MANDATORY LISTING: Was DSE chair forced out over letter to JK?

Mkandara nimeyasoma hayo maneno. Nadhani utakubaliana na wachangiaji wengi hapa kwamba FDI na economic fundamentals ndiyo zinazostimulate market developments and listing. Kwahiyo nadhani hata tundiko lako lililopita nalo ni batili. Economic theories hazikubaliani na hili kabisa. Kuna mchangiaji hapo juu kasema wazi, sasa ni km wanaalika investors wasiona capital waje kuiba. Hivi km tunadhani kuna wizi kwenye tax, inamaana tunashindwa kabisa kuweka mechanisms za kulinda hayo. Sometime hawa watu wa TRA wanahakiki statements za makampuni inamaana hawana mechanisms za ku uncover wizi huo? Achilia mbali hilo, hivi nani aliyesema listing itapunguza kuibiwa? Hata nchi zilizoendelea shareholders hawana nguvu km wanavyotaka kutuaminisha wanasiasa ispokuwa Marekani huko ndiyo kuna kazi. Km tunaamini tunaweza kuraise capital internally kuna haja watu wa investment centre kusafiri kila leo kwenda kuita wawekezaji?
Hv serikali inadhani duniani kooote sehem iliyobaki kwa Uwekezaji ni Tanzania pekee. Ukweli nchi yetu ni masikini, na katika eneo ambalo lingeweza kutuinua ni sekta binafsi lkn km tutaendelea na sheria zisizoeleweka itakuwa ni kichekesho. Maana hata hao Watanzania ukiondoa wanasiasa wengi wao hawana uwezo wa kununua share na hata hawafaham shares ni nini! Tufike mahali kwenye masuala ya kitaalam wanasiasa wakae kando. Inawezekana kbs wapo wataalam walijadili hili lkn kutokana na nguvu ya wanasiasa tumejikuta tunapitisha sheria za ajabu.

Sasa tulianzisha hii DSE na CMSA za nini kama hatuko tayari?Lile dude lililoitwa PSRC ndio lilichinja watanzania...ilitakiwa hiyo DSE ianznishwe halafu hayo mashirika ya Nyerere 400 yauziwe huko...kwa mekezaji and sundries...Nadhani mtanzania wa kawaida hana investment opportunities za kutosha ndio maana wote tunarundikana kwenye informal businesses kama Daladala,saluni,groceries etc lakini kama tungekuwa sensitised kuhusu umuhimu wa masoko ya hisa basi uwezo wa kuwekeza upo....sio lazima mtu awe na hisa za mabilioni(hiyo 0.001%)
 
Wangapi wa hao watanzania wa kawaida wamenunua sheaz DSE?

Amandla.....
 
99% hata hawaijui ndio maana nimesisitiza sensitization....hata Dar penyewe over 85% hawajui hii kitu wanasink mitaji yao kwenye outfits zilizo in high risk on returns kama taxi,bajaj,daladala.....na hiyo DSE yeneyewe in kampuni hazifiki 10 ukilinganisha na ya jirani ziko 100+....kwa nini kwetu iwe ngumu wakati wao wame force SAFARICOM iko kwenye bourse??????
 
Serikali ya Kenya walikuwa wanamiliki asilimia 60 ya kampuni. Kama majority shareholder wakaamua kuuza 25% ya shea zao kwenye soko lao. Hakulazimishwa mtu. Ulikuwa ni uamuzi wa kibiashara. Kama serikali yetu inamiliki majority sheaz katika kampuni yeyote wanauwezo wa kuamua iwe listed kwenye Stock exchange billa kubadilisha sheria. hii sheria ninavyoelewa mimi inataka kulazimisha hata makampuni ambamo serikali haina hata thumuni yawe listed! Hiyo si haki.

Hiyo sensitization unayoizungumzia itakuwa na lengo gani? kuwashawishi watu wawekeze kwenye sheaz? Na soko liki-crash au kampuni ambamo watawekeza zisipofanya vizuri (TOL n.k.), hiyo serikali itawarudishia vijisenti vyao? Hapa hapatakiwi sensitization walla nini. Hata huko kwenye Stock Exchange zilizokomaa si wananchi wengi wana hisa. Huko ni kamali na mnunuaji anatakiwa yeye mwenyewe afanye due diligence anapochagua shea zipi anunue au auze. serikali haina nafasi katika hilo isipokuwa kuhakikisha kuwa hapafanyiki michezo kama insider trading. hii sheria haifai, full stop. Na inaonyeshe jinsi tusivyo na wawakilishi kama bunge limeweza kupitisha upuuzi kama huu!

Amandla....
 
Mkandara nimeyasoma hayo maneno. Nadhani utakubaliana na wachangiaji wengi hapa kwamba FDI na economic fundamentals ndiyo zinazostimulate market developments and listing. Kwahiyo nadhani hata tundiko lako lililopita nalo ni batili. Economic theories hazikubaliani na hili kabisa. Kuna mchangiaji hapo juu kasema wazi, sasa ni km wanaalika investors wasiona capital waje kuiba. Hivi km tunadhani kuna wizi kwenye tax, inamaana tunashindwa kabisa kuweka mechanisms za kulinda hayo. Sometime hawa watu wa TRA wanahakiki statements za makampuni inamaana hawana mechanisms za ku uncover wizi huo? Achilia mbali hilo, hivi nani aliyesema listing itapunguza kuibiwa? Hata nchi zilizoendelea shareholders hawana nguvu km wanavyotaka kutuaminisha wanasiasa ispokuwa Marekani huko ndiyo kuna kazi. Km tunaamini tunaweza kuraise capital internally kuna haja watu wa investment centre kusafiri kila leo kwenda kuita wawekezaji?
Hv serikali inadhani duniani kooote sehem iliyobaki kwa Uwekezaji ni Tanzania pekee. Ukweli nchi yetu ni masikini, na katika eneo ambalo lingeweza kutuinua ni sekta binafsi lkn km tutaendelea na sheria zisizoeleweka itakuwa ni kichekesho. Maana hata hao Watanzania ukiondoa wanasiasa wengi wao hawana uwezo wa kununua share na hata hawafaham shares ni nini! Tufike mahali kwenye masuala ya kitaalam wanasiasa wakae kando. Inawezekana kbs wapo wataalam walijadili hili lkn kutokana na nguvu ya wanasiasa tumejikuta tunapitisha sheria za ajabu.
Mkuu badiko langu ni ktk kuonyesha faida ya FDI ktk uchumi wa nchi husika na mara zote tumeona mchango wazi wa FDI ktk GDP ya nchi hizo. Pili zipo sheria za usajili ambazo zinamfunga mwekezaji ktk shares hivyo tywe makini na lugha hii ya kulazimisha kwani kila nchi inapokea wawekezaji toka nje with only 10% ya voting power. Na hata vigogo wa inward foreign investment kama Marekani wanahesabu mchango wa aya mashirika ktk ukuaji wa stock market. China vile vile,zote hizi zinakaribisha wawekezaji kwa mfumo uliokuwa wazi na wenye manufaa kwa nchi zao ktk soko la dunia. Tatizo la Tanzania na mashirika haya sii ukusanyaji wa kodi, hasha na wala sii kweli GDP haipandi kutokana na kodi zinazokusanywa. Hivi vitu haviuhusiani kabisa isipokuwa kuna kipengele hapa cha Ukuaji wa uchumi yaani GDP, stock market na maendeleo ya nchi yenyewe.

Mara zote nchi kama Marekani, UK, China na hata India wamejivunia FDI kwa uwekezaji wao ktk kufungua viwanda vya uzalishaji. Ikiwa ni Nokia basi kuna uzalishaji wa simu au parts za simu, iwe kitu chochote kile kuna uzalishaji wa aina fulani ambao nchi hiyo ita export au kuuza nchini lakini hapa kwetu wawekezaji wengi wamekuja sokoni kuuza mali zao.. Tanzania is a distribution centre ya mali zao na wananchi wake ni wanunuzi...lugha ni ile ile - IMPORTS, IMPORTS wakati hatu export kitu iwe mali au service kwa sababu hatuzalishi wala hatujulikani smasoko mengine..
Hivyo ili nasi tufaidike na soko letu hamzalishi kitu hapa, na maadam Tanzania ni sokoni basi itakuwa vizuri kuiweka mali yenu sokoni..Sheria hii ni sawa na Mkulima au mlanguzi kulazimika kuuza mazao yake soko la Karoiakoo, Tandale au Manzese ili mradi kurahisisha ufuatiliaji wa mapato, kodi na maswala mengine mengi yanayohusiana na taratibu za kuwa na soko.

Tatizo nililoliona mimi hasa kwa nchi yetu Tanzania tuna wawekezaji nchini waliokuja kuchota tu, iwe fedha au maliasili zetu. Hatuna faida ya kuwepo kwa Barricks nchini zaidi ya ajira. Hatuna faida ya mashirika ya simu zaidi ya Tanzania kuwa ndio soko la kuuzia mali zao, hivyo hata sokoni kuna utaratibu wake. Pili, ni muhimu sana wananchi wafahamu umuhimu wa stock market badala ya kufikiria tu kwamba stock zikishuka itakuwaje!..Na stock Market hazinunuliwi na Wananchi tu ila soko lake lipo wazi dunia nzima. Mtu aliyeko Marekani, China au Arabuni anaweza kununua shares ktk mashirika ya simu yaliyopo sokoni DSE, na sii kweli wala haki kusema kwamba lengo ni kumwezesha mwananchi asokuwa na uwezo kununua shares.
Maadam Tanzania tumeingia ktk Utandawazi na nchi za dunia nzima wanaweka mali zao sokoni iweje sisi tuwe wazito kuweka mali zilizowekezwa nchini ktk soko la dunia..Ni kwa kupitia DSE ndipo mali zetu zinaonekana ktk soko la dunia na kumwezesha Mkandara hapa niweze kununua shares nikiwa Ulaya kwa sababu naelewa biashara ya simu Tanzania ni - USHINDI mtupu lakini siwezi kununua shares isipokuwa kwa viongozi wa serikali na baadhi vigogo..

Wakuu zangu, Mzee Machunde namfahamu fika, ni mtu wa home ambaye kasoma na makini sana ktk maswala ya Uchumi lakini dunia alosoma yeye sio tena dunia hii ya Utandawazi ambapo kila shirika linavyokuwa wazi ktk stocks ndivyo linavyoweza kuboreka zaidi na kuiletea nchi mafanikio. Sasa hivi ni mashindano makubwa ya mashirika yote duniani kuonyesha Ubora wa investment yao, kuwavuta wanunuzi wa shares na hata thamani ya shirika kupanda kunatokana na sifa ya mauzo ktk soko huru..Ndio maana kila unapofungua Tv au internet stock market za kila soko ndio kichwa cha habari...Hii ndio maana halisi ya kuanzishwa kwa Utandawazi na soko huria na sii biashara ya gengeni tena.
 
Mkandara hapo kwenye red, ni kweli stock markets zina maana kama ulivyosema na kwa utandawazi huu mtu anaweza kutrade hata online. Lakini sasa kinachotakiwa kufika huko si kulazimisha watu walist. Na pia sheria hii nadhani inawazungumzia Watanzania hailengi kwa watu wa nje. Lingine swali dogo tu la kujiuliza. Hivi kama kampuni haina mahitaji ya mtaji kwa wakati huo sasa watalist nini au wanataka watu wadilute ownership kwenye makampuni? Ukweli culture ya ownership inatofautiana saana kati ya nchi na nchi. Kuna nchi nyingine kampuni zinakuwa owned na family kwa kiasi kikubwa km Ujerumani ingawa trend inabadilika kwa sasa. Nadhani kulazimisha kulist hakuna tofauti na nationalisation ya bw Hugo kule Venezuela ingawa hii wanajifanya kuwapa wananchi hata wasiofaham stock market inafanyaje? Maana hata wale wanaofaham wengi wao hawafuatilii trend ya share na hata hawajui mazingira gani yanaweza kuporomosha thamani ya shares.
Pia bwana Mkandara suala la kuzalisha ni lingine na kuuza ni lingine. Maana unalinganisha role ya Vodafone na Nokia kwa mfano huo. Kikubwa tuandae mazingira.
 
Mkuu badiko langu ni ktk kuonyesha faida ya FDI ktk uchumi wa nchi husika na mara zote tumeona mchango wazi wa FDI ktk GDP ya nchi hizo. Pili zipo sheria za usajili ambazo zinamfunga mwekezaji ktk shares hivyo tywe makini na lugha hii ya kulazimisha kwani kila nchi inapokea wawekezaji toka nje with only 10% ya voting power. Na hata vigogo wa inward foreign investment kama Marekani wanahesabu mchango wa aya mashirika ktk ukuaji wa stock market. China vile vile,zote hizi zinakaribisha wawekezaji kwa mfumo uliokuwa wazi na wenye manufaa kwa nchi zao ktk soko la dunia. Tatizo la Tanzania na mashirika haya sii ukusanyaji wa kodi, hasha na wala sii kweli GDP haipandi kutokana na kodi zinazokusanywa. Hivi vitu haviuhusiani kabisa isipokuwa kuna kipengele hapa cha Ukuaji wa uchumi yaani GDP, stock market na maendeleo ya nchi yenyewe.

Mara zote nchi kama Marekani, UK, China na hata India wamejivunia FDI kwa uwekezaji wao ktk kufungua viwanda vya uzalishaji. Ikiwa ni Nokia basi kuna uzalishaji wa simu au parts za simu, iwe kitu chochote kile kuna uzalishaji wa aina fulani ambao nchi hiyo ita export au kuuza nchini lakini hapa kwetu wawekezaji wengi wamekuja sokoni kuuza mali zao.. Tanzania is a distribution centre ya mali zao na wananchi wake ni wanunuzi...lugha ni ile ile - IMPORTS, IMPORTS wakati hatu export kitu iwe mali au service kwa sababu hatuzalishi wala hatujulikani smasoko mengine..
Hivyo ili nasi tufaidike na soko letu hamzalishi kitu hapa, na maadam Tanzania ni sokoni basi itakuwa vizuri kuiweka mali yenu sokoni..Sheria hii ni sawa na Mkulima au mlanguzi kulazimika kuuza mazao yake soko la Karoiakoo, Tandale au Manzese ili mradi kurahisisha ufuatiliaji wa mapato, kodi na maswala mengine mengi yanayohusiana na taratibu za kuwa na soko.

Tatizo nililoliona mimi hasa kwa nchi yetu Tanzania tuna wawekezaji nchini waliokuja kuchota tu, iwe fedha au maliasili zetu. Hatuna faida ya kuwepo kwa Barricks nchini zaidi ya ajira. Hatuna faida ya mashirika ya simu zaidi ya Tanzania kuwa ndio soko la kuuzia mali zao, hivyo hata sokoni kuna utaratibu wake. Pili, ni muhimu sana wananchi wafahamu umuhimu wa stock market badala ya kufikiria tu kwamba stock zikishuka itakuwaje!..Na stock Market hazinunuliwi na Wananchi tu ila soko lake lipo wazi dunia nzima. Mtu aliyeko Marekani, China au Arabuni anaweza kununua shares ktk mashirika ya simu yaliyopo sokoni DSE, na sii kweli wala haki kusema kwamba lengo ni kumwezesha mwananchi asokuwa na uwezo kununua shares.
Maadam Tanzania tumeingia ktk Utandawazi na nchi za dunia nzima wanaweka mali zao sokoni iweje sisi tuwe wazito kuweka mali zilizowekezwa nchini ktk soko la dunia..Ni kwa kupitia DSE ndipo mali zetu zinaonekana ktk soko la dunia na kumwezesha Mkandara hapa niweze kununua shares nikiwa Ulaya kwa sababu naelewa biashara ya simu Tanzania ni - USHINDI mtupu lakini siwezi kununua shares isipokuwa kwa viongozi wa serikali na baadhi vigogo..

Wakuu zangu, Mzee Machunde namfahamu fika, ni mtu wa home ambaye kasoma na makini sana ktk maswala ya Uchumi lakini dunia alosoma yeye sio tena dunia hii ya Utandawazi ambapo kila shirika linavyokuwa wazi ktk stocks ndivyo linavyoweza kuboreka zaidi na kuiletea nchi mafanikio. Sasa hivi ni mashindano makubwa ya mashirika yote duniani kuonyesha Ubora wa investment yao, kuwavuta wanunuzi wa shares na hata thamani ya shirika kupanda kunatokana na sifa ya mauzo ktk soko huru..Ndio maana kila unapofungua Tv au internet stock market za kila soko ndio kichwa cha habari...Hii ndio maana halisi ya kuanzishwa kwa Utandawazi na soko huria na sii biashara ya gengeni tena.

Ahsante sana Mkuu Mkandara kwa mchango wako mzuri sana, nakubaliana na yote uliyoyaandika.
 
Bnhai,
Mkuu nachozungumza mimi na nadhani lengo la sheria hii sii kila private company inalazimishwa kuingia soko la DSE isipokuwa hao wageni kuweka mali yao sokoni ktk mazingira ambayo yametaarishwa kwa ajili hiyo..Sidhani kama serikali italazimisha mtu yeyote as they feel so! - hapana ila maadam kuna soko la Kariakoo hilo DSE hayo mazao ya nje kama simu yanapokuja kuwekeza yanatakiwa yauze mali zao sokoni na sio magengeni. Mkuu navyofahamu mimi na elimu yangu ndogo ktk Uchumi, lengo la Ku attract wageni ni kuinua soko letu la DSE ambapo wawekezaji wengi kama sii wote hutazama ktk Internet, TV, magazeti na vyombo vya kiuchumi kuwekeza au kununua mali na ndipo kipimo cha Tsh yetu kinapoweza kuwa strong au weaken..Tsh yetu inapopata nguvu, ndivyo pia foreign investors wanakuwa attracted kuwekeza kibiashara hivyo kesho thamani ya Tsh ikishuka watatukimbia wote hata kama tumeondoa barriers zote zinazowabana wawekezaji. Hoja yangu kubwa kimsingi ni kwamba kwa kila deregulation inayofanyika ktk nchi zetu lengo ni ku attract investors ktk mfumo wa foreign exchange investment -ambapo DSE inacheza karata kubwa as a plus for the country's capital account.

Kiuchumi hatuwahitaji foreign investors kwa sababu tuna shida ya huduma ya simu. Hii ndio fikra ya watu wengi sana ambao wanafikiria Umaskini wetu kwanza badala ya biashara. Sisi hatuwahitaji foreign investors kwa sababu tuna shida au kuondokana na ukame alowacha Nyerere na Ujamaa (Umaskini), hivyo waje hapa kuchuma tu maadam tunapata vitu vya nje au waingie hapa kama NGO kutusaidia Yatima na vilema wa Ujamaa...Hapana, mkuu this is Business...Waje hapa tufanye biashara nao na sii wafikirie sisi tuna shida saaana ya simu na huduma zingine ndio sababu yetu kuwaalika wawekezaji nchini. Haya yatakuwa makosa makubwa sana kufikiria kimaskini hata kama tuna shida kiasi gani.

Kwa kila deregulations tunazozifanya nchini lengo ni kuwavutia wawekezaji wa nje waingie ktk soko letu kibiashara na sio msaada au kutupa huduma kwa sababu tuna shida.. Tutakuwa tumekubali na kupoteza maana kamili ya Utandawazi na soko huria kwa sababu ya Umaskini wetu. Itakuwa tumefungua milango ya biashara kwa sababu sisi ni maskini tunahitaji Kusaidiwa..

Mkuu mimi sipendi wala siamini ktk extreme economic liberalization ambayo ni sawa na Neoliberalism. The ultimate transfer na control ya uchumi wa nchi kutoka public ama government kwenda Private sectors ni muhimu sana utazamwe kwa umakini kwa kuzingatia mfumo mzima wa Utandawazi na soko huria. Laa sivyo tutaachwa nyuma tukifikiria kwamba issue ilikuwa kuondoa uchumi mikononi mwa serikali na kuwapa nafasi watu binafsi basi imetoka hawa foreigners waje kama watakavyo, wakati moja ya vivutio vya wawekezaji ni kuwepo kwa hilo soko.

Nadhani mkuu wangu umenipata nakotoka...
 
BNHAI
haya mashirika yapo kwenye service sector na sio manufacturing kama viwanda vya saruji.
ingekuwa ni kiwanda cha simu ningesema serikali inafanya kitu sio sahii, lakini hii service sector wawekezaji watakuja tuu.
ni muhimu sana kwa serikali kuhakikisha haya mashirika ya simu yana list TZ ili kupunguza capital flight.

kila industry lazima iwe treated differently kutokana na mazingira ya nchi, kwa mfano walmart walitaka kwenda kufungua supermarket india serikali ya india ikakataa kwa sababu kubwa kuwa wahindi bado hawana supermarket na hawatoweza kucompete na walmart. watu wengi india wanafanya biashara ya maduka na maduka yao ni madogo, kwa hiyo walmart ikiingia itafanya maduka madogo kufilisika na kusababisha social unrest. uamuzi huu wa india haujazuia FDI hata kidogo
 
Bnhai,
Mkuu nachozungumza mimi na nadhani lengo la sheria hii sii kila private company inalazimishwa kuingia soko la DSE isipokuwa hao wageni kuweka mali yao sokoni ktk mazingira ambayo yametaarishwa kwa ajili hiyo..Sidhani kama serikali italazimisha mtu yeyote as they feel so! - hapana ila maadam kuna soko la Kariakoo hilo DSE hayo mazao ya nje kama simu yanapokuja kuwekeza yanatakiwa yauze mali zao sokoni na sio magengeni. Mkuu navyofahamu mimi na elimu yangu ndogo ktk Uchumi, lengo la Ku attract wageni ni kuinua soko letu la DSE ambapo wawekezaji wengi kama sii wote hutazama ktk Internet, TV, magazeti na vyombo vya kiuchumi kuwekeza au kununua mali na ndipo kipimo cha Tsh yetu kinapoweza kuwa strong au weaken..Tsh yetu inapopata nguvu, ndivyo pia foreign investors wanakuwa attracted kuwekeza kibiashara hivyo kesho thamani ya Tsh ikishuka watatukimbia wote hata kama tumeondoa barriers zote zinazowabana wawekezaji. Hoja yangu kubwa kimsingi ni kwamba kwa kila deregulation inayofanyika ktk nchi zetu lengo ni ku attract investors ktk mfumo wa foreign exchange investment -ambapo DSE inacheza karata kubwa as a plus for the country’s capital account.
Kiuchumi hatuwahitaji foreign investors kwa sababu tuna shida ya huduma ya simu. Hii ndio fikra ya watu wengi sana ambao wanafikiria Umaskini wetu kwanza badala ya biashara. Sisi hatuwahitaji foreign investors kwa sababu tuna shida au kuondokana na ukame alowacha Nyerere na Ujamaa (Umaskini), hivyo waje hapa kuchuma tu maadam tunapata vitu vya nje au waingie hapa kama NGO kutusaidia Yatima na vilema wa Ujamaa...Hapana, mkuu this is Business...Waje hapa tufanye biashara nao na sii wafikirie sisi tuna shida saaana ya simu na huduma zingine ndio sababu yetu kuwaalika wawekezaji nchini. Haya yatakuwa makosa makubwa sana kufikiria kimaskini hata kama tuna shida kiasi gani.

Kwa kila deregulations tunazozifanya nchini lengo ni kuwavutia wawekezaji wa nje waingie ktk soko letu kibiashara na sio msaada au kutupa huduma kwa sababu tuna shida.. Tutakuwa tumekubali na kupoteza maana kamili ya Utandawazi na soko huria kwa sababu ya Umaskini wetu. Itakuwa tumefungua milango ya biashara kwa sababu sisi ni maskini tunahitaji Kusaidiwa..

Mkuu mimi sipendi wala siamini ktk extreme economic liberalization ambayo ni sawa na Neoliberalism. The ultimate transfer na control ya uchumi wa nchi kutoka public ama government kwenda Private sectors ni muhimu sana utazamwe kwa umakini kwa kuzingatia mfumo mzima wa Utandawazi na soko huria. Laa sivyo tutaachwa nyuma tukifikiria kwamba issue ilikuwa kuondoa uchumi mikononi mwa serikali na kuwapa nafasi watu binafsi basi imetoka hawa foreigners waje kama watakavyo, wakati moja ya vivutio vya wawekezaji ni kuwepo kwa hilo soko.

Nadhani mkuu wangu umenipata nakotoka...
Mkuu Mkandara kwa mara nyingine naomba nitofautiane na wewe. Ukweli mengi uliyoyaeleza yanatofatiana saana na kanuni za kiuchumi. Kulazimisha investors kulist katika soko ni moja ya kucreate mispricing ya shares. Imagine investors wanakuforced kulist shares zao what do you expect. Inamaana kuna element ya restrictions whether directly or indirectly ambayo inakuwa priced kwenye shares maana listing yenyewe sio voluntary. Lingine pia ni kwamba unacreate classes ya shares. Very likely kwamba ile cap ambayo kampuni yenyewe itaweka inaweza kuwa overpriced relative to the percentage owned by the founder/owners prior to IPO's (listing) decisions.
Sasa nikija kwenye hizo rangi nilizoweka. Umezungumzia kuimarika kwa Tshs. Ukweli ni kwamba thamani ya pesa yetu haiwezi kujengwa na kulist shares. Zipo issues za fiscal na monetary policy ambazo serikali inatakiwa iziaddress kabla ya kuwaza kulazimisha watu hawa kulist. Mf inflation ni issue kubwa saana katika nchi yetu na impact yake tunaona kwenye interest rates ambayo borrowers wanachajiwa na bank. Vivyo hivyo, unamwambia mtu akalist kwenye pesa ambayo Mf 2008 exchange rates ilikuwa 2100 leo inakaribia 2400, unamueleza nini. Kumbuka pia kampuni hizi zilizowekeza nchini si pesa ya mfukoni kwa wamiliki nyingi ni borrowings, how will then service their borrowings. What signals are we sending to potential investors? Kwahiyo issue kubwa ni kujitazama tunaenda wapi. Nadhani ni bora serikali ingeandaa mazingira ya kuwawezesha Watanzania waweze kuchanga capital na kuwa na viwanda vya kati ambavyo vitawezesha kutengeneza basic items ambazo demand yake ni kubwa nchini na raw materials tunazizalisha wenyewe kuliko kuendelea kuagiza hata vitu tunavyoviweza. NICOL walitaka kuliweza hili lakini kwa bahati mbaya nadhani regulators hawakuwa makini katika kumonitor all the steps of the company.
Mkandara unasema hatuwahitaji investors kwa vile tunashida ya huduma. Mie naona apart from business, there are issues of employment (thus tax etc.), communication and the likes ambazo zinatusaidia kumove. Kwahiyo business ni pamoja na maendeleo at a micro level yaani individuals. Ukweli hatuna mtaji bali tumejaa maneno mengi tena basi wengine hudiriki hata kuingiza siasa pale ambapo hitajio ni professionalism. Mf Russia stock market is one of the volatile stock market in the world, however recent years the government has lifted alot of restriction to allow participation thus boosting investors confidence. Na hii ndiyo modernisation inayofanyika kwa nchi kama Cuba ingawa kwa kasi ndogo saana.

Hii siyo deregulation km ulivyiita. Hii tunarudi nyuma. We need to move forward sisi bado ni masikini angalia turnover ya DSE na umri wake sasa hivi. Hakuna hata wanunuzi wa hizo share. Tuandae mfumo imara wa uchumi na tunawezeshe wananchi ndipo tufikirie soko la hisa. Kuna wakati naamini tulikimbilia mno kutengeza hili soko, lingetokea naturaly nadhani lingekuwa mbali kuliko sasa hivi linavyosuasua.
 
BNHAI
haya mashirika yapo kwenye service sector na sio manufacturing kama viwanda vya saruji.
ingekuwa ni kiwanda cha simu ningesema serikali inafanya kitu sio sahii, lakini hii service sector wawekezaji watakuja tuu.
ni muhimu sana kwa serikali kuhakikisha haya mashirika ya simu yana list TZ ili kupunguza capital flight.

kila industry lazima iwe treated differently kutokana na mazingira ya nchi, kwa mfano walmart walitaka kwenda kufungua supermarket india serikali ya india ikakataa kwa sababu kubwa kuwa wahindi bado hawana supermarket na hawatoweza kucompete na walmart. watu wengi india wanafanya biashara ya maduka na maduka yao ni madogo, kwa hiyo walmart ikiingia itafanya maduka madogo kufilisika na kusababisha social unrest. uamuzi huu wa india haujazuia FDI hata kidogo
Semilong, ni kweli india wamekuwa na sheria juu ya foreign investment. Lakini nachofaham ni kwamba Walmart wapo India ispokuwa hawaruhusiwi kufanya retail business, wanafanya wholeselling na wamepartner na one of the giant store overthere.
Pia India ni tofauti saana na Tanzania ingawa yapo maeneo ya watu masikini saana lkn angalau wao wanaviwanda, teknolojia nk. Labda tungeanzisha investment hizo kwanza kabla ya kung'ang'ania listing. Pia mbona tulikuwa na tunayo TTCL, performance yake ikoje hadi leo wamekuja wawekezaji tunapiga kelele ya capital flights. TTCL ingekuwa competitive leo tusingefika hapa tulipo. Kimsingi tunawaona foreign investors kama wezi lakini upande mwingine tunawahitaji.
 
bnhai,
Kwanza unapotumia neno kulazimisha ni muhimu ufahamu umuhimu wa regulations ktk Biashara. Unachojaribu kusema ndio hayo ya kuingia Ubepari tukifikri hakuna miiko na maadili. Unaweza kusema hata kuingia Ubepari tulilazimishwa, hali ni mazingira yanayolazimisha sisi kuchukua hatua kama hizi.

Ebu nambie wewe unaelewa vipi Soko huria na Utandawazi..Pili, huko Uznuguni kwa nini kuanguka kwa stock exchange huathiri uchumi wa nchi hiyo na duniani kote masoko yao huteteleka..Kunaconnectiongani kati ya stock market na uchumi wanchi zao..Kama wao wamefika huko kiuchumi kwa nini sisi bado tupo ktk Biashara ya magengeni hali tunadai kuingia ktk mfumo wao?.

Zipo risk factors ambazo zinaweza kuwasumbua wawekezaji ktk Mazingira inapohusiana na policies za kibishara kama kodi, quality ya miundombinu, ukosefu wa Talent na skilled labor na mengineyo kuliko soko ni gani wanatakiwa kuuza mali zao.

Kisha mkuu wangu, walioambiwa kujiunga na DSE ni Mashirika ya simu, sijaona mahala serikali ikidai all Private companies at certain level should list with DSE....Na laukama hofu yenu sii wageni, mimi sioni kwa nini mnaweka hofu juu ya kuja kwa Wawekezaji ikiwa mashirika ya simu yamelazimishwa kuingia DSE..Na mbona wananchi wamelazimishwa kusajili namba zao za simu tena kwa sheria na hata faini kupangwa kwa wasiosajili lakini wao wapete kama wanavyopenda kwa sababu tuna shida ya simu...

Kisha mashirika yote ya simu ni mashirika ya nje yanakuja nchini na kuform kampuni as a subsidiary. Hao viongozi wetu wanapewa kishare kidogo pengine hata asilimia 10 tu. Mashirika mengine yanaingia kama Frenchise kama hizo McDonald ambazo huko kwao zipo sokoni lakini sii kwetu, Na nyingine zinaingia nchini kwa Ushirika (Associate) lakini ukweli ni kwamba wote hawa financial statements zinakuwa consolidated na hayo mashirika mama. Sisi hapa tunabakia na huo ushuru, kodi za pango na vitu vidogo sana hakuna mzunguko wowote wa fedha yao ndani kwetu kwa sababu kila kitu chao kinaletwa toka nje. Tena basi kila baada ya miaka mengine yanabadilisha majina kuepa kodi hali ambayo huikuti Ulaya.

Mkuu wangu, in the midst of this global economic uncertainty - Kila nchi itatazama WATU na MAZINGIRA yake ktk kujenga mikakati inayowawezesha kukuza uchumi wao. Sasa hivi nchi za Ulaya wanajadili kutoza Bank zote kodi (Tax) kama limbikizo la fedha pindi zikianguka kiuchumi zipate kunasuliwa kwa fedha yao..Lakini nani atakaye umia hapo - Mwananchi. Ukweli ni kwamba Banks zitapandisha gharama za huduma zake kufikidia kodi hizo. Hapa nyumbani hatuna sababu ya kuiga ila kuweka taratibu zinazotuwezesha kushindana ktk soko huria.
 
Yaani tunafanya mambo ki-Soviet Soviet, na totalitarian commands kwenye stock exchange ya dunia ya leo?

One step forward, two steps back.

Sasa hivi utasikia wanatuandika on the same breath na Mugabe, Chavez na Morales.

Kwa Mugabe kumetulia na Zimbabwer inasonga mbele. Hata China walisemwa sana, lakini leo hawana la kusema.
Makampuni yapatayo faida kubwa hapa kwetu, sioni kwa nini yasiorodheshwe DSE.
 
Katika nchi yoyote,sekta ya mawasiliano ni big fish!!!Ni sector ambayo inaingish apesa nyingi sana.Hata yule billionare wa Mexico,yuko kwenye simu!
Kabla sijapost hii mada,nimeenda kwenye DSE website,hakuna hata kampuni moja ya simu ambayo iko registered!Hata TTCL ya umma???????

Kuna watu wanatuibia sana hapa,pia wanajificha!Kuna tetesi,which ni za kweli kapmuni hizi za simu ni za vigogo wa CCM,mafisadi wakuu.
Mpaka hapo nchi yetu tunapokuwa open na kupata viongozi wanaojali maendeleo ya mwanachi wa Tanzania,hatutafika mbali.
Eti 15 companies ndio tu registered kwenye nchi kubwa kama yetu?kati ya hizo 2 za Wakenya na moja Swissport!What a joke??????
 
Sasa, utaratibu wa kutunga sheria za kulazimishana kuingia DSE utaishia wapi? Au siku ikifika tutamlazimisha pia wakina Bakhresa, Mengi, Manji, Barick, Tanzaniaone etc??

Tunapenda sana njia za mkato badala ya kutumia njia ndefu ya kuelimisha Wananchi.
Nadhani SS Phares unakosea mie kwa hili niko pamoja na kikwete irrespective of the environment ya Tanzania I believe mobile phone companies should be listed to Stock market. Likewise for the other large industrial companies like Barrick. Kwanza hizi kampuni haziko wawazi ni kiasi gani wanapata katika makampuni yao. Wanaficha ficha mapato yao kukimbia kodi na pamoja kuendelea kutumia exemption zinazotolewa na Taifa. Sasa kuna faida gani ya kuwa na hizo kampuni nchini.

Wewe soames unajua hakuna mtu anayependa kulipa kodi but unajua tunalipa kodi ili serikali ipate mapato iweze kuendesha nchi. Matokeo yake hizi kampuni zinachukua faida na kwenda kuwekeza makwao. Kimsingi hili jambo lina faida zaidi ya hasara tunazoziogopea. Wazungu wanataka ideal investment environment but wazungu hao hao wanataka favorable conditions zitakazowasaidia wao wapate faida zaidi wasichangie hata senti tano tanzania na hilo i am sorry lads i beg to differ.

Niko pamoja na mkuu wa kaya kwa hili
 
Back
Top Bottom