Ndiyo, naongea kwa kujiamini kwa sababu mimi ni mfuasi wa Man United; hivyo ninaelewa mambo yalivyo kuanzia kwenye uwanja hadi boardroom.
Sasa kama ndivyo, hiyo si inadhiirisha alivyo super sub? Unakumbuka Ole Gunnar alishapiga goli 4 baada ya kuingia uwanja kama sub katika dakika 12 za mwisho za mchezo dhidi ya Nottingham Forest?
Kumbuka pia ligi ya Uingereza ni ya kasi sana; huwezi kuifananisha na ligi ya Mexico!
Thibitisha! Leta ushahidi wa games alizocheza dakika 90 pale United; na ulete thathmini ya jinsi alivyocheza.
Hiyo system haikuji tu bila kupimwa; pale kuna wataalamu kuliko mimi na wewe. Sasa wenyewe wanamwona Javier anafaa kuwa super sub. Na hadi sasa ameonekana kufit ile mbaya katika mfumo huo!
Narudi tena kwa Ole Gunnar a.k.a baby-faced assassin, yeye alikuwa super sub pale United na alifunga magoli 91 jumla. Katika kipindi chake akiwa United kuanzia mwaka 1996-2007, ni msimu wa 2001/2002 ndiyo alianza kama mshambuliaji wa kuanza akiwa na Ruud van Gol!
Alipoulizwa siri ya usuper sub wake, Ole Gunnar alijibu: "I had to think about myself, how can I do the most damage for the opposition if I come on? I sat there and I studied football games but I didn't exactly analyse their strikers. Instead I would pay attention to what the defenders and full-backs were doing wrong".
Hivyo Javier anaweza kuwa legend pale United kwa kuwa super sub; na fews games akianza na kutoka. Na hata kutungiwa nyimbo kama super sub baba-faced assassin alivyotungiwa pale OT!