teh teh teh
nimeiangalia video kwa sekunde 20 nimeachana nayo na si kwamba sina bando la kutosha.
mkuu nimegundua unashabikia liverpool baada ya kufanikiwa kuziona comment zako kwenye uwanja wenu wa anfield.
je Aron Wan Bissaka anamzidi
trent alexander arnold kiuwezo?
naomba uwe mkweli kwenye majibu
msimu uliopita tumemtukana
ashley young kwa kukosa kwake uwezo wa kushambulia hususan uwezo wa kupiga krosi za uhakika kuwa ni dhaifu cha ajabu tunamleta tena ndugu yake huoni kama ni kituko cha karne tunachoelekea kukifanya.
huo mpira wa kujiweka nyuma muda wote kama sungura mwenye mimba hata shomari kapombe anao uwezo wa kucheza style hiyo, unapolipa paundi millioni 50 kwa mlinzi wa pembeni anapaswa awe na sifa za kulinda na kupandisha mashambulizi kama walivyo walinzi wengine tuliowahi kuwashuhudia kama vile dani alves, marcelo wa misimu miwili iliopita, alexandro kutoka juve, robertson kutoka liverpool n.k
diogo dalot ana uwezo mkubwa wa kushambulia lakini uwezo wa kujilinda ni mdogo
ashley young amepoteza muelekeo (hawezi kulinda kwa nidhamu wala kushambulia)
aron wan bissaka uwezo wake ni kulinda tu.
kwa maarifa yangu dhaifu kwa mpira huu wa kisasa ujio wa aron wan bissaka itakuwa bado hatujatatua tatizo kwa sababu jukumu la mashambulizi litaendelea kubaki kwa winga.
kwa anayeamini ya kwamba aron wan bissaka atabadilika naomba abaki na imani hiyo mpaka ila mimi siamini kama jamaa atabadilika na sababu kubwa ni aina ya mwalimu tulienaye ni muumini wa pressing kwenye interview.
View attachment 1133351