Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hahaha Mwandende anataka atengeneze mfumo wake mwenyewe ili DVB acheze pamoja na kina Pogba na Bruno.

Labda tumuulize nani kati yao atacheza kama DM ?
 
Okay
 
Yaa,,anacheza chini ,,kidogo,,ila wanakuwa wanacheza kwa pamoja kwa ushirikiano..POGBA,,VDB na FERNANDEZ..
Mkichezesha kiungo hao watatu kiokwel mtajiexpose sana maana hamna natural dm hapo. Anahitajika mtu atakayelink defence na forward line pogba hawez hiyo kaz na uliona kipind cha morinho alikuwa akimpa role ya kukaba na alikuwa anaanza kupoteana kwahio there is no way hawa viungo watatu watacheza pamoja yaani mkichezesha hivyo mtafungika kirahisi sana
 
Mkuu nimekupa prediction jinsi watakavyocheza,,,
Zipo njia mbili au tatu..
1 ..vbd atacheza kulia ,,tunaua wings ya kulia
2..atacheza matic,, kama DM then pogba,,vbd,,na Fernandez watacheza kwa pamoja huku tumeua wing moja,,
3..tukacheza bila matic na kuwaweka wote pamoja bila kuua wings zetu..
Hilo linawezekana na ole alishatumia sn,,
 
ni kweli kabisa tena ole asije akajaribu hata siku moja kucheza bila DM halisi maana siku hiyo tutasonyana humu ndani sana.
 
4-4-2 Diamond ndio mfumo pekee utakaowawezesha VDB, POGBA na BRUNO kuweza kuanza kwa pamoja huku wakilindwa na MATIC katika kiungo mkabaji...Ila tofauti na hapo timu itapata shida sana na hivi sioni kama kuna dalili yakusajili beki wa kati.

Kuhusu namba 9 kwakweli hawa wazee naona waache masihara kabisa katika eneo hili...Martial ni mzuri ila ni laini sana, hapendi shida yule chalii lazima aletewe mtu mwingine ili achangamke pindi akianza kukaa benchi(wakachukue hata Cavani atusogeze hata misimu miwili) ila kumwacha Martial tutaendelea kugombea nafasi za kucheza UEFA tu.
 
Chelsea na Man U sijui wameishiwa

Third release kit ya Chelsea copy and paste ya Crystal Palace
Third release kit ya Man U copy and paste ya Newcastle
View attachment 1563171
Kuna kitu kimoja kuhusu hii jezi. Mchoro wa hii jezi unaitwa Dazzle Camouflage.
:
Dazzle camouflage ni mchoro ambao ulikuwa unatumika kwenye vita vikuu vya kwanza vya dunia.
:
Dazzle camouflage kwenye meli za Kivita ilikuwa inachorwa kwa kumaanisha hao ni MA - FIGHTER , WANA SPEED , HAWAPIGWI OVYO.
:
Wenzetu kibiashara kila kitu huwa kina kuwa na theme au meseji ya kibiashara.
:
Meseji ambayo wateja wengi huwa wananunua kwa ajili ya kunimotivate n.k.
:
Wenzetu hawauzi bidhaa wanauza feelings iliyopo ndani ya bidhaa.
:
Feelings zinazowekwa kwenye bidhaa ndiyo huwa zinanunuliwa.
:
Mtu ananunua feeling ya NIKE na siyo kiatu pamoja na kwamba kiatu kinaweza kikawa kizuri lakini ile feelings ya JUST DO IT inanunuliwa sana.
:
NDIYO maana asilimia kubwa ya Campaigns za Nike ni kuhusu na ujumbe wao wa Just Do It na siyo Campaign za kutangaza mchoro wa kiatu.
:
Watu wana focus kwenye kuuza na kununua feelings iliyopo ndani ya bidhaa.

Turudi kwenye hii Dazzle camouflage. Kwanini Nike walifanya vyema kwenye design ya Dazzle camouflage ? kwenye viatu na jezi ya timu moja huko Marekani ?Walichukua meseji ya Dazzle camouflage ( FIGHTER , SPEED , UNBEATABLE ) afu wakachanga na yao ile ya Just Do It .
:
Wakawezeka kutuambia Just Do It kwa sababu wewe ni fighter , una speed ya kukimbilia mafanikio na uko unbeatable.

Watu wanatumia aspirations na siyo price na uzuri kuuza jezi zao.Adidas baada ya kuona hivo wakacop design ya dazzle camouflage.
:
Lengo lile lile kuichukua meseji iliyopo kwenye Dazzle Camouflage. Meseji ambayo ilikuwa inatumika kwenye vita kuu vya kwanza vya dunia.
:
Meseji hii itafanya kuuza jezi nyie dunia ya tatu mtalalamika kuhusu ubaya wa jezi lakini dunia ya kwanza kwenye soko la Adidas watakuonesha namna ya kuuza feelings za hizi jezi ambazo sisi tunasema ni mbaya.
 
Hakika kabisa mkuu,,lazima tupate striker mwenye nguvu na mwenye uwezo wa kufunga magoli aina zote,,
Bila hivyo ubingwa tusahau..
 
★Real talk★
 
Nimeona tetesi za Man united kumtaka Alex Telles wa FC Porto
hata wolves pia wanamtaka.......usajili wa sergio reguilon huenda ukawa mgumu kwa sababu real madrid inavyosemekana wanahitaji kuwepo kipengele cha buy-back clause.
kama watamuhitaji tena mbeleni wawe na mamlaka ya kumnunua kwa bei fulani
 
hata wolves pia wanamtaka.......usajili wa sergio reguilon huenda ukawa mgumu kwa sababu real madrid inavyosemekana wanahitaji kuwepo kipengele cha buy-back clause.
kama watamuhitaji tena mbeleni wawe na mamlaka ya kumnunua kwa bei fulani
Nadhani kwa age yake wanaona huenda akawa na future nzuri huko baadae hasa ukizingatia Marcello anamalizikia na back up yake hawaonyeshi kupanda viwango
 
Kama wamewatengenezea watu Wa dunia ya kwanza basi sawa ila kwa Mimi hapana asee!
 
Kama wamewatengenezea watu Wa dunia ya kwanza basi sawa ila kwa Mimi hapana asee!
Dunia ya tatu ni lini watu walinunua jezi original/original replica ya £75-100??..si wananunua tu za Tsh15k zinazofyatuliwa uchochoroni China na kuanikwa pale Kariakoo?
 
Nadhani kwa age yake wanaona huenda akawa na future nzuri huko baadae hasa ukizingatia Marcello anamalizikia na back up yake hawaonyeshi kupanda viwango
swadakta, pia wanaweza kutufanyia kama vile ishu ya moratta na juventus.
real madrid walikuja kutengeneza faida baada ya kumuuza tena chelsea baada ya kumnunua tena kutoka juventus (kama nitakua nipo sahihi).

man utd pia waligomea dili la haaland kwa sababu kubwa ya buy clause, raiola na baba yake haaland walihitaji wapige hela pindi mchezaji atakapouzwa
 
Yeah nafikiri ni utamaduni wao Real Madrid kufanya hivyo kwa wachezaji wao vijana ili wapate unafuu watakapotaka kumnunua.

Uko sahihi kwa Morata nako alifanya hivyo hivyo wakati wanamnunua kutoka Juventus.

Then wakaja kumuuza chelsea kwa dau kubwa mara mbili ya kile walicholipa kwa Juventus.
 
The history of the United third kit


★Naona Kheri zilizopita kwakweli kuliko hii Mapunda Punda



manutd |
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…