Manchester United (Red Devils) | Special Thread

ETH is cooking, inabidi aweke standards kwa players wake, refer jinsi pep alikuw unexpected kwa decision ya etoo, gaucho, Toure. Surely hakuna mkubwa kukiko ETH pale United kwa sasa.
Me naamin hii timu jamaa anaiweza,sio tusipoelewa mwanzon, ttamwelewa mwishoni.
OGS tulimwelewa mwanzon, mwishon akatuchanganya.
 
Najibu shutuma moja moja

Kuhusu magwaya, mashabiki wa man u 90% na pundits wenu moja kwa moja mnahusika
Mara ngapi hapa the gunners tunamuongelea vizuri magwaya

Nilishawai kusema, timu ya taifaagwaya ni panga pangua. Ila akiwa kwenye club mnamvunjia heshima Sana

Au nitafutie meseji ya mtu wa arsenal hapa jukwaa tulimsema vibaya (kumkosa bila mantiki)

Mashabiki wa man u, sometimes mnazingua Sana. Price tag ya mchezaji bas mnataka output yake ije fasta fasta tu.
Hamuangalia adaption ya player Wala nini

Huu ujinga mnawaambukiza team gunners Kule, kuwatia pressure wachezaji.
mfano Kai mnalazimisha tumuimbe, Kama mnavyomuimba magwaya.
 
OGS alisalitiwa ,yule jamaa hakuwa mzoefu Sana but alikuwa anaileta DNA yenu kwa ufasaha ,

Ukweli alisalitiwa
 
Hii kitu inawafanya player wazidiwe presha ,wakiwa uwanjani hawajiamini kabisa

Fans wanawapelekea Sana Moto

Nakumbuka Saliba alijifunga goli mwaka Jana na ndio amefika tu Arsenal, mashabiki walishangilia na kumtia moyo , kuanzia pale alikuwa na confidence kubwa Sana hata ndan ya box anafanya kwa utulivu bila presha ,

Now days limeibuka kundi linataka mchezaji awe robot , lasivyo atapelekewa Moto had akome
 
Ukweli nadhani ni swala la Antony kuwa trash ila kocha anamlinda.

Kiukweli Antony hakutakiwa awe regular starter mbele ya Sancho. Walitakiwa wafanyiwe rotation ila TH anakomaa na kijana wake, swala ambalo Sancho halikubali.
Sancho anasema Kuna double standard
 
Sancho anasema Kuna double standard
Na hiyo ndiyo imeibua story za Carrington sasa, wote tulijua ni doubles standards kumbe mazoezini anachelewa bado hajitumi atapataje namba sasa?

Sitashangaa kesho kumuona Bruno au Garnacho RW maana EtH usipomu-impress kwenye training ni bench tu. Wengi tunataka Pellistri acheze ila hatujui kwanini EtH hampangi.

Sancho kale kadogo ni kavivu na ubishoo mwingi. Msimu ulipoisha fasta tu akadandia Jet yupo na machupa kibao ya alcohol na soft drinks. Wachezaji wanatakiwa kujua career waliyochagua inahitaji afya nzuri ya mwili na akili, sasa dogo kama Sancho analamba £350k utamuambia nini!

Sancho anatafuta tu Social Media sympathy hakuna kitu apambane na hali yake.
 
Moja ya Walimu Bora sana ku-Grace Game ni JOSE MOURINHO, Kuna wakati Dili la Shaw kufeli Chelsea alilaani sana Mshahara aliokuwa anautaka na akasema ni mwanzo wa kuharibika kwa Mpira, watoto wadogo Mishahara Mikubwa na ndo Shida kubwa sana leo Players wengi wanaenda timu kwa Packages. {Mpira ni Passion ila imebaki kwa Fans tu}

UTD alitaka mchukua Sancho kwa 130m dili likashindikana msimu ulofata akanunuliwa kwa 70's. {Alijipunguzia matatizo} BVB, AJAX, na TIMU Nyingine nyingi zinazocheza Mpira NIDHAMU Huwa kitu namba 1 na hii huwa rahisi wachezaji kutimiza Majukumu.

Nje ya Haaland na Gundo, asee unaweza watafuta Players wengine walokuwa na Career Yenye mafanikio kama Individuals nje ya BVB ukakosa, {Goetze, Sahin, Mikhi, Dembele, Mor, Matt, Auba, Alcaraz, Weigl, Grobkreutz, Kuba, et.al}
Twende Ajax {De light, FDJ, Sanchez, Neres, Ziyech, Donny, Dolberg, Shonne, Blind, et al.}
Hao ni players wamekuwa wa kawaida mbali na uwezo mkubwa wameonyesha katika timu walimokuwa, Sababu kubwa walimu wao waliwajenga katika TIMU.

Kuna Hoja ya De Zerbi na Ange kucheza Mpira Mzuri {kila mtu anatafsiri na Mpira mzuri kwa Mapenzi yake} Hawa Brighton na Spurs wanaanza season na malengo tofauti na UTD, Arsenal, Liver na ndo mana ni rahisi weka falsafa zao kwa haraka maana Pressure ni ndogo. Siku zote timu inajengwa na Muunganiko uliojengwa na Nidhamu inayotokana na Mwalimu Husika. Arteta alitaka timu yenye umoja ila alijua ni ngumu ipata kukiwa na Gap kubwa sana la Salaries Auba, Lacca, Ozil wakapisha Project yake leo timu inacheza kwa Taswira anataka Yeye na Nidhamu iko fresh.
 
Kwa suala la Maguire kukataa kujiunga na Westham na kung'ang'ania kubaki Utd ili aendee kula mshahara mkubwa ambao hauendani na anachodeliver mimi kama shabiki kindakindaki wa Man Utd nasema "Maguire aendelee kupigwa mtungo na mashabiki wa timu zote ili tamaa yake imtokee puani"
Wazungu especially Waingereza hua wana utamaduni wa kujiwajibisha wenyewe pale yanapotokea mapungufu/kasoro katika majukumu yao.
Tumeona mara kibao viongozi mbalimbali katika serikali ya Uingereza wakijiuzulu wenyewe nyadhifa zao kama ishara ya kuonesha kukubali kuwajibika kutokana na makosa.
Maguire tamaa zake binafsi ndio zimemfanya akatae kuwajibika, hivyo mtu wa aina hii hua ni dhambi kumhurumia pale majanga yanapomkuta kutokana na tamaa zake.
 
Rubbish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…