Manchester United (Red Devils) | Special Thread

waangalie vizuri wasilete ushabiki
Hili goli la wazi kabisa hata mimi nafunga...msitetee upupu hapa alichosita kupiga nini alipatwa na maruweruwe au mzimu wa wenger ulimjia.....anapata tabu huyu jamaa dah na nina uhakika kule arsenal angecheza sana maana alikuwa amezungukwa na mafundi ila hapa atatundika daluga mapemaaaaaaaaaaa maana waliomzunguka ni utoto na ushubwada mtupu kina martial hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Maneno ya kishabiki tu kwani huko ARSENAL ALIKUWA AKOSI MAGOLI
Anafunga kila mechi
 
Newcastle jana walicheza mpira swafi kabisa walikuwa wanapiga pasi zinaonekana na wala hawakupaki basi timu ilikuwa inasogea mbele inaonekana ..........
 
Box to box ni kama Artulo Vidal yule aliyemfanya pogba ang'ae juventus
 
Mkuu ule ni mfumo wa kujilinda 4231 unapata goli la haraka unaanza kuzuia kucheza counter atack hawa newcastle wakujinda kweli?

Halafu najiuliza sana sawa pogba hatendewi haki ina maana hata jonjo wa kumpoteza?
Mkuu jonjo ni complete midfielder tatzo nyota tu
 
Mimi ndio nimeuliza swali, naomba majibu kwanza ndio uulize swali lako!!
Swali nililokuuliza ndio jibu lako. Jana tumecheza na double number 6 ( matic na Pogba ) ... Lingard alikuwa false number 8.... Alexis Sanzez alikuwa namba 11 ila hakuwa natural namba 11... Muda Mwngi upande wa winga ya kushoto alikuwa anacheza Ashley young kama WING BACK ( beki wa kupanda na kushuka).



Una lingine ????.
 
Pogba ni mzuri akipiga 10 hakika,ila chini yake wawepo watu wa maana ,kumbuka juve kulikuwa na watu mfano pirlo na vidal ila hapo dah mtamlaumu sana........wacha KDB aupige mwingi hivi unajua shughuli inayopigwa na kina FERNANDINHO pale chini?unaachaje kung'aa kwa mfano?
 

Mi hapo ndo nnapochokaga kiungo hadi tumnunulie watu wa kumsaidia ili ang'ae shida ipo mahali sasa atatengeneza vipi ufalme wake? Ukiwa umesajiliwa kwa mapesa mengi kuna Muda unatakiwa kuibeba timu haijalishi mazingira gan tukirud kwenye mpira tuweke pembeni ushabik.
 

Ndugu hilo goli ni gumu alishakuwa kwenye angle kufunga hapo ni bahat tu ila la martial ndo goli la wazi alikuwa anaona na kipa alex alishatoka pembeni kwa macho upo vizur hizo goli ungefunga nyingi sana ungebeba viatu vya dhahabu kila uchwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…