Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakuu mnazikumbuka 4G za Mou mwanzoni mwa msimu lakini?... Kuweni na akiba ya maneno hata kidogo mana naona mshaanza tayari
 
Lukaku anafit kwenye hii timu kweli??...why tusimwamini hata sanchez upfront??

Binafsi siioni nafasi yake,lakini ngoja tuone kocha akimpa nafasi atafanya nini??
Upfront ni Rash mkuu. OG anawapa nafasi watoto wa academy. Sanches atacheza wide role aki-altenate Lingard.
 
Bora wewe umenena vyema Mkuu, afu hii staili ya kuongea sana kumbe Man U nao huwa wanayo?

Mi nadhani Arsenal ndiyo huwa wanayo kumbe hadi hawa mashetani wekundu?
Nitajie mechi ambayo Mourinho aliongoza team kushinda magoli matano.

Ukinitajia hiyo mechi naihama Manchester nakuwa shabiki mnazi wa Burnley
 
Ukiisoma hii interview unaona tofauti ya yule jamaa na Huyu wa sasa.
 
Kumbe wewe ni Chelsea

Pole sana, MPE salamu Vardy.
 
Wakuu mnazikumbuka 4G za Mou mwanzoni mwa msimu lakini?... Kuweni na akiba ya maneno hata kidogo mana naona mshaanza tayari
Tunazikumbuka ila hazikuwa msimu huu. Zilikuwa msimu wa 2017/2018, mwaka ambao Lukaku alisajiliwa. 4G kwa msimu huu was 2018/2019 ni ile ya 4 kwa 1 dhidi ya Fulham pekee.
 
Tunazikumbuka ila hazikuwa msimu huu. Zilikuwa msimu wa 2017/2018, mwaka ambao Lukaku alisajiliwa. 4G kwa msimu huu was 2018/2019 ni ile ya 4 kwa 1 dhidi ya Fulham pekee.
Mkumbushe pia hata kama tulikuwa tunashinda nne hatukuwahi kucheza mpira mzuri kama tuliocheza jana,aache kubwabwaja na kujitoa akili!
 
Ukiisoma hii interview unaona tofauti ya yule jamaa na Huyu wa sasa.
Hapa kanifurahisha sna kamsifia hapa lazima mchezaji aongeze juhudi maana kocha anamuangalia ujue macho ya wengi ni kwa namna gani pogba atatumika hapo sanchez hajarud kwa spid ya jana tungekuw nae had 7 tungeshind

So he's got quality to play many positions and today I thought he did excellent.
 
Nakumbuka mwanzoni mwa msimu tuliwahi kujadili na wewe kuhusu ubora wa wachezaji kama Rashford, Martial na Pogba, tukisema hawa wachezaji wangekuwa chini ya kocha mwingine tungewaona ni top class.

Ndicho kinachoenda kutokea.
 
Kweli mkuu jana walijiachia sana nawaza kama bodi ingekubali martial auzwe kwenda chelsea kisha tumchukue willian walahi ilikuwa biashara kichaa kwa upande wetu maana willian 30+ halafu martial under 24 chelsea wangefaidika sana kwa mpira aliocheza jana alikuwa vizur sana tukiimarisha na upande wa mabek mwanga unaonekana.
 
Kuna issue ya Technical Skills na Management Skills, kuwa manager mzuri ni zaidi ya kuwa na technical skills. Mara nyingi sana makocha huwa wanazidiwa mbinu na wasaidizi wao, ila wasaidizi wanachokosa ni hiyo Management Skills, kwa hiyo wanaendelea kuwa wasaidizi.

Angalia hata maofisini, wale watu ambao ni mabosi siyo kwamba ni wazuri sana utendaji isipokuwa ni ujanja wa kiuongozi. Kazi wanafanya wengine yeye anaiwasilisha kama ndiye aliyeifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…