Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kumbe waliingia, nilifikiri walianza

By the way unabishana na mtu/timu aliyekupiga mara 3 msimu huu, ujasiri huo unatoa wapi?
Umempiga mara 3 ila amekuzidi bado kwenye msimamo wa EPL,jana umekula goli 3 mtu anaenda final,hahahaaa! Poleni sana,ila endeleeni kujifariji.
 
Hapa sina haja ya kubishana

Ukweli wa Man Utd ulionekana baada ya Pogba, Martial, Greenwood kuingia

Usitake kuniambia majembe yenu mnayoyaaminia ni akina Tomori, Abraham
Mwanaume hana visingizio...hukubali kuwa amezidiwa....visingizio vyanini wakati hicho kikosi alokipanga ni kocha wenu....TULIA DAWA IINGIE....UMEPIGWA za kutosha.....

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni nondo yenye ujazo
 
  1. team zote zina equal share jambo linalopelekea kila timu ivune gawio sawa na msimu wa 2018/2019 kila team ilipata paundi millioni 80
  2. utofauti wa mapato hujitokeza pale wanapoangalia nguvu ya timu kimatokeo ( merit payments) ambapo mshindi wa kwanza anapata zaidi ya mshindi wa pili na wengineo. Msimu uliopita man city walipata paundi millioni 38 za kubeba ubingwa huku liverpool walipata paundi millioni 36 kwa kushika nafasi ya pili
  3. halafu nadhani wanaangalia team ambayo itakayoonyeshwa zaidi mechi zake moja kwa moja (live match), hapa mara nyingi team yenye ushawishi mkubwa ndio huvuna zaidi pasina kuangalia matokeo husika ya team hiyo, msimu uliopita mechi za liverpool zilionyeshwa live mara 29 huku man city mechi zao zikionyeshwa live mara 26 (city hatimaye walivuna paundi millioni 30 na liverpool walivuna paundi millioni 33, cha ajabu zaidi man utd walioshika nafasi ya sita walivuna paundi millioni 31, inamaana man utd amemzidi bingwa man city)
  4. ukipiga hesabu jumla ya mapato ya msimu unakuta liverpool amemzidi man city kwa tofauti ya paundi millioni 1 (152 millioni vs 151 millioni kwa mujibu wa msimu uliopita)
mapato ya televisheni na dividend kwa shareholder ndio yanayowapa jeuri vilabu vya uingereza kwenye soko la usajili na mishahara kwa sababu vina uhakika wa kupata fedha nyingi.
======================
kwa mujibu wa the guardian:

  • msimu wa 2017/2018 vilabu 20 vya uingereza vilijikusanyia mapato yanayofikia paundi billioni 4.8 na gharama za mishahara ilikuwa ni paundi billioni 2.4
  • ukija la liga vilabu vya 42 (la liga 1 and 2) kwa pamoja vilijikusanyia mapato yanayofikia paundi billioni 4.48.
  • ukija ujerumani vilabu 36 (bundesliga 1 and 2) vilijikusanyia mapato yanayofikia paundi billioni 4.42
=========================================
kabla ya mabadiliko ya msimu wa 2014/ 2015 hali ilikuwa hivi nchini spain ni mwendo wa 38% au zaidi kwa wababe wakubwa


===========================
baada ya mabadiliko hali imekuwa hivi kwa misimu miwili iliopita hao wababe wawili mgawanyo umepungua kwa 23% ukilinganisha na mwanzoni

  1. la liga team ya mwanzo msimu uliopita kimapato ambayo ni barcelona imekusanya euro millioni 166 na team ya mwisho imepata euro millioni 44
  2. uingereza team ya mwanzo msimu uliopita kimapato ambayo ni liverpool walikusanya euro €180m ($200m) na team ya mwisho ambayo ni Huddersfield walipata euro €114m ($127m)
 
Chelsea wametufunga easy goals sana jana..
tokea ligi irudi tumekuwa tukiruhusu magoli mepesi zaidi kufungwa
  1. mechi ya spurs beki walitegeana wakiongozwa na maguire halafu degea akashindwa kupunch mpira kwa nguvu
  2. mechi ya bournermouth maguire alipigwa chenga ya kifala ndani ya box, degea akashindwa kuziba nguzo ya goli.............goli la pili refa alisema bailly amenawa mpira ndani ya box
  3. mechi ya southampton walitufanyia higher pressing hatimaye pogba akapoteza mpira
  4. mechi ya jana hayasemeki (giroud na uzito wake anauwahi mpira wa krosi dhidi ya lindeloff, degea anajichanganya)
 
Kumbe EPL anakula mpunga mrefu ivyo!! Kwanin sasa mkuu...me nnanvyojua UEFA ndo ina mpunga mrefu then epl afu FA ndo ije europa na mengineyoo..au!!!
Uefa ndo inampunga mrefu ukichanganya na bonus za kushinda kila mechi na kama umeingia hatua nyingine kuna bonus pia

Na katk makombe ambayo hana fedha ni FA na EFL bora hata Europa inapesa kuliko hayo makombe ndani
 
Ule ni uzembe.

Alilegeza mguu mpira ukamgonga ukaingia.

Angekuwa Baily kusingekuwa na uzembe wa aina ile.

Maguire anafanya makosa ya wazi kabisa.
Muongezee mshiko kama De Gea si ninyi matajiri?
 
Nasema hivi tarehe 22 lazima Cheltako walie watka wasitake tunamchakaza West ham alafu tunaisubiria game yao hawa takataka
 
Umeniongezea upeo wa kufikiri kuhusu hii timu.

Nakuunga hoja, nafikiri uchovu si sababu pekee ya sisi kufungwa jana.

Na pia kuna mahali nimesoma OLE akikiri kubugi kwenye team setup.

Hili swala la opposition pressing, ni gumu maana pengine baadhi ya wachezaji tulionao wanaturudisha nyuma.
De gea - poor ball distribution.
Maguire - anachelewa kurelease mpira.
AWB- poor on ball.
Matic - naona kama sio press resistant kivile.
Pogba- yuko slow( center of gravity)
Fred- hana pass za uhakika, ni rahisi kunyang'anywa mpira.

Au hatuna coaches wa kufundisha hiku kitu

Against low blocks,
Ukipata RW creative, CM creative, na Attacking FB, hili litapungua ama kuisha kabisa.

Haya yote yataenda poa kama coaching itakuwa nzuri,
Mfano mara nyingi huwa wana cheza slow sana. Mi naona inasababisha adui ajipange. Kwnn isiwe Quick passing, one touch.

Kama vipi atafutwe coach mwenye uwezo wakufundisha mambo hayo.

Naombea huko Europa, tusonge nusu fainali tukutane na Sevilla, tuone njinsi team itakavyocheza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…