Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Naona wadau washaanza kumpigia chepuo Edwin van de Sar kuchukua nafasi ya bwana Woodward pale united.
Binafsi naona atafaa kama atapewa mamlaka kamili ya kuchagua watu wa kufanya nao kazi na sio ilimradi kujaza nafasi tu kama sasa.
 
Huyu choko nini...unasave football kwa izo timu zako 12...View attachment 1759484
Sikuisapoti SL sababu hawajaainisha ni kwa namna gani walikuwa wanakuja kuokoa timu nyingine za chini zaidi ya hizo top layers.
Jana niliona Pep akiuliza why ajax who are 4 times champions are not included in that plan?
Pep has my respect for that.
Ole is a coward.
 
Naona wadau washaanza kumpigia chepuo Edwin van de Sar kuchukua nafasi ya bwana Woodward pale united.
Binafsi naona atafaa kama atapewa mamlaka kamili ya kuchagua watu wa kufanya nao kazi na sio ilimradi kujaza nafasi tu kama sasa.
Nafasi ya Ed ni ya kuzibwa na mtu wa uchumi na mipango.

Huyo Van der Sar ni kwenye technical ambako wapo kina Fletcher na mwenziye yule tuliyemtoa everton kipindi cha Moyes.
 
Ole fala sana ndio maana nataka afukuzwe
Hebu ona mchango wa pep na klopp mpaka bosi wa liva katoa mafichoni kuomba msamaha....
 
Lakini inaonyesha hata ajax Van der SAR alianzia kwenye masoko kabla ya nafasi aliyonayo sasa.
Manchester ni kubwa sana mkuu..na kipindi hiki cha hii crisis ya corona basi mtu atakayekuja inabidi awe ameshafanya makubwa kwenye maswala ya fedha.

Huyu Ed kabla ya kuja United alikuwa kigogo kwenye hii bank ya kimarekani iliyokuwa inataka kudhamini haya mashindano ya ESL,JP Morgan.

Tukileta masihara tutafikisha deni la £1B kama Barca na timu itaenda kujifia tu taratibu kwa kushinda kusajili superstars.
 
Hawa matajiri kiliwashinda nini kufuta ili deni??
Kwanini waliliacha likaongezeka ivi huku timu inaingiza faida kila mwaka???
 
Tumepost 160m pound faida kwenye Corona hii, for comparison madrid na Barcelona wapo Hoi, na bayern mwenye UCL hana faida kama sisi. Man united wana structure nzuri ya kuingiza mapato kwa muda mrefu.

Japo Woodward ni clueless kwenye mpira, kuleta clueless mwengine wa fedha na acafocus kwenye mpira pia ni mistake.

Balance ipatikane, mambo ya mpira waachiwe watu wa mpira na mambo ya fedha wabaki nayo watu wa fedha.
 
Hawa matajiri kiliwashinda nini kufuta ili deni??
Kwanini waliliacha likaongezeka ivi huku timu inaingiza faida kila mwaka???
Madrid anarekebisha uwanja wake bado effect za corona na nini ndo visababishi..hizi timu zinaendeshwa kwa gharama kubwa sana..faida inayopatikana inatengwa kidogo kulipa deni.faida ni ndogo kuliko deni,so kulimaliza ni si kazi ndogo.
 
Mkuu si tume-appoint Technical Director,na Director of Football..Bado watu wa mpira hatujawapata hadi CEO awe mtu wa mpira 100pc?
 
Ole fala sana ndio maana nataka afukuzwe
Hebu ona mchango wa pep na klopp mpaka bosi wa liva katoa mafichoni kuomba msamaha....
Makocha wote hao walipata muda wa kujiandaa kutoa speech zao, Ole habari inaibuka ni dakika 20 kabla ya mchezo, kifupi yeye katoa maneno yasiyo ya kukaririshwa kaongea cha moyoni,

Na huyo Pep unaemsifia kwanini Anaitwa Bald fraud? Ni moja kati ya watu wenye mafanikio ya kisoka ila ni binadamu mbaya, yeye na ole ni mbingu na ardhi.
 
Pep ana mabaya gan mkuu...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…