Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi sio kocha nimekwambia kubadili wachezaji haikufanyi wewe kuwa kocha bora, sisi tunaongelewa mechi ya juzi ungekuwa wewe kocha ungempanga nani? waliocheza ndio best wako ukiangalia bench hakuna aliyebora kuliko anayecheza na mbaya zaidi alifanya mabadiliko na tukaona team ilikuwa afadhali kuliko baada ya mabadiliko. unaniandikia sababu ya ya kubadili mchezaji kila mtu anajuwa.
  1. Kwa asili kuna wachezaji amabao sio consistence( hupangi mchezaji hujui atakupa nini wanapangwa best 11)
  2. Bahati mbaya siku hiyo mchezaji unayemtegema anaweza akashuka form( ikiwa wote 11 wameshuka utabadili wote)
  3. Kwa bahati mbaya timu pinzani inaweza kumkamia na kumfanya asicheze kabisa nje na matarajio( ndio kazi ya kocha team iinaweza kubadili shape tu wachezaji walewale)
  4. Anaweza mchezaji unayemtegemea akakamia kucheza sana na kuchoka mapema( Uliona lini Messi, Ronaldo, au mchezaji yoyote katolewa sababu ya kuchoka kikosi kinapangwa ukiwa 100% fit labda ungesema siku hiyo hakucheza vizuri lakini wako wachezaji hata asipokuwa vizuri hatolewi sababu hujui utapata ni kwake muda wowote)
  5. .............................??
  6. ...........................??
kocha akipanga kikosi nia yake kikosi kucheza dakika 90 na kama kapata anachotaka anaweza kubadili mfumo kujlinda zaidi au kushambulia zaidi na sub zingine wakati ziko 3 anaacha ikitokea tu kaumia kulazimishwa kubadili mchezaji, mimi nadhani unakariri sana nimekutajia kuna vikosi kama Real ile iliyoshinda UEFA mara 3 walikuwa wanacheza wale wale kila mechi akibadilishwa mtu mmoja tu, Barca ya Gurdiola wale wale liverpool ya mwaka jana walewale sasa usiniambie hapa kigezo kocha bora kufanya sub 5.
 
✓ Man U tutaendelea kusajili wachezaji wanaotaka mshahara mnono nasio Wanaotaka kuipa Timu mafanikio.

✓ Tutaendelea kusajili wachezaji wadogo au wasio na uwezo ili waje kujifunzia mpira Manchester.

✓ Kwa Kocha kama Ole kuendelea kuwepo United basi hata Next season Top 4 Itamkosa ,Achana na Kubeba FA na Makombe madogo ambayo Yamemshinda na Hatabeba kombe lolote.

NB: TIMU KUBWA ZINA MAKOCHA WAKUBWA NA WAZOEFU.
 
Nime-like

Ole kazi alioifanya inaoneka na itazidi kuonekana. Mandezi mnaomponda ole wala msichoke
Msimu mpya Utaanza na nyimbo za kwaya kama hizi zitaendelea.

Timu zinajipanga sio blaa blaa, KAMA ni kujenga Timu bado Ole hatoshi sababu hajawahi kujenga Timu yeyote ikafanikiwa.

Unaposikia Glazer Out usifikiri wale Wamarekani Wakitoka OLE Atabaki Salama.
 
★Ten years ago today, at Wembley Stadium...

Pedro 27'
Rooney 34'
Messi 54'
Villa 69'

Barcelona dismantled Manchester United to win their fourth Champions League title


Their greatest moment under Pep Guardiola?


#GGMU


manutd |
 
★Man United are genuinely interested in Kingsley Coman & are offering €12m p/a after tax. Coman wants to become one of Bayerns top earners.★

#GGMU


manutd |
 
★Ryan Giggs will make his first appearance at Manchester Crown Court on Friday for a plea and trial preparation hearing.★

#SkySports
#GGMU


manutd |
 
Msimu umeisha rasmi jumatano wacha tuteme vinyongo vyetu.
The end justify the means.
Ole hajabeba walau kombe hata moja la kuzugia na mbaya zaidi alikuwa anatolewa na timu zisizotarajiwa kwenye mashindano mbalimbali.
Kwenye FA tumetolewa na leicester ya Brendan Rogers ambaye liverpool walimfukuza baada ya project yake kufeli pale anfield.
Europa kashindwa kuchukua ndoo dhidi ya villareal ya Unai Emery aliyeshindwa kufanya kitu na arsenal pale emirates.
Champions League kashindwa kupata matokeo sahihi dhidi ya waturuki na kahitimishiwa safari na Leipzig ilhali alikuwa ameishatanguliza mguu mmoja ndani ya 16 bora. Sina kumbukumbu sahihi kuhusu carabao alitolewa na nani.

Miaka 3 ni mingi sana kwa kocha sahihi kuonyesha mwelekeo wa timu kama united katika kugombania makombe makubwa na madogo. Kwa walio wengi wanaamini Ole ni mtu sahihi kwa united sababu amerudisha utulivu ndani ya dressing room iliyovurugwa na Pogba (ugomvi wake na mourinho). Binafsi kama ambavyo nimekuwa nikipinga uwepo wake united,sababu kubwa anapungukiwa mbinu dhidi ya makocha wanaofundisha timu tunazoziita midtable ila ana kismarti na timu za top 6. Hii inatoa tafsiri kuwa ana staili moja tu ya ushindi (low blocks kama anavyoisemea mkuu Daemusin ). Bruno amekuwa akichagiza matokeo ya ushindi kwa united kwa kiasi kikubwa nadhani kuliko Ole mwenyewe ndio maana hata mechi ndogo tu za mchangani akikosekana yeye unaona tunacheza mpira usiokua na malengo kabisa. Kwenye mashindano ya carabao,fa,epl,europa na champion league mbinu hubadilika kutokana na mpinzani unayekabiliana naye,hatua uliyopo na hata muda wa ligi unaokuwa umebaki,lakini mbinu pamoja na mifumo ya Ole imebaki ile ile kila siku na kila mechi kwa kila mpinzani.

Sababu ya pili kwa nini Ole si mtu sahihi kwa united ni uoga wake wa kufanya maaamuzi kabla na wakati wa mechi. Tumekuwa tukiona marudio ya makosa ya wachezaji wa kiingereza ndani ya united lakini watalazimishwa kumaliza mechi hivyo hivyo au mechi inayofuata wataanza kama kawaida. Kama rashford alivyomaliza msimu akiwa kwenye kiwango cha chini,ndivyo ambavyo tuliona maguire akilazimishwa kucheza game after game kipindi akiwa hana kiwango cha kuridhisha.

Mwaka 2013 zambia walifuzu kucheza kombe la mataifa huru ya afrika wakiwa chini ya kocha ambaye chama cha soka cha zambia hakikuridhishwa na mbinu pamoja na mifumo yake hivyo wakamtema na kumchukua renee mfaransa ambaye alifikia kuwapa kombe mwaka huo. Hivyo natoa rai tuachane na Ole maana kwa hapa alipotufikisha inatosha hivyo tumtafute kocha atakayeweza kutuvusha hatua hii tuliyokwama na babyface assassin wetu.
ze-dudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…