Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Former England manager Sam Allardyce says it is possible that Manchester United could be relegated from the Premier League this season. - Talksport
 
nimemfuatilia sana OLEGUNAR nimegundua anakua kocha hatari akiwa hapati matokeo. Atatufikisha tunapotaka.

msimu huu hadi napata marafiki wapya wa kike kisa kunihurumia vipigo nnavyopokea na man u yangu. Naweza kusema hiki ndio nnacho faidi kwa sasa.

Ole at the wheel
 
Mnataka kufika wapi ?
 
Mkuu n matches 8 tu zimepita nahakika tunazama UCL. Au hata through Europa league

#ole apewe muda#
 
Chief klopp imemchukua misimu mitano kufikia hapa why not ole kupewa muda
 
Mkuu n matches 8 tu zimepita nahakika tunazama UCL. Au hata through Europa league

#ole apewe muda#
ndicho tunachokiomba kwa sote na sidhani kama yupo shabiki wa manchester united anayetamani kushuhudia timu ikiendelea kufanya vibaya.

lakini ukiziangalia hizo mechi 8 zilizopita hapakuwepo sababu ya msingi ya kutufanya tupoteze alama 15.
mchezo wa soka hauna rafiki wa kudumu ndio maana kundi hili linaloongoza kampeni ya kumponda OGS nyakati hizi wengi wetu ndio wale wale tulio ongoza kampeni ya kumsifia nyakati zile anafanya vizuri.
 
Chief klopp imemchukua misimu mitano kufikia hapa why not ole kupewa muda
Klopp alishaonesha ni nan kwenye tasnia ya soka

Alishajenga BVB Kali ya kuogopwa ,iliyobeba back to back Bundesliga ,

Nilishuhudia klopp akiinyanyasa baryen iliyokamilika kwa kuipiga 5-0

Klopp aliipandisha daraja Mainz timu ya kijijini kwao kwa Mara ya kwanza ,

Hivo alipowaambia Liverpool wampe miaka 3 aijenge alieleweka

Ole gunar historia yake ya ukocha tuliyonayo aliishusha daraja Cardiff city .
 
hizo hoja zake zote ameshajibiwa na Belo huko nyuma lakini jamaa bado ameendelea kubaki na msimamo huo huo, imefikia nyakati unaweza ukadhani unajadiliana na binadamu mwenye tabia za kasuku.
 
nimebaki naangalia mechi zetu kwa sababu ya mapenzi. Sina imani kabisa na mbinu za kocha, unafungwa goli dakika ya 40 lakini unarudi kipindi cha pili na style ile ile ya uchezaji. Pass nyingi kutoka mid kwenda nyuma. Mpira ukienda mbele tunapoteza, hii ni zaidi ya transition period
 
"nimemfuatilia sana OLEGUNAR nimegundua anakua kocha hatari akiwa hapati matokeo"

Umemaanisha nini hapa exactly??
 
Chief klopp imemchukua misimu mitano kufikia hapa why not ole kupewa muda
Hahahahahaha.....Klopp anaichukua Liverpool October 8 2015,
February 28 2016 Anacheza Final ya kwanza ya League cup
May 18 2016 Anacheza Fainali ya pili ya Europa league
Kocha wa hivi unaweza kushindwa kumpa muda.
Acha kumvunjia Jurgen klopp bana.Jiheshimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…