Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Watu waanza kushtuka Ten hag Hana tofauti na Ole

UKWELI MCHUNGU


Dwight Yorke:

“Hakuna mahali pa kuficha. Ole Gunnar Solskjaer alikuwa na rekodi nzuri zaidi ya Ten Hag katika misimu yake miwili kamili akisimamia klabu, watu wanazungumza kuhusu maendeleo ambayo tumefanya na mtindo bora wa soka unaochezwa. United wamefika fainali ya Kombe la FA, wameshinda Kombe la Carabao na kufika mbali kwenye Ligi ya Europa kwa hivyo ni maendeleo, lakini Ten Hag kupoteza mechi nyingi za Premier League kuliko Solskjaer katika misimu ya 2019/20 na 2020/21. Matokeo hayajakuwa mazuri vya kutosha msimu huu, United wanaangalia juu ya bega lao na wanajaribu sana kushikilia nafasi ya nne, sina uhakika hapo ndipo klabu inataka kuwa."

"Huwezi kujificha katika mazingira haya, wachezaji na meneja wanahitaji kuwajibika. Ten Hag anapata sifa timu inapocheza vizuri, inabidi apokee ukosoaji pale anapokosea pia. Jambo la kukatisha tamaa katika uchunguzi wangu katika michezo ya hivi karibuni ni kwamba Manchester United hawajui jinsi ya kushinda, lazima kila wakati uwe na mchezo mzuri wa mpira wa miguu. Mara chache huwa tunashinda 1-0, soka sio kufunga mabao mengi, ni kupata matokeo na kuinua mikono yako katika baadhi ya michezo, kama mchezo wa West Ham"
 
Glazers wajiongeze. Wakibaki next season yatafanyika maandamano makubwa sana.

Labda kama wana plan za kuwapoza mashabiki kwenye usajili.
Grazzer dirisha lililopita si walitoa hela ya usajili €245m Kama sikosei

Mnataka watoe kiasi gani mseme kweli wametoa pesa? Kumbuka Kuna FFP, wage bills , operation cost
 
Grazzer dirisha lililopita si walitoa hela ya usajili €245m Kama sikosei

Mnataka watoe kiasi gani mseme kweli wametoa pesa? Kumbuka Kuna FFP, wage bills , operation cost
1. Wameipa club deni. Kipindi wanainunua United ilikuwa haina deni.

2. Hawajaboresha miumdombinu ya timu tangu wameinunua United.

3. Hawajaboresha uwanja (Old Trafford) na kuweka huduma za kisasa kuendana na kasi ya Teknolojia, ikiwemo upatikanaji wa Internet (Wi-Fi) kwenye uwanja mzima.

4. United ndiyo timu pekee kwenye EPL inayotoa gawio. Katika miaka 7 ni £155m zimetolewa kwenye gawio.

5. United inaendeshwa kwa misingi ya kibiashara zaidi hivyo watu chini ya Glazers hawana nguvu ya maamuzi zaidi ya Glazers wenyewe.

6. United inajiendesha yenyewe, hiyo €245m unayoisemea ilitokana na mapato ya timu. Na Glazers hawajawahi kufanya uwekezaji wowote ktk timu.

7. Tokea 2006 United imetumia £1.1B (kwa report za 2021) kwenye financing.

£724m interest
£185m debt repayments
£149m dividends

Hiyo ni £1.1B ambayo ingeweza kuboresha United ktk miaka yote hiyo. Kwenye miundombinu, wachezaji, makocha, wafanyakazi wazuri na wabobezi ktk soka ila kwasababu ya Glazers pesa yote wameikomba.
 
Grazzer dirisha lililopita si walitoa hela ya usajili €245m Kama sikosei

Mnataka watoe kiasi gani mseme kweli wametoa pesa? Kumbuka Kuna FFP, wage bills , operation cost
Angalia hii chart ya 2016-2020. United ndiyo timu ambayo wamiliki wake walichukua pesa nyingi zaidi kutoka kwenye club. £133m ilitolewa kama gawio. Everton wamiliki wake walitumia £348m kuboresha timu yao.

Kama bado unadhani wanachofanya mashabiki wa United wanakosea kwasababu ya hizo namba kwenye pesa za usajili itakuwa bado hujaliona tatizo.

Misimu yote pesa za usajili zinatokana na mapato ya timu. Uwekezaji mpya maana yake watatoa pesa kuwekeza kwenye timu na kuboresha miumdombinu ya timu.
 
Ni aibu kuwa na wachezaji kama Masho na Sancho first eleven. ETH apambane mapema atoe Sancho amuweke Garnacho mapema sana. Na asirudie makosa ya kumtoa Anthony, kila mechi anamtoa na tunakimbizwa kweli kweli lakini hajifunzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…