Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Safari ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya manchester united (1)
Yawezekana utawala wa Ole Gunnar Solskjaer akiwa kama ni kocha wa muda pale mitaa ya carrington umeshasahaulika baada ya miaka miwili kupita tokea ateuliwe kuwa kocha mkuu wa manchester united, lakini sidhani kama kuna mshabiki wa manchester united atasahau tukio la comeback lililofanywa na man utd dhidi ya PSG kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya champions league huku Ole akiwa bado ni kocha wa muda (man utd walipata ushindi wa magoli 3 dhidi ya 1). Hapo ndipo ulipozaliwa ule wimbo wa "Ole at the wheel"

furaha na dhoruba kwa wakati mmoja
Baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya PSG, Ole gunnar alihudumu mechi mbili tu akiwa na nyadhifa ya ukocha wa muda (caretaker) wa manchester united na mechi hizo ziliishia kwa man utd kuambulia vipigo na baada ya hapo akateuliwa kuwa kocha mkuu wa manchester united.

kiuhalisia ulimwengu wa bwana Ole kwa upande wa mfumo rasmi wa kiuchezaji, fikra, na mipango aliyokuja nayo tokea mechi ya kwanza (tactical perspective) uliishia usiku ule tuliofungwa magoli 2 dhidi ya PSG ndani ya Old trafford na baada ya hapo kila kitu kikabadilika (wengine wakasema honeymoon imeisha) kwa sababu tofauti ikiwemo majeruhi ya wachezaji muhimu.

Ole alirithi timu iliokosa umoja ndani na nje ya uwanja, licha ya kuwepo kwa mazingira mabaya ndani ya kikosi Ole pia alirithi timu iliokwisha poteza pattern ya kiuchezaji na identity. Ole pia alirithi timu iliokwisha onyesha madhaifu makubwa sana kwenye safu ya ulinzi baada ya kuruhusu magoli 29 kwenye mechi 17.

Jose anafukuzwa, Ole anaanza kazi rasmi:
mechi ya kwanza chini ya utawala wa Ole tulianza na mfumo wa 4-3-3 na high pressing system , mechi ya kwanza tulianza na midfield ya matic, herrera na pogba huku safu ya ushambuliaji tulianza na martial, rashford na lingard.

Kwa aliyesikiliza mahojiano ya ole atakuwa anayakumbuka maneno matamu aliyoyaongea, alisema anataka kuona wachezaji wake wanakimbia sana, pressing ya hali ya juu (chini ya ole, pressing intensity ilikuwa ni 8 ukilinganisha na 10 ya jose mourinho, kwa ufupi tuliimarika zaidi na zaidi chini ya ole ukilinganisha na jose chini ya miaka yake miwili), pasi za haraka za kwenda mbele ndio maana si ajabu alianza na watu watatu hao safu ya mbele na hapo katikati akifaidika na uwepo wa pumzi ya ander herrera aliye kwenye ubora, pogba akitokea upande wa kushoto kama alivyokuwa juventus.

Jesse lingard alikuwa ndiye mzungukaji mkuu wa ndani ya uwanja akiongeza work rate hapo juu na chini, kwa ufupi jesse alisimama kama ni kiunganishi kikuu cha safu ya kiungo na ushambuliaji. Uwepo wa jesse, herrera na matic kiulinzi kulimzawadia uhuru wa kiuchezaji paul pogba kwa mara ya kwanza.

Uhuru huo aliutumia vizuri sana paul pogba kwani alifunga magoli matano (non penalty) ndani mechi 9 za mwanzo za ole gunnar, pia aliweza kuongeza assist nne ndani ya hizo mechi 9, kiwango cha kupiga mashuti kiliongezeka kutoka 2.93 chini ya mourinho hadi 4.08

marcus rashford naye kiwango chake cha kupiga mashuti kiliongezeka kutoka 2.0 chini ya mourinho kwa dakika 90 hadi 4.8 huku pia akifunga magoli 6 ndani ya hizo mechi 9 za mwanzo za Ole gunnar. pia ndani ya mechi 10 tulishuhudia mabadiliko makubwa sana ya kiuchezaji, kitakwimu na kimatokeo,
  • kwa mfano non-penalty xG ( expected goal) per game tulipanda sana kutoka 1.41 chini ya jose hadi 1.90 chini ya Ole.
  • non-penalty xG against tulishuka kutoka 1.43 chini ya jose kwenda 1.07(safu yetu ya ulinzi iliimarika, hatukuwa tunakaribisha mashambulizi ya mara kwa mara)
=================
 
Ndio imeisha iyo
 
Safari ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya manchester united (2)

Ole na mkataba wa kudumu
licha ya kuanza kupata matokeo yasioridhisha ndani ya muda mfupi hilo halikuwazuia watendaji wakuu wa man utd kutokumpa kandarasi ya miaka mitatu ole gunnar solskjaer, wapo baadhi ya wadau waliamini bado haukuwa muda muafaka kumhukumu ole gunnar solskajer (nyakati zile hawa walionekana na wachukiaji) na baadhi yetu tulio wengi tuliamini Ole ndiye mwanadamu pekee mwenye uwezo wa kuitandaza tena DNA ya klabu iliokuwa inapotea kwa kasi ya ajabu hivyo alistahili mkataba wa kudumu licha ya kwamba bado tupo katikati ya msimu.

majeruhi ya wachezaji muhimu na athari zake
yawezekana zipo sababu nyingi sana zilizopelekea Ole aanze kuonja joto ya jiwe pale klabuni lakini hatuwezi kuiondoa sababu ya majeruhi ya wachezaji wetu muhimu kuwa ni kikwazo kimojawapo kilichopelekea dunia imuangalie Ole kwa jicho jengine, wengine walihitaji kumuona Ole anadhihirisha ubora wake kwa malighafi alizonazo.

dakika 90 za mechi dhidi ya PSG ziliharibu kwa kiasi kikubwa ile imani ilioanza kujengwa na mashabiki mbali mbali wa mchezo wa soka dhidi ya ole, kwa kuanzia majeruhi ya lingard na martial ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, licha ya kwamba wachezaji wote hao wawili hawakuwa na takwimu nzuri za kiufungaji lakini uwepo wao uwanjani ulikuwa ni faida tosha ya kimfumo.

Miguu iliochoka ya alex sanchez na juan mata ndio ililazimika kutumiwa na Ole gunnar solskjaer kuziba nafasi ya majeruhi, both sanchez na mata hawakuwa na uwezo wa kuendana na falsafa mpya za mwalimu kutokana na kukosa kwao fitness pamoja na kasi ya kukimbia.

siku chache baadae man utd wakiwa wanajiandaa na mechi dhidi ya liverpool zikazuka taarifa rasmi za kupata majeruhi kwa nemanja matic. Ilipofika mechi ya liverpool tulishuhudia ndani ya dakika chache tokea kuanza kwa mechi mchezaji mwengine muhimu kwenye ule mfumo wa 4-3-3 akipata majeruhi na hapa namzungumzia ander herrera na nafasi yake ilizibwa na andreas perreira.

kimiujiza mchana huo tulishuhudia kurudi uwanjani kwa jesse lingard na kutokana na ufinyu wa kikosi ole alilazimika kumtumia jesse lingard licha ya kwamba bado hakuwa fiti kimapambano, mchana huo tulishuhudia kwa mara nyengine tena jesse lingard akipata majeruhi na nafasi yake kuzibwa na juan mata.

mchana huo huo pia tulishuhudia tukio jengine la kusikitisha lililomhusu mchezaji mwengine muhimu anayeunda mfumo ule wa 4-3-3, hapa namzungmzia marcus rashford na jinamizi la majeruhi alilolipata baada ya kuchezewa rafu na jordan henderson. Licha ya rashford kuendelea kucheza ndani ya mechi hiyo ila hakuwa tena na uwezo hata wa kukimbia jambo lililopelekea unite waonekane kuwa na wachezaji 10 kwa 11, baada ya hapo marcus rashford naye alianza rasmi jinamizi hilo la majeruhi.

mabadiliko ya tactics
majeruhi ya wachezaji takribani wanne muhimu ndani ya kikosi cha kwanza yalimfanya Ole afikirie njia mpya ya kutengeneza kikosi chake kwa kutumia mfumo mwengine wa kiuchezaji kutokana na kundi la wachezaji waliopo na hapo ndipo tulipoanza kuufahamu upande wa pili wa Ole, si hivyo tu hapo ndipo Ole na makocha wengineo mfano wake wanaokutana na changamoto ya majeruhi wanapopaswa kutuonyesha upande wa pili wa ufundi wao (kupata matokeo bora kwa malighafi ulizonazo).

Majeruhi yalipelekea tushuhudie mabadiliko ya mara kwa mara ya mifumo ya kiuchezaji, zipo baadhi ya mechi tulicheza na 4-4-2 diamond tukimtegemea juan mata, zipo baadhi ya mechi tulicheza 4-3-3 tukimtegemea sanchez eneo la ushambuliaji huku romelu lukaku akicheza winga licha ya kwamba kiasili yeye ni namba 9 mahiri kuliko wengineo tuliokuwa nao kipindi hicho.
kwa ufupi baada ya kuvurugika kwa ile 4-3-3 aliyoanza nayo siku ya kwanza ya kukabidhiwa timu bwana OIe hakuwa na mfumo rasmi wa kiuchezaji na kubaki na ubabaishaji (labda tuseme hakuwa anawafahamu wachezaji wake).

majeruhi ya matic na herrera yalizalisha tatizo la ukosefu wa ball progressing, ball winners kwa wachezaji waliorithi nafasi zao (namzungumzia fred, mctominay, perreira) jambo lililokuwa linamlazimu paul pogba afanye majukumu ya kutafuta mpira chini na kucheza long pass kwa safu ya ushambuliaji.

kurudi kwa wachezaji walio majeruhi
licha ya kwamba baadhi ya wachezaji muhimu waliweza kurudi uwanjani lakini bado hali yakiuchezaji ilishindwa kuimarika kwa kiwango kilichozoeleka na hapo ndipo ubora wa ole juu ya game managements ulipozidi kujadiliwa
  • rashford alifunga goli 1 badala ya lile alilofunga dhidi ya psg (naruhusu marekebisho)
  • romelu lukaku (winga teleza wa Ole) alishindwa kufunga goli, martial naye alifunga goli 1
  • manchester united walicheza dakika 530 bila ya kufunga kupitia open play.
kunyimwa mkataba kwa ander herrera
chini ya ole tulishuhudia kupewa mkataba mpya kwa scott mctominay ambaye alionekana kama ni damu mpya ndani ya kikosi cha man utd tokea alipoanza kupewa nafasi na ole dhidi ya liverpool pia tulishuhudia kutokufikiwa kwa makubaliano ya kimkataba dhidi ya herrera na hatimaye jamaa akatangaza kuondoka kikosini dirisha lijalo.

tukumbuke katikati ya ligi baada ya kupata majeruhi kwa ander herrera wachezaji waliopo walishindwa kuziba nafasi yake kiufasaha na naamini mpaka leo hii bado tumeshindwa kupata ile chemistry ya kiuchezaji tulioishuhudia kutoka kwake tunapoanza na fred mctominay.

kupewa mkataba mpya kwa martial
baada ya kuteuliwa kuwa kocha mkuu, ole alihitaji kujenga timu itakayoongozwa na fikra zake mwenyewe na alianzia kwanza safu ya ushambuliaji kwa kumpa kandarasi mpya martial aliyeamini ndiye namba 9 sahihi kwenye kikosi kwa msimu ujao (lukaku alianza kucheza kati mechi za mwisho licha ya baadhi ya wachezaji kurudi)
Martial huyu aliyepewa kandarasi mpya ya miaka 5 cha kustaajabisha alifunga magoli mawili ndani ya muda wote wa uongozi wa Ole kama nitakuwa sahihi.

  1. Je martial alistahili kuwa mshambuliaji badala ya lukaku?
  2. je herrera ulikuwa ni muda muafaka kwake kuondoka kwa kuwategemea scott, perreira na fred?
======================

Nitaendelea insha'allah
 
Safari ya Ole Gunnar Solskjaer ndani ya manchester united (3)

msimu mpya, usajili na mfumo mpya
msimu wa 2019/2020 tulishuhudia kwanza mabadiliko rasmi ya kimfumo kutoka ule alioanza nao akiwa caretaker (4-3-3) hadi kuelekea 4-2-31 akiwa kama kocha mkuu na tukumbuke mfumo ulichukua takribani miezi mitatu hadi kuanza kutumiwa rasmi.
tulianza msimu mpya huku tukiongozwa na maswali mengi yaliokosa majibu rasmi kwa nyakati zile.
  • wachezaji wapya wataleta impact gani ndani ya kikosi (james, bissaka, maguire)?​
  • ilikuwa ni sahihi kumuondoa ander herrera bila ya mrithi wake kutafutwa huku tukiwaamini zaidi waliopo?​
  • ilikuwa ni sahihi kumundoa romelu lukaku kwa kumtegemea martial kama ni false 9?​
  • je ni lini tutatatua tatizo la winga wa kulia au ndio usajili wa james ndio muokozi wa eneo hilo kutoka Championship?​
  • ni yupi mchezaji wetu wa kutegemewa?​
pia nakumbuka nyakati zile za maandalizi ya msimu mpya humu ndani mijadala inayohusu mustakabali wa timu iliendelea mara kwa mara, kupitia matokeo ya mechi za pre season baadhi yao waliamini timu imebadilika na wengineo waliamini bado tupo vile vile kama tulivyomalizia msimu. Nimeikumbuka kauli yangu kabla ya ligi kuanza msimu ule
"mashabiki wa man utd tuache kujificha kwenye kivuli cha mchicha tukiamini hatutoathiriwa na mvua"
dhumuni kuu la usajili linaendelea kuwa ni lile lile la kuimarisha kwanza safu ya ulinzi ilioruhusu magoli takribani 54 kwa mechi 38, kutengeneza safu ya ushambuliaji itakayoongozwa na wachezaji vijana wenye ari ya kupata mafanikio huku lengo kuu ni kuzigeuza zile mechi tulizotoa suluhu au kufungwa kuwa ni ushindi utakaotokanwa na uimara wa safu ya ulinzi iliiongezewa mabeki wawili wa gharama kubwa kwa pamoja (paundi millioni 140).

herrera aondoka na 4-3-3,
kuondoka kwa herrera na kushindwa kuletwa mchezaji mbadala wake ulileta tafsiri ya kwamba yule paul pogba aliyepewa uhuru wa kucheza kushoto na Ole sasa anarudi rasmi katika hali yake ya mwanzoni (mfumo wa viungo wawili wa mourinho). Kutokana na performance mbovu ya fred kwa msimu wa mwanzo wa ligi hapakuwepo na mchezaji mwengine mwenye uwezo wa kudeliver performance mfano wa ile tulioishuhudia kwa ander herrera kwa wachezaji waliokuwepo (fred, mctominay, perreira)

mabadiliko ya mfumo na uwepo wa martial na rashford
Ole alijenga timu kwa kuwaangalia zaidi wanadamu hawa ambao msimu uliomalizika walishatuonyesha kwa mara nyengine tena ile sura yao ya kukosa makali ya kudumu (consistency).
  • martial alifunga magoli 4 ndani ya miezi sita ya mwanzo ya Ole (naruhusu masahihisho)​
  • rashford alianza kwa kufunga magoli 6 ndani ya mechi 9 za mwanzo za ole, mwishoni mwa msimu rashford alimaliza na goli moja tu ukiachana na lile alilofunga dhidi ya psg kwa njia ya penalty (naruhusu masahihisho)​
Ole alisahau yote hayo badala ya kumalizika kwa msimu na hatimaye akaamua kuulisha ubongo wake mawazo hasi tu juu ya wachezaji hao wawili (alijisemea moyoni hawa ndio watakaonifikisha nchi ya ahadi).
faida moja kubwa ya martial ni ubora wake wa kufunga pindi anapokuwa karibu na goli ila anakuwa useless akiwa nje ya box, hivyo basi ilihitajika plan itakayomfanya martial awe anakimbia kuelekea golini mara kwa mara

ligi inaanza rasmi, ushindi mkubwa dhidi ya chelsea, matic na sintofahamu yake
mechi nne za mwanzo Ole alimtumia paul pogba namba 8 pamoja na scott mctominay nafasi ambayo ulikuwepo uwezekano wa kumtumia nemanja matic then paul pogba acheze namba 10 au juan mata, kinyume chake alikuwa anamtumia andreas perreira au jesse lingard kwa takribani miezi minne ya mwanzoni.

licha ya paul pogba kucheza chini zaidi bado aliendelea kuwa muhudumu bora kwa safu ya ushambuliaji kwa kutumia ufundi wake wa kupiga pasi ndefu, jambo lililokuwa likisaidia washambuliaji wetu wawili kuweza kukimbia kutoka nyuma ya nafasi ilioachwa wazi na adui na mfumo huu ulitusaidia sana kwenye mechi dhidi ya chelsea tulipopata ushindi wa magoli 4.

majeruhi yaanza tena, je ole alijifunza ya msimu uliopita?
mkakati huu wa kumdeploy pogba ulifanya kazi kwa kiasi kikubwa sana mpaka pale martial na paul pogba walipopata majeruhi na hatimaye rashford akarudi eneo la ushambuliaji. Majeruhi ya paul pogba yaliodumu kwa takribani majuma sita tofauti yalipelekea timu ikose creativity ndio maana si ajabu ilifikia hatua timu ilifunga magoli mawili.

twende na counterattacks
kutokana na ufinyu wa wachezaji wenye ubora si vibaya kama nitasema wachezaji wa manchester united wa kikosi cha kwanza walikuwa wakijichagua wenyewe ukiachana na baadhi ya maeneo kama vile beki tatu na namba 10 yaliokuwa na wagombeaji wengi wa nafasi.

Ole alishape timu kuelekea 4-2-3-1 ambapo tulishuhudia martial akiwa ndiye false 9, huku rashford na daniel james wakishuka chini zaidi kupitia pembeni ili kutengeneza space ya kukimbia.
Kupitia mfumo huu tulishuhudia marcus rashford akifunga magoli 11 kutoka oktoba hadi january (magoli 8 ni open play),
kwa upande wa daniel james kwa kutumia zaidi mbio zake tulishuhudia akiwa ni creators zaidi ya ufungaji japokuwa tulishuhudia mwanzoni mwa msimu alifunga magoli matatu ndani ya mechi 4, kutoka oktoba hadi January alifanikiwa kutengeneza assist 6 ndani ya mechi 11.

kipi kitatokezea unapocheza na wajanja zaidi yako
kupitia mfumo huu mmoja wa kiuchezaji baadae ulipelekea wingu zito kwa upande wa timu ya manchester united, timu nyingi ziliamua kuja na mfumo wa kukaa chini zaidi (low blocks) kwa kucover space behind.
kwa kuwa man utd imekosa creativity hususani kwa midfields (lingard, perreira, fred, scott) wenye profiles bora kwenye eneo la upigaji wa pasi through the lines na kutengeneza movements (mpaka sasa tatizo hili lipo) mwenendo wa manchester united ukaendelea kuwa ni mbovu.

baada ya kumaliza mechi ya chelsea, mchambuzi wa sky sports anayeitwa jose mourinho alisema
I think United will find it much more difficult to play against teams with low compact blocks, if the block is low blocks, it will be really difficult for them without pure striker"

kilichotokezea kwa baadhi ya mechi dhidi ya low blocks mpaka september.
wolverhampton 1 vs man utd 1
man utd 1 vs crystal palace 2
southampton 1 vs man utd 1
man utd 1(penalty) vs leicester city 0
man utd 1 vs astana 0
westham 2 vs man utd 0.​

je tatizo la ukosefu wa creativity ole alitatuweje na dirisha limekaribia?
============================
itaendelea Insha'allah
 
Nguvu zote mnakuja kumalizia kwa city ,Milan anakuja kuwapelekea moto hapo OT

Nguvu ya soda tu

Man utd sio timu ni genge LA wahuni

Westahm anakuja kuwapelekea moto mwingine mkali
Usitutishie kujamba wakati una harisha.......
 
★Bruno Fernandes has covered the most distance of any #mufc player in the Premier League this season. His biggest distance came against Brighton in September and he was close to topping that against Man City last weekend (both over 12km each)★

#GGMU


manutd |
 
★Solskjær: "There are a few players I’ve played with that I’d love to have in my team, of course. I’d love the player Roy Keane, I’m not sure if I could manage him though!"

Solskjær: "I’d sign him [Keane] every day of the week, Roy was so influential but then again, I played with Cristiano and he’s been the best player in the world alongside Messi for the past 10 to 15 years now, so Cristiano. You’d take him in your team, for sure."

NAONA KAMA CR7 ANATAFTIWA MAZINGIRA YAKURUDI★

#GGMU


manutd |
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…