Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mourinho bado yupo Old Trafford??..No way!!!!

Ingetakiwa awe anauza sambusa kwao Madeira Ureno
 
Kuna mido ya Serbia ya kuitwa Sergej Milikovic Savic,vuta iyo inataka sana kuja
 
Huyu ni mtu wa kukaa pa pogba ujue kiachotuchanganya ni vile matarajio tuliyowekeza kwa pogba na hata wachezaj wenzio lakin kiwango anachokionesha ni duni sana.
Ngangari sana iyo,inakichafua sana kati unaweza hata kuifanya back up ya matic au ukaitaftia dimba no 8 Pogba akafanye mbwembwe zake no 10
 
Mkuu timu yetu inayumba na factor nyingi sana kama ni makocha tushafukuza cha msingi tupunguze kuwa timu ya wauza jezi bodi iyajue majukum yao hii ya kuvutana na kocha haitatuacha salama.
Ni kweli Mkuu ila alipo fika Mou anastahiri afukuzwe na tufanye double recruitment ya kocha na director of football.....
 
Ni kweli Mkuu ila alipo fika Mou anastahiri afukuzwe na tufanye double recruitment ya kocha na director of football.....
Mkuu aachwe najua anajua madhaifu yetu kwa sasa ni bora kumuacha apewe fungu atatue matatizo yetu angalia timu alizopita na wachezaj aliowaacha kaacha misingi imara sana mourinho anajenga timu mi nataka ajenge timu kisha apewe giggs tu
 
Mkuu aachwe najua anajua madhaifu yetu kwa sasa ni bora kumuacha apewe fungu atatue matatizo yetu angalia timu alizopita na wachezaj aliowaacha kaacha misingi imara sana mourinho anajenga timu mi nataka ajenge timu kisha apewe giggs tu
Mkuu Radika ......... Timu kiufundi iko vibaya sana Tactical display za Kocha hamna ......... Manchester United wanacheza mpira wa ovyo kama kuku aliyekatwa kichwa Kuna timu zina average players lakini zinacheza mpira Mkubwa kuliko Manchester hii ya Jose kwa sababu tu ya kuwa na Manager mwenye Tactical display.
 
Mkuu hapa ukiangalia timu yetu haina nidhamu pogba alianza kusumbua tokea alipowekwa bench siku alicheza vibaya na spurs pale alikasirika mech ya liverool alikaa tena bench akacheza scott sasa tokea hapo akaanza vituko yeye nani asikae bench mkuu akicheza hovyo? Hawa wachezaj wa kawaida wa timu ndogo wanacheza kwa umoja na nidhamu sisi hamna hivyo vitu ukiangalia martial aliambiwa kabisa afanye juhuzi kuboresha kiwango chake hatak anataka kuondoka sasa nidham iko wap ya mchezo wakat sane jana kaambiwa na pep anatakiwa kukaza sasa kwa kile kiwango cha sane bado anaambiwa akaze sisi vipi martial? Juzi pogba anamjibu hovyo kocha mbele ya madogo na wachezaj wenzie huoni kama analeta mtafaruku ndani ya timu? Ifike mahala wachezaj wetu watambue wanavyotakiwa kuipigania timu hata kipind cha sir alex hatukuwah kucheza mpira wa barcelona ila nidham na kumheshimu kocha na mbinu zake zilitufikisha hapa tulikuwa na wachezaj kawaida tu ila wapambanaji sana angalia kwa mfano burnley wanavyocheza kwa nidhamu kwamba kocha wa burnley ni mzur zaidi ya mourinho? Wachezaj wa burnley ni wazur zaidi ya pogba? Ukivimba kichwa utapotea tu takwimu zainaonesha ktk timu za top 6 pogba ndio kiungo anaeongoza kwa kuporwa na kupoteza mipira sasa hapa timu inachezeje ikiwa kiungo kinapotea hivyo wakat ndo injini ya timu???
 
Kuna mahali nimeona wamepiga kura nani aondoke kati ya Mou au Pogba. Asilimia 60 wanataka Pogba afurumushwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…