MANDATORY LISTING: Was DSE chair forced out over letter to JK?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
MANDATORY LISTING: Was DSE chair forced out over letter to JK?

By Samuel Kamndaya and Hassan Mghenyi

The chairperson of the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) governing council, Mr Peter Machunde, has resigned over what appears to be pressure over his opposition to the recently enacted Electronic and Postal Communications (EPOC) Act, 2010.The DSE governing council yesterday released a statement confirming that Mr Machunde tendered his resignation before the council’s 58th extraordinary meeting last Friday.

Some DSE governing council insiders told The Citizen later yesterday that the council’s vice-chairperson, Mr Yacoub Kidula, was the acting chairperson.

Mr Machunde found himself in trouble with stockbrokers and other DSE stakeholders after signing a letter said to be from the DSE governing council, which was addressed to President Jakaya Kikwete, and which urged the Head of State not to sign the EPOC Bill into law on the grounds that it would be detrimental to the country’s investment climate.

The Bill had a number of contentious clauses, including the one compelling mobile telephone companies to list at the DSE, and was strongly opposed by the firms.

The Tanzania Stockbrokers Association (TSBA) disowned the letter, saying it had not been consulted. TSBA said the letter neither expressed the official position of the body nor the DSE governing council.

TSBA chairman Leandri Tairo-Urassa said the association had learnt that Mr Machunde neither consulted the DSE management nor the DSE governing council before writing the letter.

He added that TSBA fully supported the law, and said the Mobile Operators Association of Tanzania (Moat) was unhappy because listing would require mobile phone companies to operate transparently by revealing their finances.

The DSE governing council also distances itself from the letter in its statement announced Mr Machunde’s resignation.

“The DSE governing council disassociates itself from both the statement (as quoted in a section of the media) and the contents of the said letter because those are his (Mr Machunde’s) personal views,” the statement said.

It could not be immediately established whether Mr Machunde had been forced out or had resigned of his own volition as his phone was switched off when The Citizen attempted to call him several times yesterday.

The two-page letter signed by Mr Machunde said forcing mobile phone companies to list their shares at the bourse would have a negative impact on the firms, the capital market and buyers of the shares.

“Your Excellency, as much as we want more companies to list on our stock exchange, we are, however, reluctant to support the forced listing of shares by private companies,” Mr Machunde said in the letter, which has been disowned by other DSE functionaries.

The contents of Mr Machunde’s letter largely reflected the views of Moat members. Moat said in its letter to President Kikwete in February that forcing mobile phone companies to list at the DSE was contrary to other laws such as the Companies Act, the Capital Markets and Securities Act, and even the Constitution as regards private ownership of property.

“The mandatory listing requirement will surely discourage potential long-term investors in capital intensive sectors, given that it has already caused existing investors in our sector to seriously re-evaluate their long-term expansion and investment plans,” says the letter, whose copy was seen by The Citizen.

In the same vein, Mr Machunde’s letter, a copy of which was also seen by The Citizen, argued that the decision on whether or not to list a company established by private capital or its timing, should be left to shareholders.

“Mandatory listing thus goes against the grain of free enterprise and could potentially jeopardise rather than support DSE’s growth prospects,” the letter stated in part.

It warned that although the law aimed to increase local ownership and management of the mobile phone companies, this might prove unfeasible because the stock market’s capacity was limited.

“Your Excellency, the reality is that DSE’s absorption capacity is, sadly, still very low given the relatively low savings ratio amongst Tanzanians,” the letter said.

Should the mobile companies be forced to list, there was a danger of the market demand failing to cope with the large companies’ initial public offer as all existing companies would also have to list their shares at the same time, it further argued.

But equally worrisome is the risk of probable difficulty of exit by Tanzanian investors participating in the IPOs, who might find it hard to dispose of their shares after the public share offer due to a shortage of buyers.

“As a matter of fact, we are already experiencing this problem with CRDB and Dar es Salaam Community Bank’s listed shares, which clearly demonstrates the existence of this risk.”

Mr Machunde said investors should be given the freedom to choose when to register with the DSE owing to their capital needs and their own assessment of the market appetite as well as fiscal and other listing attractions.

Mr Machunde did not take part at yesterday’s official opening of the special training on bonds organised by the DSE with financial support from the World Bank.

Instead, it was Mr Kidula who delivered the opening statement at the start of the three-day-course at a Dar es Salaam hotel.
 
I think he did the right decision, coz wajua hawa watu wengine huko IKULU hawa mshauri rais no mambo gana na yana kwenda aje? ni bora awaachie hicho kiti chao na wamweke wanaetaka kumbuluza.

Zengwe kila kona maana mmh
 
Wakuu zangu,
Mimi naweza kabisa kumuunga mkono rais wetu ktk maamuzi haya ikiwa bunge letu limepitisha sheria hiyo.. Kila nchi ina sheria zake inapofikia swala la private companies kuwa na limited shareholders in certain number...
Na kila nchi itachukua mfumo ulio bora kulingana na mazingira yake kibiashara. In third world countries esp. Tanzania, I believe power and economic decision-making should be spread among as many people as opposed to being concentrated into the hands of a few...still its Capitalism in the form of nationalism.
 
Wakuu zangu,
Mimi naweza kabisa kumuunga mkono rais wetu ktk maamuzi haya ikiwa bunge letu limepitisha sheria hiyo.. Kila nchi ina sheria zake inapofikia swala la private companies kuwa na limited shareholders in certain number...
Na kila nchi itachukua mfumo ulio bora kulingana na mazingira yake kibiashara. In third world countries esp. Tanzania, I believe power and economic decision-making should be spread among as many people as opposed to being concentrated into the hands of a few...still its Capitalism in the form of nationalism.
Mkandara kwa hili napingana kabisa na Kikwete na serikali yake. Bado mazingira ya uwekezaji Tanzania hayajafika hapo tunapolazimisha. Ukweli kabisa hatueleweki. Upande mmoja tunaita wawekezaji na upande mwingine tunaweka sheria ngumu ambazo hatuwezi kuzisimamia.

Tukubalie wazi miundombinu yetu ya aina yoyote kuanzia barabara na utawala bora yaani legal institutions bado ni kichekesho. Ukiachilia mbali hilo, hitajio la Taifa kwa sekta binafsi ni kubwa saana kuliko wakato wowote. Sasa km tunarudi kwa sheria ambazo ni kandamizi kwa sekta binafsi. Sidhani km tunaendelea mbele.

Pia sheria hii ni tofauti na kanuni nyingi za kiuchumi. Nadhani km tungeandaa mazingira bora kuanzia kanuni za soko la hisa nk, wawekezaji wenyewe wangeweza kuissue shares voluntary kwani kwa hali yyt mahitajio ya mtaji na makubwa saana na opportunies kwenye sekta ya mawasiliano bado ni kubwa saana.

Kwa maana hiyo, Tanzania haikupaswa kufuata taratibu lazimishi za kulist shares ktk stock markets. Km kulikuwa na haja ya kufanya hivyo kwanini serikali imeendelea kuuza Taasisi/mashirika yake na isihamishie ownership kwa wananchi??
 
Yaani tunafanya mambo ki-Soviet Soviet, na totalitarian commands kwenye stock exchange ya dunia ya leo?

One step forward, two steps back.

Sasa hivi utasikia wanatuandika on the same breath na Mugabe, Chavez na Morales.
 
Wakuu zangu,
Mimi naweza kabisa kumuunga mkono rais wetu ktk maamuzi haya ikiwa bunge letu limepitisha sheria hiyo.. Kila nchi ina sheria zake inapofikia swala la private companies kuwa na limited shareholders in certain number...
Na kila nchi itachukua mfumo ulio bora kulingana na mazingira yake kibiashara. In third world countries esp. Tanzania, I believe power and economic decision-making should be spread among as many people as opposed to being concentrated into the hands of a few...still its Capitalism in the form of nationalism.

Mkandara hapa tuko pamoja. Mimi si mfagiliaji wa Kikwete lakini hapa alifanya uamuzi wa busara kabisa. Sheria zetu zinazotungwa na Bunge ni lazima ziheshimiwe na hawa Wawekezaji kama hawako tayari kuziheshimu basi waende zao. Nchi za magharibi wanaona ujiko kuweka shares zao katika masoko ya hisa za nchi za magharibi lakini kwetu wanakataa kata kata, basi ni lazima walazimishwe tu kama hawakupenda wafungashe.
 
Mkandara kwa hili napingana kabisa na Kikwete na serikali yake. Bado mazingira ya uwekezaji Tanzania hayajafika hapo tunapolazimisha. Ukweli kabisa hatueleweki. Upande mmoja tunaita wawekezaji na upande mwingine tunaweka sheria ngumu ambazo hatuwezi kuzisimamia.

Tukubalie wazi miundombinu yetu ya aina yoyote kuanzia barabara na utawala bora yaani legal institutions bado ni kichekesho. Ukiachilia mbali hilo, hitajio la Taifa kwa sekta binafsi ni kubwa saana kuliko wakato wowote. Sasa km tunarudi kwa sheria ambazo ni kandamizi kwa sekta binafsi. Sidhani km tunaendelea mbele.

Pia sheria hii ni tofauti na kanuni nyingi za kiuchumi. Nadhani km tungeandaa mazingira bora kuanzia kanuni za soko la hisa nk, wawekezaji wenyewe wangeweza kuissue shares voluntary kwani kwa hali yyt mahitajio ya mtaji na makubwa saana na opportunies kwenye sekta ya mawasiliano bado ni kubwa saana.

Kwa maana hiyo, Tanzania haikupaswa kufuata taratibu lazimishi za kulist shares ktk stock markets. Km kulikuwa na haja ya kufanya hivyo kwanini serikali imeendelea kuuza Taasisi/mashirika yake na isihamishie ownership kwa wananchi??

Nadhani hakuna point hapo.kwani miundombinu (barabara sheria, utawala bora) wanazotumia wawekezaji wa sasa na inayowapa faida wenyeji wakinunua hisa zitabadilika? ni ubwenyenye tu ndo unaoonyesha.
 
Kuna baadhi yetu tunadhihaki uwezo na mwamko wa waTanzania pamoja na majirani zake kuwekeza katika masoko ya hisa na mitaji. Kwa kila TOL kuna TBL, NBC na Twiga. Pia na mchakato wa kuruhusu mitaji kuhama katika jumuiya ya Afrika Mashariki, makampuni haya yatapata tu fedha yanazozitaka. Tusije sahau kwamba IPO ya Safaricom ilikuwa oversubscribed by a country mile na kwa baadhi ya mitandao ya hapa kwetu ndani hili pia laweza tokea.

Restrictions kama hizi mbona zimetapakaa sana katika nchi nyingi za Asia? Hakuna mtu anayetwaa kampuni binafsi kimabavu, mabavu yanatumika kuwalazimisha wajiweke sokoni ili wazawa wapate kula au kuliwa na wao. In many ways this is a disguised anti trust directive/legislation
 
Nadhani hakuna point hapo.kwani miundombinu (barabara sheria, utawala bora) wanazotumia wawekezaji wa sasa na inayowapa faida wenyeji wakinunua hisa zitabadilika? ni ubwenyenye tu ndo unaoonyesha.
Sina sababu ya kuonyesha ubwanyenye zaidi ya kujadili kile ninachokiamini. Unajua uwekezaji kwenye nchi kama Tanzania unaambatana na rushwa kwa hali ya juu, na pia ucheleweshwaji wa kesi za kibiashara ni kitu cha kawaida saana. Sasa kuwekeza ktk mazingira haya ambayo kwa hali ya sasa sheria zake zinabadilikabadilika kutegemeana na nani kiongozi inamaanisha higher level of risks. Ingawa returns inaonekana kuwa promising si kila mtu yupo tayari kuwekeza kwenye mazingira tete. Kwahiyo kwa sasa kazi kubwa ingekuwa kuvutia uwekezaji na ukuaji wa sekta binafsi kabla ya kukimbilia kutunga sheria zinazokwamisha uwekezaji.
 
Sasa tunaita wawekazaji kutoka nje wa nini kama mtaji unaweza kupatikana DSE? Essentially sheria hii ina maana watu waje hapa bila kitu, tuwape mitaji, walipane mishahara minono halafu waende zao!
 
Bnhai,
Nitakubakubaliana nawe tu ikiwa hali halisi ya uwekezaji kwetu inafanana sawa na nchi za nagharibi kwa ujumla. Hata wao sheria zilizopo UK hazifanani na zile za Marekani au Ausralia au hata China kwa sababu ya kimazingira. Kwa mfano, chukulia haya mashirika ya simu toka nje yamejiandikisha ktk masoko ya Ulaya lakini sii hapa kwetu yanapofanya kazi. Kifupi yamekuja hapa kuchuma na faida yote inakwenda nje kuwanufaisha wao. Mara nyingi mashirika ya nje yanayowekeza UK au USA utayakuta yakiuza share zao masoko ya ngi husika hata kama share kubwa imeshikiliwa na Mwarabu, mchina au Mzungu... mbali na huduma kuna mahusiano ya kibiashara baina ya mwenyemali na wananchi hasa ktk mashirika makubwa.

Pili, wenzetu wana uwezo mkubwa wa wananchi wao kufungua biashara hizo ndani na nje hali sisi tunachokifanya ni kuita wawekezaji kwa malengo ya upatikanaji wa huduma fulani..hivyo sisi tunabakia kama wateja tu ktkkukuza biashara ya wageni wawekezaji ambao wako nje. Ndio maana tumeshindwa kupata chochote toka barricks kwa sababu sisi ni wahitaji, hivyo chochote tutakacho pewa iwe ruzuku tumshukuru Mungu (size yetu).
Mimi nafikiri lengo haswa la kulazimisha mashirika haya kuingia ktk soko letu ni kuongeza nafasi ya wananchi wetu kukuza mitaji yao, kupata kufaidika kibiashara na uwekezaji huo badala tu ya kutumiwa kama wanunuzi wa mali ya nje. Kifupi misingi yetu ya biashara inatulazimu kubakia wahitaji wa hufduma toka nje na hakuna uwezekano wa wananchi kukuza mitaji yao..Ni kama maskini omba omba wanaotaka wafundishwe nao kuvua samaki badala ya kusubiri kupokea sadaka kila siku.

Sawa, tunaweza sema ni mfumo wa Kisoshalist kulazimisha uwekezaji wowote kwa manufaa ya umma hivyo kuondoa uhuru wa biashara na Utandawazi, lakini pia kwa nchi kama zetu Uhuru huu na Utandawazi unabakia somo tu la Kiuchumi pasipo sisi kuwa na mchango wowote zaidi ya kutumiwa kama wanunuzi wa mali inayotengenezwa Ulaya..Na ndipo wengi tunaposhindwa kufahamu, kwani tunahitaji vitu vya Ulaya lakini hatuna vitu ambavyo wao wanahitaji toka kwetu. Ukitazama nchi zote za Ulaya hata hizo za Nordic wote wanatuuzia kwa mabillioni mali zao lakini wao wakinunua asilimia 10 tu ya mali zetu.. Hakuna mzani wa balance of trade kabisa na kibaya zaidi hata kile ambacho wanatakiwa kukunua toka kwetu tunalazimika kuwaita wao wakizalishe na kisha wajiuzie wao wenyewe..

Kama nilivyosema hapo awali Ubepari ni mfumo unaotazama nchi zenye uwezo wakuzalisha. Unatazama matahjiri wa ndani wanaweza vipi kuongeza mafanikio ya kiuchumi ya wananchi na nchi husika na sii kweli kabisa kwamba Ubepari unatazama pia kuziwezesha nchi na watu maskini kuendelea. Maadam hatuna uwezo wa kivbiashara, ubepari sio wetu... na ndio nikatoa mfano wa maskini ombaomba anayetaka kujiingiza ktk biashara pasipo kuwa na Mtaji, elimu wala uzoefu wa uzalishaji wa biashara hiyo ila kwa kuiga tu. Hawezi kufanikiwa na hawezi kutajirika isipokuwa kwa kujipima uwezo wake kwanza.. Kufahamu aliposimama kimaskininaanaweza kufanya kitu gani..Msaada wowote atakaopata utahusiana na malengo ya kile anachotaka kuanza kukifanya iwe ktk misingi ya Kujinyima na kubana ****** (matumizi) kama Mkomunist na iwe hivyo..

Matajiri wote unaowajua wewe iwe Bakhrea au Mengi wote hawa walianza na maisha ya chini sana. walijinyima kiasi kwamba familia zao ziliwaona kama ni makomunist, wakafuata misingi bora ya kujinyima ktk matumizi yasiyokuwa ya msingi.. wakajali kila senti inayohusiana na biashara zao.. Wakaongeza muda wa kazi na mahusiano (contacts) kwa malengo ya kubadilishana mazao kwa bei halali pasipo dhulma. Muhimu interest zilikuwa mbele ya mahitaji yao binafsi..Hivi ndivyo walivyoweza kufanikiwa kutoka ktk umaskini, haikuwa bahati wala hawakufuata misingi na taratibu za Kibepari toka siku ya kwanza, ila kile kilichowezekana kulingana na mzingira ya biashara yaliyokuwepo. Kikubwa zaidi ni kwamba kufanikiwa kwao hakukuhusiana kabisa na ELIMU ya darasa iwe Uchumi au Ubepari, isipokuwa ubunifu wa biashara na misingi bora ya kulinda na kukuza mali zao ktk mazingira magumu.

Hivyo mkuu wangu hata kufanikiwa kwetu kama nchi kunategemea zaidi Ulinzi wa mali zetu.. uwezo wetu ktk kuingia sokoni na kuuza mali zetu.. Mgeni atakaribishwa tu kuwekeza hapa ikiwa atakuwa mmoja wetu yaani mali yake ni kati ya mali inayowalenga Watanzania na sio kuwafanya Watanzania wahitaji wasiokuwa na haki yoyote. It's all business mkuu wangu, siku hizi Kariakoo ukitaka kununua nyumba hupewi 100% umiliki, Unalazimika kuacha asilimia 35 kwa mwenye kiwanja pamoja na masharti mengine ili mradi nyote mnafaidika na uwekezaji huo..Yale maswala ya kununua jumla kwa mabillioni imeonekana haina faidakwa maskini ambao hawajawahi kushika fedha. Mara zote wazee hawa wamejikuta wakipoteza hayo Mabillioni within short period kwa sababu hawakuwa wabunifu, hawajawahi kuona fedha nyingi kiasi hicho, kupitia hatua za kuzaa Utajiri ama uzoefu wa biashara yoyote kwa mtaji mkubwa.. ni kiwewe tu mkubwa, kiwewe unajua tena maskini akipata.
Hivyo inatudhihirishia kwamba maskini akipata hata fedha kiasi gani hakuna guarantee ya mafanikio...Ni ukweli usiopingika kwamba FEDHA sio msingi wa Maendeleo.. Na wazee sasa hivi wameshtuka na kudai asilimia kwa kila uwekezaji wa jengo Kariakoo. Na hakika wengi wametoka mkuu wangu wanaiona faidi ya kuingia Ubia ktk biashara kuliko kuuza nyumba nzima kwa cash money ambayo hawana nidhamu ya kuiwekeza..

Kama Kariakoo inavyokwenda na mafanikio yanaonekana basi bila shaka hata mfumo huu wa kuwalazimisha wawekezaji toka nje kuingia Ubia (kuuza share) kwa wananchi ktk soko la DSE ni bora zaidi kulingana na mazingira yetu. Kinachowezekana Kariakoo kibiashara, ndicho kinatumika Kitaifa kulingana na mazingira yetu..Alaaah, tutandaze fibre sisi (miundombinu) wao waje kuchuma tu mara wauziane mashirika kila baada ya miaka mitano kukwepa kodi... wakuu zangu hatuwezi tena kuvumilia upuuzi huu. Kwa kila hila wanayoifanya kuepa kutuwezesha ni lazima nasi tuwe na hila suluhisho ya biashara zote za kiujanja ujanja..
 
Hii sheria essentially ina wa patronise Watanzania negatively.

Itafanya dunia iamini kwamba, Tanzanians are not investment savvy, and the DSE particularly, is not a desirable place to do Initial Public Offerings, na ndiyo maana serikali inalazimisha wawekezaji wa-float shares zao DSE.

Badala ya serikali kukazania kuendesha uchumi kwa command system, inatakiwa iweke mazingira mazuri ili wananchi waweze kuwa na disposable income, waweze kujua kuinvest DSE, tuone investors wenyewe wanapigana vikumbo kuja kutoa IPOs hapo DSE.

Tusipende short cuts tu, tufanye kazi kubadili fundamentals za uchumi wetu, kupandisha GDP, disposable income na level of investment. Unaweza kulazimisha wawekezaji wa float shares DSE halafu watu Per Capita income yao ni $ 500, na wanaoinvest DSE hawafiki hata 0.001 ya population. Unachukua cost kubwa katika PR kwa kitu ambacho hakikusaidii lolote.

Ukianza kulazimisha watu kufloat shares zao tu una send red flags, watu wanaanza kujiuliza kesho keshokutwa utataka kutaifisha haya makampuni nini?

Badala ya kuchochea investment sheria hii itadumaza investment, na DSE particularly.
 
Sasa, utaratibu wa kutunga sheria za kulazimishana kuingia DSE utaishia wapi? Au siku ikifika tutamlazimisha pia wakina Bakhresa, Mengi, Manji, Barick, Tanzaniaone etc??

Tunapenda sana njia za mkato badala ya kutumia njia ndefu ya kuelimisha Wananchi.
 
Sasa, utaratibu wa kutunga sheria za kulazimishana kuingia DSE utaishia wapi? Au siku ikifika tutamlazimisha pia wakina Bakhresa, Mengi, Manji, Barick, Tanzaniaone etc??

Tunapenda sana njia za mkato badala ya kutumia njia ndefu ya kuelimisha Wananchi.

Phares,

Mimi nasema watatumia commands zote wanazozijua, lakini kama fundaments za uchumi wa nchi mbovu, uzalishaji hamna, disposable income haipo, watu hawana jinsi ya kuinvest kwa sababu kila mtu anaganga njaa - kuacha hiyo talented 0.001%- tutanunua jina baya kwa bei kubwa tu, hamna la zaidi.
 
Kama kawaida yetu. Kwa kupenda vya kunyonga tunajipiga risasi kwenye mguu! Kwani transparency inapatikana kwenye stock exchange peke yake? Hivi tunaamini hao wawekezaji awana pengine pa kwenda isipokuwa Tanzania peke yake? Tunakimbilia mgao wa faida wakati tunasahau ajira, kodi n.k. ambazo wanalipa hapa nchini. Hao watanzania, ni wangapi wana uwezo wa kununua sheaz katika hilo soko la hisa? Mimi ningedhani kuwa badala ya kukimbilia huku ambako watakaofaidika ni mabwanyenye wachache tungekazania kuimarisha sheria zetu za ajira na mazingira ili kuhakikisha mtanzania au mtu mwingine yeyote atakayeajiriwa nchini mwetu hatadhulumiwa na kufanyishwa kazi katika mazingira ya kitumwa na kuwa mazingira yetu hayataharibiwa na mwekezaji yeyote! Hii sheria ni ya kipuuzi na huyo mwenyekiti anastahili pongezi kwa kukataa kuhusishwa nayo.

Amandla.......
 
Peter amejiuzuru mapema mno unless kama kalazimishwa kutoka ngazi za juu. ile position yake siyo ya kisiasa na ni ya kitaalam zaidi ilipaswa akae na kuzitetea hoja zake ili zieleweke na kukubaliwa. hata hoja ikikataliwa kwa sababu moja au nyingine unapaswa uvumilie..Ustaarabu ni pamoja na kukubali mawazo ya watu wengine.
 
Mkandara I fully support you. The chairperson was either being used by the Mobile Phone Company Operators knowingly or unknowingly to their windfall profits which are untaxed. Let transparency prevail in their accounts and the commonman get a share in their coys.
 
Good for him! Hii sheria haieleweki kabisa!
Kama kuna mtu ana copy ya hii Act aibandike, nimeshindwa kuipata kwenye tovuti ya bunge.

Hauwezi kulazimisha listing, kama hakuna demand kwa shares zao je? Itakuwaje hapo, serikali itaguarantee ununuzi wa hizi shares?
Na point ya hii sheria ni nini hasa? Kama wanataka transparency si wangebadilisha sheria za accounting and reporting, hii mbona roundabout way ya kuleta transparency?

Na kama wana taka wananchi "wafaidike" na hizi kampuni, kununua shares sio guarantee ya kufaidika, kuna kuingia hasara pia.
Na dividends kampuni yenyewe ndo inaamua kama itatoa, sasa mkiwalazimisha kuuza shares mnafikiri hizo dividends mtaambulia?
 
Maneno haya HAPA

Mkandara nimeyasoma hayo maneno. Nadhani utakubaliana na wachangiaji wengi hapa kwamba FDI na economic fundamentals ndiyo zinazostimulate market developments and listing. Kwahiyo nadhani hata tundiko lako lililopita nalo ni batili. Economic theories hazikubaliani na hili kabisa. Kuna mchangiaji hapo juu kasema wazi, sasa ni km wanaalika investors wasiona capital waje kuiba. Hivi km tunadhani kuna wizi kwenye tax, inamaana tunashindwa kabisa kuweka mechanisms za kulinda hayo. Sometime hawa watu wa TRA wanahakiki statements za makampuni inamaana hawana mechanisms za ku uncover wizi huo? Achilia mbali hilo, hivi nani aliyesema listing itapunguza kuibiwa? Hata nchi zilizoendelea shareholders hawana nguvu km wanavyotaka kutuaminisha wanasiasa ispokuwa Marekani huko ndiyo kuna kazi. Km tunaamini tunaweza kuraise capital internally kuna haja watu wa investment centre kusafiri kila leo kwenda kuita wawekezaji?
Hv serikali inadhani duniani kooote sehem iliyobaki kwa Uwekezaji ni Tanzania pekee. Ukweli nchi yetu ni masikini, na katika eneo ambalo lingeweza kutuinua ni sekta binafsi lkn km tutaendelea na sheria zisizoeleweka itakuwa ni kichekesho. Maana hata hao Watanzania ukiondoa wanasiasa wengi wao hawana uwezo wa kununua share na hata hawafaham shares ni nini! Tufike mahali kwenye masuala ya kitaalam wanasiasa wakae kando. Inawezekana kbs wapo wataalam walijadili hili lkn kutokana na nguvu ya wanasiasa tumejikuta tunapitisha sheria za ajabu.
 
Back
Top Bottom