Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Timu ambazo Pep na Klopp wanapita kama wanateleza,sisi tunaacha point plus mpira mbovu,je hili nalo lilihitaji CB mzuri kulirekebisha?
Ulinganifu wa wachezaji wa Mou na city ya Pep ulitakiwa kuwa kwenye mechi kati yao au miongoni mwa top 6 na si BHA na wenzie.
Kwa mtizamo wangu mimi,ndani ya miaka 3 ya Mou,hakuna eneo la uwanja ambalo tumekamilika na tunaweza kujivunia kupata matokeo licha ya ubora wa wachezaji tulionao.
 
Kwenye mpira Wa miguu huwa hatutoi fact ya "angekuwa flani asingekosa" kwa sababu kuna magoli anakosa ronaldo na Messi na unabaki umeduwaa amekosaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu umekosea sehemu moja tu pale uliposema mourinho amesababisha mgawanyiko kwa mashabiki kati ya Mou na ED Woodward. Ni kwamba Mou kasababisha mgawinyiko kati ya wanaomuunga mkono yeye na wenye uchungu na Manchester United japo hatutoi senti ingawa kwa upande wangu kila msimu ni lazima ninunue jezi mpya ya Man U kwa elfu 25 au 30 pale Dar es salaam japokuwa naishi Mwanza, japo sijui kama huwa wanafaidika na mimi au la. Na kuna kipindi tushawahi kukwaruzana kidogo juu ya huyu Mou. Kwingine kwote ulikoandika ni sahihi tena umeonyesha emotion ya hali ya juu na nimekuingiza kwa kundi linaloipenda Man U toka moyoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ahsante sana kumbe nilipaswa niseme ni vita kati ya timu mourinho na timu wapenzi wa kudumu wa manchester united na si team ed woodward.
unajua upande wangu nilipenda manchester united tokea nina miaka 7 sasa ninapoona tuna mwendo usioeleweka japo sina mchango mkubwa zaidi yako huumia sana.
tunadhalilika sana mtaani.
mkuu lakini utakaposoma andiko langu la mwisho utabidi univumilie.
mwili wangu una nafsi mbili
hahahahahahaaa
ahsante sana
 
Mkuu radika Mou huwa anapenda sana kuwa na rundo la wachezaji hata asiowatumia. Na kitu alichoambiwa na bodi ni kuhakikisha ana offload baadhi ya wachezaji asio na manufaa nao kabla ya kuomba hela ya kuongeza wengine. Yeye hilo hakulifanya sasa watu watakuwa wanatoa hela tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaffload vip bila kwanza kuwa na uhakika wa kuingiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…