

Mjali kama mtu wa karibu kwako
Wengine uanza kwa masihara, kushauri, kukomenti statasi zake, kumsalimia, kumpa vijizawadi vya kawaida visivyoonesha mapenzi. Lazima utambue na hadhi yake na hali yake, unaweza kuwa mtu wa msaada kwake katika mahitaji yake kama chakula, mavazi, urembo,vocha, ugonjwa, sherehe nk. Hii inafanya aweze kuirudisha thamani yako taratibu.

Msifie
Unapaswa kuwa jicho lake la kumsifia alichovaa, anachofanya na alivyo yeye. Penda sana kumsifia kwa wakati uliomkuta na sivyo mlivyokuwa huko nyuma. Mwanamke ama mwanaume upenda kuonekana amefanya mazuri baada ya kuachana, hakuna ex anayependa kuambiwa amefubaa.

Mkumbushe mazuri yake na yako unapopata nafasi
Kama ni kwa ujumbe au kuzungumza nae hata kama kwa muda mfupi. Unapomkumbusha mazuri yako unamsaidia kuzivuta kumbukumbu zake na zako na kulinganisha kuona ipo haja ya kuendelea nawe au hapana. Watu katika mahusiano huwa na tabia ya kuachwa, kujitenga, kuchukia, kutamani, kukumbuka na kurudia mahusiano.

Mtambue kwa zawadi
Ili kuonyesha anaishi hisiani mwako na unania nae, basi uwe mtu wa kumpatia vitu vidogo vidogo vya kula, kuvaa nk. Zawadi ina thamani yake, ila ndio unapaswa kujua aina ya zawadi na nguvu yake kwa unayempelekea. Zawadi ina maana nyingi moja ni kumuonyesha mtu yeye ni wa muhimu kwako.

Usiwe na papara
Unaposaka penzi kwa Ex wako upaswi kuwa mwenye pupa na kuonyesha ni mtu mwenye tamaa sana ya vitu vya hisia. Unapaswa uwe mpole na mtaratibu, kila analokueleza lisikie kama ni zuri basi inshalah ila kama ni baya unapaswa kusikiliza na kuwa mpole na kujipanga upya kukivuka. Lazima ujue Ex huwa na jazba, matusi, dharau, visasi na wengine ngumi mkononi, lakini yote hayapaswi kukutisha maana umeyatengeneza mwenyewe.

Onyesha wewe ni mtu tofauti
Jifunze yale uliyokosea usiyarudie tena, kuwa romantiki ( mnogeshaji kihisia), jiongeze kwa kila kitu, mheshimishe na mtunze bila kujali anakuchukuliaje kama rafiki, mshenzi fulani au mpenzi. Unapokuja kivingine uonyesha umekua, umebadilika, upo tayari kufanya nae maisha, umejua mapungufu yako na uko tayaro kuishi atakavyo.

Hivyo suala la kuachana lipo halifanyi kuwa ndio chanzo cha kuua mapenzi yaliyopo katika hisia za waliopenda awali, maana sio wote uachana kwa sababu moja, lazima tukubali hata mtenda mabaya uamini ipo siku utakuwa mwema na kujiokoa katika mabaya.

Unapoona wenzio mahusiano yao yamekuwa salama ina maana walikuwa kama wewe ila sasa ni tofauti. Ogopa sana kufanya maamuzi ambayo baadae yatakufanya ujutie na unapojua umekosea huna haja ya kujizungusha bali omba radhi, kama anayekupenda atakupokea.

20221028_161814.jpg
 
View attachment 2400532
Hadi upambane kumrudia unakuwa umesahau nini kwake?

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Kwa hesabu zangu nilizopiga haraka haraka kwa kutumia ile njia ya magazijuto,jibu limekuja ya kuwa kumrudia Ex(mpenzi) ni gharama kubwa kuliko kutongoza upya lkn ni rais sana na ninafuu kumrudia Ex(mke wa zamani aka mtaraka wako)
 
... sipashagi makabichi...

BTW kurudiana na X ni kama kumsukuma mlevi vile.
 
Kwa hesabu zangu nilizopiga haraka haraka kwa kutumia ile njia ya magazijuto,jibu limekuja ya kuwa kumrudia Ex(mpenzi) ni gharama kubwa kuliko kutongoza upya lkn ni rais sana na ninafuu kumrudia Ex(mke wa zamani aka mtaraka wako)
Hatari
 
Ni watu wengi wanaotaka kurudia mahusiano, wanataka kuanzisha mahusiano mapya na wnao endelea kutunza mahusiano yao. Hivyo ni haki ya kila mtu kuona lipi ni jema kwake katika mapenzi.
 
Kwan Marioo anasemaje
Ni wimbo tu ila katika uhalisia wapo walio acha wapenzi kwa maneno ya kuambiwa alafu baada ya kuujua ukweli. Wanahaha kuyafuta makosa yao. Ama amepata mpenzi mpya alafu ni pasua kichwa anaona eeh bora kule nilipotoka.
Mapenzi ni nouma
 
Sawa
 
Back
Top Bottom