Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mi nimeongeza ya pili na liverpool

Liverpool kwa tactics za Mourinho sidhani kama mnahitaji kuiogopa, kiuhalisia Man Utd haiko kwenye ubora kwa EPL, na bado imestruggle UEFA vs Valencia na Juve, halafu uje useme eti ni Barca tu ndo wa kuwaogopa?

Hapo kuna teams kama Dortmund, PSG, Madrid (ingawa nao ni tia maji tia maji), Juventus.

Hapo sijazitaja teams za EPL.

Labda kama tunaongea kishabiki na si kimpira.
 
Nakubali, lakini kwa kiwango alichonacho Man Utd ya sasa huwezi kusema eti wa kumwogopa Ulaya ni Barca pekee!

Hiyo ndo kauli ninayoikataa.
uliangalia hizi games against United??
Tottenham
Chelsea
Juventus......tulipoteza though, ila commitment ilikuaje??

United ya msimu huu ikikutana na timu ndogo ndo inakuwa kama zezeta ila si kwa wakubwa wenzao kama huamini suburi game ya City na Juve
 
Mpira ungekuwa hivyo basi hata chelsea ungemfunga wewe upo uefa yy yupo europa
 

Game zote hizo nimeziangalia, labda niulize swali, kuna timu kubwa ambayo mmeifunga msimu huu?
 
Nakubali, lakini kwa kiwango alichonacho Man Utd ya sasa huwezi kusema eti wa kumwogopa Ulaya ni Barca pekee!

Hiyo ndo kauli ninayoikataa.
Kufungwa kupo, sometimes ni incidental. Mechi ya Juve Man iliingia uwanjani na woga. Juve hata km ni wazuri si timu ya kuogopwa na Man U kiasi cha kuingia uwanjani na hofu na kucheza defensively. City kadhalika ni wazuri lakini hatupaswi kuingia uwanjani ukiwaogopa as if ni timu kuubwa!!
 
Mpira ungekuwa hivyo basi hata chelsea ungemfunga wewe upo uefa yy yupo europa

Hatuzungumzii bahati mkuu, tunazungumzia kiwango cha timu.

Mara chache kuna kitu tunasema mpira unadunda, na chochote kinaweza kutokea ndani ya dakika 90.

Pamoja na hizo kauli, bado ubora wa timu ndo unaoweza kufanya timu ijiamini kukutana na timu zingine, haitakiwi ijiamini kwa kutumia bahati.

Chelsea ni unbeaten mpaka sasa kwenye mashindano yote, yeye kuwa Europa haishushi ubora wake, kwa sababu kwanza Europa au Uefa inakuwa determined na results za msimu wa nyumba, na kama unavyojua timu zinafanya mabadiliko off season na kuwa na viwango tofauti. So Liverpool siyo kubwa kiviwango kwa Chelsea.
 
True ile gemu ya Juve tulishindwa tu kujiamini..tungepata hata sare.
 

Kuna kutoogopa kwa sababu nyingi:-
  • Una kikosi kizuri ambacho una uhakika kwamba ni bora kuliko mpinzani unayeenda kukutana naye.
  • Una kikosi kibovu na umeshazoea kufungwa, huogopi kufungwa na uko kwenye status ya liwalo na liwe.
  • Matokeo yoyote utakayoyapata hayaleti tofauti yoyote.
So, nitaomba uniambie game yenu na Juve hamkupaswa kuiogopa kwa sababu gani?
 
kwa jibu la sasa hapana, ila hili swali sidhani kama ni muda sahihi wa kuliuliza

Probably siyo muda sahihi, ila hii discussion imeibuka baada ya mdau mmoja kusema kwamba Man Utd inatakiwa kumwogopa Barca peke yake Ulaya.

Nadhani yeye yuko kwenye nafasi nzuri kunijibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…