Daaa hao wahuni wana zali sana
 
Wewe jamaa nadhani hunijui vizuri kwenye huu Uzi wa timu yangu pendwa kutoka mitaa ya Great Manchester pale Jijini Manchester.

Ambacho kimenishangaza zaidi ni tabia zako za "Kimwajuma mwajuma" kuleta mambo ya Forex kwenye kabumbu la wanaume wa shoka. Sasa basi kwasababu umekuja "Kijuma lokole" Mimi huwa siungi mkono huo ujio wa namna hiyo.
Na kwasababu umeamua kuhamisha mjadala kutoka kuwa mjadala wa kikabumbu na kuufanya mjadala kuwa wa mashambulizi binafsi dhidi yangu, nakuomba kabla sijaandaa makombora ya Ballistic missile kuja kukusasambua ufanye yafuatayo;

1. Naomba unitake radhi kwa kunihusisha Mimi na forex katika Uzi wangu huu pendwa


2. Nakuomba ufute kauli yako kwamba mimi nimewahi kusema Forex ni utapeli


3. Nakuomba ufute kauli yako kuwa Mimi Nina chuki binafsi na Mourinho ..


Nimejijengea heshima kubwa katika forum hii , sitakubali "Mpuuzi " yoyote Mwenye akili za "Kimilembe milembe" , kwasababu tu ya kumiliki smartphone na bundle la chuo anichafue. Sitakubali.


Sasa mimi ninaweka notification on ili nisubiri utakachoandika ili nikubalase kisawasawa mpaka utakapokuwa unaona hii ID uwe unasema "Shikamoo" .




Wahedi wewe.
 
Ha ha haaa...mkuu nitafasirie neno "wahedi wewe" limeniacha junction isjekuwa tusi ndug....
 
Ed Woodward: "Preparations for the new season are underway and the underlying strength of our business will allow us to support the manager and his team as we look to the future."
Yan haya maneno inaonyesha ni jins gani anawaza biashara zaid kuliko performance ya team. Business? What the hell? Haya maneno anaongea kila mwaka ila nothing new
 
Kama ni mambo ya kuanza upya bila kutegemea wachezaji wakubwa,tungembakisha van gaal,huyu ole sioni mahali akitupeleka kwa kikosi kisichokuwa na uzoefu.

Ole anaweza akizingatia vizur eneo la kiungo beki na center foward rashford na martial bado sana viungo wawili wa maana tia na bek nne na tano wa maana shaw na dalot sina wasiwasi nao ole anasimama bila hivyo ni kichapo tu
 
Waingereza watamfukuzisha kazi Ole.

Hakukuwa na haraka ya kuongeza mikataba haraka vile.

Mambo yote yalitakiwa yafanyike mwisho wa msimu.

Tufukuze beki yote tumuache Lindelof na Shaw.
 
Posibility ya kurudi ni kubwa Sancho anagoma kuja United sabubu haiko Champions league
OGS alimfundisha Zaha Cardiff City alivyocheza kwa mkopo na alikuwa anamsifia sana
Tunamhitaji Umtiti, Dyabala, Ayoze Perez na Eriksen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…