Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man U - 159M - Point 5
Chelsea - OM - Point 5

Kuna tatizo mahali
Kwanza unaamini huu msimamo ndio una reflect uhalisia

Kama una amini hivyo, basi tatizo lipo

Kama unaamini Cristal Palace aliyetumia £0 kwenye usajili ataendelea kuwa hapo alipo, tatizo litakuwepo

Kama unaamini Liverpool aliyetumia chini ya £20m ataendelea kuwa juu ya City aliyetumia £75m ujue tatizo lipo

Kama unaamini United atabaki hapo alipo (namba 8)na Chelsea atabaki hapo alipo (namba 11) ujue tatizo lipo

Au mkuu ulitaka tuangalie Chelsea na United tu, bila kuangalia big picture

Ligi ni kama mbio za marathon mkuu, sio kila aliye mbele dakika mbili za mwanzo atamaliza akiwa mbele na si kila aliye nyuma atamaliza wa mwisho. Nakumbuka mara ya mwisho Chelsea kuchukua EPL ilikuwa chini ya Conte, timu ilianza ligi vibaya mno
 
pia anaweza akatokezea muhuni akasema hata nyakati zile leicester city anaongoza ligi wakajitokeza mashabiki na maneno kama hayo mwisho wa ligi leicester akawa bingwa.
 
Tatizo lako wewe huwezagi kujenga hoja bila kutafuta Excuse ya sapoti kwa timu nyingine,Itetee Manchester United bila mgongo wa timu nyingine.
 
Kwenye Chelsea hapo usiiwekee dhamana , anaweza kubaki maeneo hayo hayo hadi ligi inaisha .
 
Leta stats zake ili tumlinganishe na wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…