Naogopa kuandika maoni yangu kabla mechi haijaisha ila ngoja niandike tu.
Kama kuna shabiki wa man utd aliahirisha kufanya mambo mengine ya msingi akiamini ligi kuu ya malkia itampatia raha kupitia man utd,afikirie upya kabla muda haujaenda mbali.
Kwa mtizamo wangu,forward line ya man utd ina mentality ya mid table teams na pengine chini ya hapo.
Matatizo ya timu yamekuwa yakihamahama tu,leo beki kesho kiungo na kesho kutwa washambuliaji. Hapa tatizo ni mwalimu hajui anafanya nini.
Ole anaamini katika wachezaji zao la man utd lakini kwa kiasi kikubwa ndio wanaomuangusha na sababu sio uzoefu bali hawajui mpira kwa kwreli. Rashford zaidi ya kukimbia na kusubiri penalty,huoni kingine anachofanya zaidi kama mshambuliaji namba moja wa klabu kubwa kama man utd.
Naamini hatamaliza msimu akiwa mwalimu wa united