Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Huyu fala mbona anajiskia sana na zaidi anacheza mpira mbovu, au ni hayo magoli 85 ndio yanampa kiburi matako yake... Magoli 85 anacheza kama hataki je angekua na magoli idadi ya Wayne Rooney si angekua anaingia na sahani ya chakula uwanjani
Collective efforts zinawin over individual efforts. By the time manchester ikianza kucheza kwa patterns of play nadhani mtakuja kuona ubora wa wachezaji.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Sas beki wamekosa nn wametoa cleansheet wewe. Timu leo ilikosa cuttinge edge upfront. Zero Creativity.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
Read between the line..

McFred kukaa sana nyuma hakusaidii timu offensively,kunaisaidia defensively..usidhani kila mtu akiandika kitu anaandika tu kwa kukurupuka.
 
Kuna vichezaji flani flani tunavyo pale man u vinakera sn, mwanzo alikuwa Fellaini na Lingard now vimebaki hivi viwili na sidhani kama vitaondolewa labda tubadili kocha.
Ukitaka kujua kocha nd tatizo lingard anafanya nn sahivi west ham? Yani shida ya mpira wa solkjaer unataka mtu awe na uwezo binafsi sana. Sasa je hao wachezaji utapata wapi na kwa shngap?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Vitu vitatu vilivyotukosesha ushindi leo:

1. Tumenyimwa penalty ya wazi pamoja na VAR kutumika.

2. Ole Gunnar Solskjaer ni kocha wa kawaida sana, United ina wachezaji wakali ila mpira wanaocheza ni kituko.

3. McTominay katulaza na viatu kama mdogo wake Rashford alivyofanya kwenye game ya Liverpool pala Anfield. Nilitegemea Scott atapiga mpira wa juu kwenye ile counter attack badala yake akapiga chini ukaishia miguuni mwa mabeki wa Chelsea.

Chelsea leo wametuzidi karibia kila kitu uwanjani, ni wazi unaona mabadiliko yao kiuchezaji chini ya Tuchel. Hapa kwa Ole tutasubiri sana.
 
Read between the line..

McFred kukaa sana nyuma hakusaidii timu offensively,kunaisaidia defensively..usidhani kila mtu akiandika kitu anaandika tu kwa kukurupuka.
ndio maana nikapendekeza fred atolewe sadaka kama itakuja ofa sahihi, najuwa wengi wetu tunamuona jamaa ana work rate kubwa sana akiwa uwanjani, good in pressing lakini jamaa bado hatoshelezi kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kwa timu inayopigania ubingwa.

bado ana madhaifu mengi sana ya kiufundi, kwa fedha iliotumika kumsajili (paundi millioni 52) alipaswa awe quick-witted pindi anapokuwa uwanjani, (kwa ufupi awe na kitu tofauti na wachezaji wanaomzunguka kama alivyo bruno fernandez).

huwezi kumtoa sadaka scott mctominay kirahisi rahisi licha ya kwamba anazidiwa kiubora na fred kwa sababu ya umri wake, bila ya kusahau dogo ni mzaliwa wa pale england na anatokea academy

tusidanganyane hakuna timu itakayokubali kulipa paundi millioni 50 kwa fred, situation yake naifananisha na usajili wa anderson miaka 12 iliopita kwa paundi millioni 18, hatimaye akauzwa kwa bei ya kutupa.

  • fred anazidiwa na kovacic
  • fred anazidiwa na gundogan pamoja na rodri
  • fred anazidiwa na fabinho pamoja na widjnaldum
  • fred anazidiwa hata na thomas partey huyu mgonjwa
==================
combo ya fred na scott ni kuendelea kumtuma bruno kama punda wa muembe makumbi kwa sababu wote wawili ni wabovu sana kwenye upigaji wa progressive pass, mara nyingi bruno akicheza na hao wajinga humlazimu ashuke upande wa kushoto zaidi kutafuta mipira.

angalau tungelikuwa na DM mmoja mwenye sifa za thiago au kovacic hapo ingelikuwa afadhali sana kwa sababu ya ubora wao(ball retention wako vizuri, progressive pass wapo vizuri, quick pass, football intelligence)
 
Kuna vichezaji flani flani tunavyo pale man u vinakera sn, mwanzo alikuwa Fellaini na Lingard now vimebaki hivi viwili na sidhani kama vitaondolewa labda tubadili kocha.
Anthony Martial huyu jamaa ana miaka 25 kwa umri huu alipaswa ndiye awe tegemeo kwenye timu amecheza PL zaidi ya miaka 5 ila ni mtu hovyo sana.

Marcus Rashford ana miaka 23 ila anacheza kama kinda kila siku huoni aki-mature huyu mpuuzi sioni akibadilika kuwa mchezaji wa maana japo ana potential zote za kufika mbali.

Kama tupo serious na kujenga timu hawa wachezaji watatupotezea sana muda wana utoto mwingi sana sioni hata msimu ujao tukiendelea kushindania makombe na wachezaji wasio na perfomance consistency.
 
Kimsingi mimi sioni kama Fred ndo anayetunyima ushindi au kutufanya tusicheze vizuri..Shida naona ni wanapewa majukumu yanayofanana(McFred) na muda mwingi wanacheza sambamba nyuma sana na inakuwa kazi kucheza key pass mbele..

Kwenye viungo tulionao hakuna anayecheza quick penetration passes za haraka kama Fred i my opinion,mfano ile aliyompa
Scot..

Nakubaliana na wewe kuwa bado hatoshi lakini sio tatizo kubwa hivyo..ishu ni setting ya timu.
 
sipo kwenye habari za matokeo ya uwanjani kwani eneo hilo namlaumu zaidi ole gunnar.
kama tunahitaji kuwa washindani barani ulaya tunahitaji kwanza tuwe na midfield wenye uwezo wa kuvuka ubora wa hawa tulionao, kwa sasa uwezo wa kununua bila ya kuuza ni mdogo sana(matajiri wetu si waarabu na corona inazidi kuadhibu vyanzo vya mapato ya uwanjani).

kama kutahitajika kuuzwa mchezaji ndipo aletwe mwengine ndio nimependekeza fred atolewe kafara.
sijamtaja matic kwa sababu safari yake inakaribia.
kama tutaianza tena ligi msimu ujao huku midfield wetu wakiwa ni scott fred basi hadithi zitakuwa ni zile kwa zile.
 
Darmian & Daemusin,

Sioni timu ikiwa imara kama tukiendelea kutumia viungo wawili eneo la ulinzi tunakuwa dhaifu sana offensively.

Ole inabidi abadili mbinu unaposhindania mashindano yenye mechi nyingi mbinu ya kujilinda haiwezi kukupa mataji hata siku moja. Sare sio ushindi.
 
sielewi ni kwa nini alisajiliwa donny van der beek.
hivi huyu jamaa alipokuwa ajax alikuwa anacheza nafasi gani?
jamaa ameanza mechi mbili tu za ligi, huo uzoefu ataupatia wapi kama anaendelea kuwekwa nje
 
Sioni timu ikiwa imara kama tukiendelea kutumia viungo wawili eneo la ulinzi tunakuwa dhaifu sana offensively.
hata huo upande wa ulinzi pia hatupo imara ndio maana tumeruhusu magoli mengi yanayofanana.
  1. kwanza degea halitawali box dogo, sijui huu woga anautolea wapi
  2. tupo ovyo sana linapokuja swala la position, shape yetu ya uchezaji haivutii
  3. wachezaji hawatimizi majukumu yao ipasavyo, kuna baadhi ya magoli tunafungwa huku nyuma tukiwa wachezaji wanne
  4. winga wetu ni wavivu sana kwenye kulinda
  5. pressing yetu ina mashaka, only bruno na cavani kule mbele ndio huanzisha pressing japokuwa leo tumejitahidi
 
Read between the line..

McFred kukaa sana nyuma hakusaidii timu offensively,kunaisaidia defensively..usidhani kila mtu akiandika kitu anaandika tu kwa kukurupuka.
Hujakurupuka tunazungumzia mpira hapa. Moja ya game tulizookota magoli mengi ambayo ni against southampton na leeds utd wamecheza hao wawili. Hakuna point hapo game nyngne ameshiriki Pogba then whats happened. Kocha nd anaechezesha hivo wawe wanashinda nyuma. Guardiola sometimez anaweka ferna na rodri kati kati ila bado anafany vizuri. Hata Gundogan sio mchezeshaji kama de bruyne ila watu wanashinda. Halafu man utd ni timu inayotakiwa iattack lawama za mabeki ni bure 2 hazina mashiko.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Kwa nafasi anayocheza Fred alitakiwa awe kiungo mchezeshaji sasa yeye ni butua butua tu na ndio maana Man U bila counter au Penalti hamuwezi funga. Mc Tomynay alitakiwa awe kiungo mshambuliaji ila nyie mnamfanya kiungo mkabaji. OGS anao wachezaji wazuri ila hajui kuwatum ia kama alivyokuwa Lampard wetu
 
Ikifika stage kila mchezaji akawa analaumiwa basi ujue tatizo hapo sio wachezaji tena kama inavosadikika. Toka lini timu ikabadilishwa kikosi kizima. Nawaonea huruma sana hawa madogo laiti kama wangemkuta babu wangekula raha sana. Madogo hawa wanacheza chini ya makocha wa hovyo hovyo 2. Nd maan waling'aa sana kwa Van Gaal. Yule mzee ana mapungufu yake ila falsafa za vijana alikuwa vizuri sio utopolo wa sahv huu.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…